SOMO LA FIQHI
Suali: Ni zipi waajibati za Swala?
Jawabu: Ni lile jambalo ambalo ni wajibu kulifanya au kusema katika Swala,na lau mtu ataacha kwa kukusudia basi swala yake inabatilika,ama aleacha kwa kusahau analazimika kusujudu sijda mbili za kusahau.
Nazo nikama zifuatavyo:
1. Takbiri za kuhamia kutoka kwenye kitendo kwenda kwenye kitendo kingine.
Kwa hadithi iliopokewa na Anas radhi za Allah ziwe juu yake Amesema Mtume:
[إنما جُعلَ الإمامُ ليؤتمَّ به، فإذا كبَّر فكبروا] رواه البخاري ومسلم
[ Hakika amewekwa imamu ili afuatwe, akipiga takbiri (akisema Allahu Akbar) na nyiyi pigeni takbiri (kwa kusema Allahu Akbar) [Imepokewa na Bukhari na Muslmu]
2. Kusema SUBHANA RABIYAL ADHIIM “Kutakasika ni kwa Mola wangu Mkubwa”.
Kwa hadithi iliopokewa na Hudheyfa radhi za Allah ziwe juu yake Amesema:
[فكان يقول في ركوعه: سبحان ربي العظيم] رواه البخاري والنسائي والترمذي وأحمد
[Alikuwa (Mtume) akisema katika Rukuu “Kutakasika ni kwa Mola wangu Mkubwa”]
[Imepokewa na Bukhari na Al Nnasaai na Al Ttirmidhiy na Ahmad]
3. Kusema SAMI’A LLAHU LIMAN HAMIDA “Mwenyezi Mungu Amemsikia mwenye kumsifu” kwa imamu na kwa mswali pweke, ama maamuma hakuwekewa na Sheria kusema neno hilo.
Kwa hadithi iliopokewa na Abuu Hureyra radhi za Allah ziwe juu yake kutoka kwa Mtume ﷺ:
[ثم يقول: سمع الله لمن حمده إذا رفع صلبه من الركوع] متفق عليه
[kisha Aseme :Mwenyezi Mungu Amemsikia mwenye kumsifu anapo inuwa mgongo wake kutoka kwenye rukuu.] [Wameafikiana Bukhari na Muslim.]
4. Kusema RABBANAA LAKAL HAMDU “Mola wetu! Na sifa njema zote ni zako” katika kuitadili kutoka kwenye rukuu.
Na hili ni kwa Imamu na Maamuma na anaeswali pekeyake.
Dadili ya kusema hilo kwa Imamu na anaeswali pekeyake ni hadithi ya Abuu Hureyra radhi za Allah zifikie yeye asema Mtume ﷺ:
[ثم يقول وهو قائم: ربنا ولك الحمد] متفق عليه
[Kisha aseme hali yakuwa amesimama:”Ee Bwana wetu ni zako sifa njema”] [Wameafikiana Bukhari na Muslim]
Ama dalili ya kusema hilo kwa Maamuma ni hadithi iliyopokelewa na Anas radhi za Allah ziwe juu yake asema Mtume ﷺ:
[وإذا قال: سمع الله لمن حمده فقولوا: ربنا ولك الحمد] متفق عليه
[Na (Imamu) anaposema “Samiallahu liman Hamida” basi semeni “Rabbanaa lakal hamdu“] [Wameafikiana Bukhari na Muslim]
5. Kusema SUBHANA RABBIYAL A’LAA “Kutakasika ni kwa Mola wangu Aliye juu” katika sijida.
Kwa hadithi iliopokewa na Hudheyfa radhi za Allah ziwe juu yake Amesema:
[ثم سجد فقال:سبحان ربي الأعلى] متفق عليه
[Kisha (Mtume ﷺ) akasujudu akasema:Ametakasika Mola wangu aliyejuu]. [Wameafikiana Bukhari Muslim]
6. Kusema RABBIGH FIRLIY “Mola wangu ! nighufirie” baina ya sijida mbili.
Kwa hadithi iliopokewa na Hudheyfa radhi za Allah ziwe juu yake Amesema Alikuwa Mtume akisema (kati ya sijda mbili)
[ربِّ اغفر لي، ربِّ اغفر لي] رواه أبوداود وإبن ماجة
[Mola nisamehe, Mola nisamehe] [Imepokewa na Abuu Daud na Ibnu Maajah]
7. Kukaa kikao cha Atahiyatu ya kwanza.
Kwa hadithi iliyopokelewa na Abdillah bin Buhayna asema:
قام في صلاة الظهر وعليه جلوس، فلما أتم صلاته سجد سجدتين يكبر في كل سجدة وهو جالس، قبل أن يسلم وسجدهما الناس معه، مكان ما نسي من الجلوس متفق عليه
[Alisimama (Mtume ﷺ) katika swala ya Adhuhuri na alikuwa akae,alipo timiza swala yake alisujudu sijda mbili akipiga takbira kwa kila sijda hali yakuwa amekaa kabla hajatoa salamu na watu wakasujudu pamoja na yeye,sehemu aliyo sahau kukaa] [Wameafikiana Bukhari na Muslim]
8. Kuleta Atahiyatu ya kwanza.
Kwa hadithi ya Abdullah bin Mas’udi radhi za Allah ziwe juu yake asema ametufundisha Mtume wa Mwenyezi Mungu tuseme tunapo katika rakaa mbili:
التحيات لله، والصلوات، والطيبات، السلام عليك أيها النبي ورحمة الله وبركاته، السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله، وأشهد أن محمدًا عبده ورسوله رواه النسائي وأحمد
[Maamkuzi mema, na rehema na mazuri yote, ni kwa Mwenyezi Mungu, amani zishuke juu yako Ewe Mtume na rehema za Mwenyezi Mungu na baraka zake, amani ishuke juu yetu, na juu ya waja wa Mwenyezi Mungu walio wema, nakiri kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwahaki ila ni Mwenyezi Mungu na ninakiri kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake.] [Imepokewa na Annasaai na Ahmad]
TANABAHISHO
Kigawanyo hiki cha wajibati za Swala ni kwa madhehebu ya Imamu abuu Hanifa na Imam Ahmad, ila ma-Hanafi hawaoni kuwa mwenye kuacha wajibu kwa kusudi inabatilisha Swalah yake bali yeye amefanya madhambi anayostahiki adhabu. Ama katika madhebu ya Imam-Maaliki na Imamu-Shaafi’y hawana kigawanyo hichi cha Waajib kwao ila wao wana nguzo na Sunnah kwa ujumla wake.
Na pia kuna wanaosema kuwa kusema “Amin”baada ya kusoma Suratul Fatiha ni katika wajibat za Swala.Kwa kuthubutu hilo katika Swala zote za Bwana Mtume ﷺ.