0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SOMO LA FIQHI

Suali: Nguzo za Swala ni ngapi?

Jawabu: Nguzo za Swala ni 14 nazo ni kama zifuatavyo:

1. Kutia Nia

Na nia Mahala pake ni moyoni na wala haikushurutizwa kuitamka kwa ulimi katika kuithibitisha nia nakufanya hivyo ni kukhalifu Sunna ya Bwana Mtume.

Na dilili ya nia ni neno lake Mtume :

[إنما الأعمال بالنيات]      رواه البخاري ومسلم

[Hakika ya vitendo ni kwa nia]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Kusimama katika swala ya faradhi pamoja na kuweza.

Na dalili ni neno lake Menyezi Mungu Mtukufu:

{حَافِظُواْ عَلَى الصَّلَوَاتِ والصَّلاَةِ الْوُسْطَى وَقُومُواْ للهِ قَانِتِينَ}    البقرة:238

[Zilindeni Sala, na khasa Sala ya katikati, na simameni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu nanyi ni wenye kuqunuti (kunyenyekea).]      [Al-Baqara:238]

Na kwa neno lake Mtume ﷺ alipo mwambia Imraan bin Huswein radhi za allah ziwe juu yake:

[صلِّ قائمًا، فإن لم تستطع فقاعدًا، فإن لم تستطعْ فعلى جنب]   رواه البخاري

[Swali hali ya kuwa umesimama, usipoweza, basi kwa kukaa na usipoweza basi kwa ubavu]   [Imepokewa na Bukhari.]

3. Takbiri ya kufungia Swala.Nao ni kusema “Allahu Akbar”

Na dalili ni neno lake Mtume ﷺ:

[مفتاح الصلاة الطّهور، وتحريمُها التكبير، وتحليلُها التسليم]    رواه أبوداود والترمذي

[Ufunguo wa Swalah ni kujitwaharisha, na kuifunga ni Takbira, na kuifungua ni kutoa Salaam.]  [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy]

4. Kusoma Fatiha katika kila Rakaa.

Kwa dalili ya neno lake Mtume ﷺ:

[لا صلاةَ لمَنْ لم يقرأْ بفاتحة الكتاب]    متفق عليه

[Hana Swala kwa ambaye hakusoma Suratul Fatihah]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

5. Kurukuu

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}   سورة الحج :77

[Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe.]      [Al-Hajj:77]

Na kwa hadithi aliyoipokea Abuu Hurayra katika kisa cha yule aliyekuwa akiswali vibaya Mtume alimwambia

[ثمّ اركعْ حتى تطمئنَّ راكعًا]   رواه البخاري

[Kisha rukuu mpaka upate utulivu hali yakuwa umerukuu.]     [Imepokewa na Bukhari]

6. Kuitadili kwa kulingana sawa baada ya kurukuu.

Kwa neno lake Mtume ﷺ alipo mwambia yule aliyekuwa akiswali vibaya:

[ثمّ ارفعْ حتى تعدلَ قائمًا]

[kisha nyanyuka mpaka ulingane sawa hali ya kusimama]

7. Kusujudu kwa viungo saba.

Kwa neno lake mwenyezi Mungu mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا ارْكَعُوا وَاسْجُدُوا وَاعْبُدُوا رَبَّكُمْ وَافْعَلُوا الْخَيْرَ لَعَلَّكُمْ تُفْلِحُونَ}   سورة الحج :77

[Enyi mlio amini! Rukuuni na msujudu, na muabuduni Mola wenu Mlezi, na tendeni mema, ili mfanikiwe.]    [Al-Hajj:77]

8. Kukaa baina ya sijida mbili.

Kwa neno lake Mtume ﷺ alipo mwambia yule aliyekuwa akiswali vibaya:

[حتى تطمئن جالسًا]

[Mpaka utulizane hali ya kuwa umekaa]

9. Kukaa kwa Atahiyatu ya mwisho.

Kwa sababu Mtume alikaa attahiyatu na alidumu kufanya hivyo katika Swala na yaya asema:

