0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ZAKA YA DHAHABU NA FEDHA NA PESA ZA KARATASI

SOMO LA FIQHI

Maana ya Dhahabu na Fedha

Dhahabu na fedha, na chochote kinachosimamia nafasi ya vitu hivi viwili miongoni mwa pesa za karatasi zinazotumiwa siku hizi.

Suali: Ni ipi Hukumu ya Zaka ya Dhahabu na Fedha?
Jawabu: Hukmu ya zaka ya Dhahabu na Fedha ni lazima, kwa kauli ya Mwenyezi Mungu Mtukuf:

{وَالَّذِينَ يَكْنِزُونَ الذَّهَبَ وَالْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِي سَبِيلِ اللَّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ}   التوبة:34

[Na wale wanaokusanya dhahabu na fedha wala hawazitoi katika njia ya Mwenyezi Mungu, wape habari za adhabu inayoumiza]   [ At-Tawbah 34]

Na kwa kauli ya Mtume ﷺ:

مَا مِنْ صَاحِبِ ذَهَبٍ وَلَا فِضَّةٍ لَا يُؤَدِّي مِنْهَا حَقَّهَا إِلَّا إِذَا كَانَ يَوْمُ الْقِيَامَةِ صُفِّحَتْ لَهُ صَفَائِحَ مِنْ نَارٍ فَأُحْمِيَ عَلَيْهَا فِي نَارِ جَهَنَّمَ فَيُكْوَى بِهَا جَنْبُهُ وَجَبِينُهُ وَظَهْرُهُ كُلَّمَا بَرَدَتْ أُعِيدَتْ لَهُ فِي يَوْمٍ كَانَ مِقْدَارُهُ خَمْسِينَ أَلْفَ سَنَةٍ حَتَّى يُقْضَى بَيْنَ الْعِبَادِ فَيَرَى سَبِيلَهُ إِمَّا إِلَى الْجَنَّةِ وَإِمَّا إِلَى النَّارِ      رواه مسلم

[Mtu yeyote atakae kuwa na Dhahabu na fedha na wala haitolei Haki yake (zaka) itajaaliwa kama vinoo ambavyo atapigwa navyo kwenye migongo na vipaji kila akipata ubaridi (yakipoa makali ya moto) anaregelewa tena (kupigwa navyo), mpaka Allaah Amalize kuhukumu waja wake siku ambayo ni sawa na miaka elfu khamsini. Kisha ndio ataoneshwa njia yake ikiwa kama ni ya peponi au motoni]     [Imepokewa na Muslim.]

Suali: Ni yapi Masharti ya kuwajibika kutolewa kwa zaka ya Dhahabu na Fedha?

Jawabu: Masharti yanayo wajibika kutolewa zaka za Dhahabu na Fedha ni haya yafuatayo:

1. Kupitiwa na mwaka.

2. Kuzimiliki kiukamilifu.

3. Kufika nisabu ya zaka.

Suala: Ni ngapi Nisabu ya zaka ya Dhahabu na Fedha?

Jawabu:

1. Nisabu ya dhahabu ni Dinari ishirini (85gms)

2. Na Dinari moja ya dhahabu = (ina dhahabu) gramu nne na robo, hivyo basi inakuwa nisabu ya dhahabu kwa gramu 4.25 x 20 = 85gms za dhahabu safi (ambayo haikuchanganywa na kitu).

3. Nisabu ya fedha ni Dirham mia mbili (595 gms)

Na Dirham moja ya fedha = (ina fedha) 2.975gms, hivyo basi inakuwa nisabu ya fedha kwa gramu = 2.975 x 200 = 595gms za fedha safi.

Mfano: Ikiwa gramu moja ya dhahabu = inauzwa Dolari 30, basi inamlazimu mtu kutoa zaka ikiwa amefikisha 85 x 30 = Dolari 2550 dolari.

Suali: Ni kiwango kinachofaa kutolewa zaka ya Dhahabu na Fedha
Jawabu: Kiwango kinachomlazimu mtu kutoa zaka katika dhahabu na fedha na stakabadhi za kiashirio cha pesa ni robo ushuri = 2.5%.

Basi kwa kila Dinari ishirini ya dhahabu atatoa zaka nusu Dinari, na itakayozidi (zaidi ya Dinari ishirini) itapigiwa hisabu, iwe imezidi kidogo au sana.

Na kwa kila Dirhamu mia mbili za fedha atatoa zaka Dirhamu tano, na kitakachozidi atakipigia hisabu; kwa kauli ya Mtume ﷺ: (Ikiwa unamiliki Dirhamu mia mbili, na zimekamilisha mwaka, basi yatakiwa utoe Dirhamu tano, na si juu yako kutoa chochote – yaani – katika dhahabu mpaka umiliki Dinari ishirini, basi ukiwa na Dinari ishirini, na umemaliza nazo mwaka, basi itakulazimu utoe nusu ya Dinari, na zitakazozidi utafanya kwa hisabu hii) [Imepokewa na Abu Daud.]

MFANO WA KUFAHAMISHA:

Mtu anamiliki Dolari 9000, na imepita mwaka mzima hali ya kuwa anazimiliki hizo pesa, je analazimika kutoa zaka?

Kwanza: Tutahisabu nisabu ya zaka kwa mtizamo wa dhahabu au fedha kama ifuatavyo:

Nisabu = Gramu thamanini na tano katika dhahabu safi = 85 x bei ya gramu moja ya dhahabu safi (inavyouzwa) siku ile ya kulazimika kwake kutoa Zaka, na tukisie kwamba gramu moja yauzwa = Dolari 30.

= 85 x 30 = Dolari 2550.

Kwa hivyo Nisabu yake = Dolari 2550, hivyo basi itakuwa mali ya mtu huyu imefika nisabu, na imekamilisha mwaka mzima, kwa hivyo inamlazimu kutoa zaka.

Pili: Tutahisabu kiwango anachofaa kutoa zaka kama ifuatavyo: –

Kiwango cha kutolewa zaka = 2.5%.

= 9000 x 2.5/100 = Dolari 225.

Kwa hivyo huyu mtu yafaa atoe kutoka kwa mali yake Dolari 225 kama zaka.

Suala: Je mtu anafaa kuchanganya Dhahabu na Fedha pamoja ?

Jawabu: Mtu anapo miliki dhahabu na fedha lakini zikawa hazifikii kiwango cha kutolewa zaka, kauli yenye nguvu ni kuwa hatowajibika kutoa zaka, wala hata zikikusanywa pamoja ili zifikiye kiwango, kwani uwajibu ni kutoa dhahabu pekeyake na fedha pekeyake kwa sababu ni vitu viwili tofauti, na hakuna dalili ya kuzikusanya pamoja ili ifikie kiwango, na kwa neno lake Mtume:

[لَيْسَ فِيمَا دُونَ خَمْسِ أَوَاقٍ صَدَقَةٌ]    رواه البخاري ومسلم

[Hakuna chini ya wakiya tano zaka]   [Imepokewa na Bukharin a Muslim]

Na atakae zikusanya dhahabu na fedha itakuwa amewajibisha zaka chini ya wakia tano.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.