0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SUNNA ZA ADHANA

SUNNA ZA ADHANA

Kumesuniwa katika adhana kufanya mambo yafuatayo:-

1. KUELEKEA QIBLAH:

Ni sunna kwa muadhini kuelekea Qiblah wakati wa kuadhini, kwa sababu bora ya pande za kuelekewa kwa ajili ya ibada ni upande uliyoko Qiblah.

Na isitoshe imethibiti kwamba waadhini wa Bwana Mtume Radhi za Allah ziwe juu yao walikuwa wakielekea Qiblah wakati wa kuadhini.

2. KUTWAHIRIKA KWA MUADHINI KUTOKANA NA HADATHI MBILI:

Ni suna mtu kuadhini hali ya kuwa yu katika hali ya twahara, yaani hana hadathi ndogo inayompasishia udhu wala ile kubwa inayompasishia josho.

Kwa Hadithi ya Ibnu Abbas Rahi za Allah ziwe juu yake amesema:

[إن الأذان متصل بالصلاة فلا يؤذن أحدكم إلا وهو طاهر]      تلخيص الخبير

[Hakika Adhana imeunganishwa na Swala asiadhini mmoja wenu ila na yeye ni Twahara]   [Talkhisul Khabir]

Na Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ:

[إني كرهت أن أذكر الله إلا على طهر]   رواه أبوداود وإبن ماجة

[Nachukia (sipendi) kumdhukuru Allah Mtukufu ila niwe na twahara].   [Imepokewa na Abuu Daawoud na Ibnu Maajah]

3. KUADHINI HALI YA KUWA AMESIMAMA:

Ni sunna mtu kuadhini hali ya kuwa amesimama.

عن أبي قتادة أن النبي-صلى الله عليه وسلم- قال لبلال:[قم فأذن]     رواه البخاري ومسلم

Amepokea Abuu Qatada radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume ﷺ Alimwambia Bilaali [Simama uadhini]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Lakini Ikiwa mtu ana udhuru kama ugonjwa akisimama ataanguka au maumivu yatazidi, basi ataadhini kwa kukaa.

4. KUGEUZA SHINGO KULIANI NA KUSHOTONI:

Miongoni mwa suna za adhana kama zilivyothibiti kutoka kwa Bwana Mtume . Ni muadhini kugeuza shingo yake kuliani wakati wa kusema: (Hayya alas-swalaah) na kushotoni anaposema: (Hayya Alal-falaah).

Imepokewa kwamba Abuu Juhayfah Radhi za Allah ziwe juu yake amesema:

وَأَذَّنَ بِلَالٌ قَالَ فَجَعَلْتُ أَتَتَبَّعُ فَاهُ هَا هُنَا وَهَا هُنَا يَقُولُ يَمِينًا وَشِمَالًا يَقُولُ حَيَّ عَلَى الصَّلَاةِ حَيَّ عَلَى الْفَلَاحِ]   رواه البخاري]

[Na Bilali akiadhini asema, nikawa ninaufuatilia mdomo wake huku na huko. (Akageuka) kuliani na kushotoni (wakati wa kusema): Hayya Alal-swalaah, Hayya Alal-falaah].   [Imekewa na Bukhari]

5. MWADHINI AWEKE VIDOLE VYAKE VIWILI VYA SHAHADA MASIKIONI MWAKE.

Na hii imepokelea kuwa Bilal Radhi za Allah ziwe juu yake alikuwa akiweka vidole vyake vya Shahada alipokuwa akiadhini kama alivyo taja Imamu Al Bukhari Mungu amrahamu

6. ADHANA ITOLEWE KWA UTULIVU:

Ni katika jumla ya suna mtu kuadhini kwa “Tartiyli”. Yaani ayatamke maneno ya adhana kwa mtungo wa utulivu.

7. KULETA “TATH-WIYBU” KATIKA ADHANA YA ALFAJIRI:

“Tath-wiybu” ni muadhini kusema baada ya (Hayya alal-falaah mara mbili aseme); ASWALAATU KHAYRUN MINAN-NAUM, mara mbili.

Amepokea Annasai kutoka kwa Abii Mah’dhura radhi za Allah ziwe juu yake amesema:

قلت: يا رسول الله، علمني سنة الأذان، فذكره إلى أن قال بعد قوله حي على الفلاح: فإن كان في صلاة الصبح قلت: الصلاة خير من النوم مرتين، الله أكبر الله أكبر، لا إله إلا الله

[Nilimuliza Mtume ﷺ nikasema Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nifundishe na mimi Sunna za Adhana, akamtajia mpaka alipofika kwa tamko la hayya Alaal Falaah :(akamwambia) ikiwa ni Swala ya Asubuhi utasema Aswalaatu Khayrun mina Nnawm (Swala ni bora kuliko usingizi) Mara mbili (Kisha utasema) Allahu Akbar Allahu Akbar Laailaha illa allah]

8. MWADHINI AWE NA SAUTI NZURI YA NGUVU:

Ni sunna muadhini kuwa na sauti kali na nzuri itakayomudu kuulainisha moyo wa msikilizaji na kumpelekea kuuitika wito huo.

Suna hii inatokana na kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu  alipomwambia Abdullah Ibn Zayd Radhi za Allah ziwe juu yake ambaye ndiye aliyeiona adhana usingizini:

[فقم مع بلال فألق عليه ما رأيت به، فإنه أندى منك صوتاً]

[Inuka pamoja na Bilali, umtamkishe (maneno) uliyoyaona (usingizini) Kwani yeye ana sauti kali kuliko wewe].     [Imepokewa na Abuu Daawoud]

9. MUADHINI AWE NI MUADILIFU MWENYE TABIA NJEMA:

Muadhini anapaswa kutangaa baina ya watu kwa tabia njema na uadilifu.

Hii ni kwa Hadithi iliopokelewa na Ibnu Abbas Radhi za Allah ziwe juu yake asema.

[ليؤذن لكم خياركم ويؤمكم أقراؤكم]    رواه أبوداود وإبن ماجة

[Awaadhini nyinyi mbora wenu,na awasalisheni nyinyi msomi wenu]   [Imepokewa na Abuu Dawud na Ibnu Maajah]

10. KUWE NA WAADHINI WAWILI:

Ni sunna msikiti kuwa na waadhini wawili kwa ajili ya swala ya alfajiri. Mmoja ataadhini kabla ya kuingia kwa alfajiri na mwingine baada ya alfajiri.

Sunna hii imethibiti kutokana na hadithi (riwaya) ya Abdullah Ibn Umar Radhi za Allah ziwe juu yake :

       أَنَّ بِلالا كَانَ يُؤَذِّنُ بِلَيْلٍ فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ : كُلُوا وَاشْرَبُوا حَتَّى يُؤَذِّنَ ابْنُ أُمِّ مَكْتُومٍر       رواه البخاري ومسلم

Hakika Bilali huadhini usiku, Akasema Mtume  [basi kuleni na kunyweni mpaka muisikie adhana ya Ibn Ummu Maktuum].    [Imepkewa na Bukhari na Muslim]

Lakini kunatakikana kwa muadhini huyu anayeadhini nje ya wakati kuwa na wakati mmoja ili kuepuka kuwatatiza na kuwachanganya watu.



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.