[صلُّوا كما رأيتموني أصلِّ]    رواه البخاري

[Swalini kama mlivyoniona nikiswali]      [Imepokewa na Bukhari]

10. Kusoma Atahiyatu

Kwa hadithi iliyopokelewa na Ibnu Mas’uud radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie yeye asema:

[لا تقولوا: السلامُ على الله، فإن الله هو السلام، ولكن قولوا: التحيات لله]   رواه النسائي

[Musiseme amani zimfikie Mwenyezi Mungu kwani Mwenyezi Mungu ndie amani,Lakini semeni Maamkuzi mema ni mwenyezi Mungu.]     [Imepokewa na Al-Nnasaai]

11. Kumswalia Mtume ﷺ katika Atahiyatu ya mwisho.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:

{إِنَّ اللهَ وَمَلائِكَتَهُ يُصَلُّونَ عَلَى النَّبِيِّ يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا صَلُّوا عَلَيْهِ وَسَلِّمُوا تَسْلِيمًا}    سورة الأحزاب:56

[Hakika Mwenyezi Mungu na Malaika wake wanamsalia Nabii. Enyi mlio amini! Msalieni na mumsalimu kwa salamu.]     [Al-Ahzaab:56]

ولحديث عبد الله بن مسعود رضي الله عنه وفيه: أمرنا الله أن نصلي عليك يا رسول الله، فكيف نصلي عليك؟ فسكت رسول الله صلى الله عليه و سلم حتى تمنينا أنه لم يسأله، ثم قال رسول الله صلى الله عليه و سلم : ((قولوا: اللهمَّ صلِّ على محمد      رواه مسلم

Na kwa hadithi ya Abdullah Ibnu Mas’uud radhi za Mwenyezi Mungu zimfikie yeye asema: Mwenyezi Mungu ametuamrisha tukuswalie ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu,tukuswalie vipi? akanymaza Mtume wa Mwenyezi mungu mpaka tulitamani kuwa hangemuliza,kisha akaema Mtume : [Semeni ewe Mwnyezi Mungu mswalie Muhammad….

[Imepokewa na Muslim]

12. Kutoa salamu.

Kwa neno lake Mtume ﷺ:

[مفتاح الصلاة الطّهور، وتحريمُها التكبير، وتحليلُها التسليم]    رواه أبوداود والترمذي

[Ufunguo wa Swalah ni kujitwaharisha, na kuifunga ni Takbira, na kuifungua ni kutoa Salaam.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Al-Ttirmidhiy]

13. Kujituliza katika nguzo zote.

Kwa sababu Mtume ﷺ alipokuwa akimfundisha yule aliyekuwa akiswali vibya alikuwa akimwambia katika kila nguzo: [mpaka utulie] na kama ilikuwa silazima utulivu basi hangemwambia.

14. Kutungamanisha baina ya nguzo.

Kwa sababu Mtume alimfundisha yule alikuwa akiswali vibaya utaratibu wa Swala,alimbwambia:

إذا قمت إلى الصلاة فكبِّرْ، ثم اقرأْ ما تيسَّرَ معك مِنَ القرآن، ثمَّ اركعْ حتى تطمئنَّ راكعًا، ثم ارفعْ حتى تعتدلَ قائمًا، ثمَّ اسجدْ حتى تطمئنَّ ساجدًا، ثمَّ ارفعْ حتى تطمئنَّ جالسًا، ثمَّ اسجدْ حتى تطمئنَّ ساجدًا، ثمَّ ارفعْ حتى تطمئنَّ جالسًا، ثم افعلْ ذلك في صلاتك كلها

[Ukisimama kuswali leta Takbiri,kisha usome ulichohifadhi katika Qur’ani,Kisha rukuu mpaka utulizane hali ya kurukuu, kisha nyanyuka mpaka ulingane sawa hali ya kusimama, kisha sujudu mpaka utulizane na hali umesujudu, kisha nyanyuka mpaka utulizane hali ya kuwa umekaa.]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.