0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

WAJIBATI ZA UMRA NA SUNNA ZAKE

SOMO LA FIQHI

Wajibu za Umra
1. Kuhirimia kutoka kwenye mahali palipowekewa kuhirimia,
kwa neno lake Mtume ﷺ baada ya kutaja sehemu za kuhirimia:

[هُنَّ لَهُنَّ، وَلِمَنْ أَتَى عَلَيْهِنَّ مِنْ غَيْرِهِنَّ مِمَّنْ أَرَادَ الْحَجَّ وَالْعُمْرَ]   رواه البخاري

[Sehemu hizo zimewekewa watu wa hapo na wasiokuwa watu wa hapo kati ya wale wanaofika hapo miongoni mwa wanaotaka kuhiji au kufanya Umra]   [Imepokewa na Bukhari.]

2. Kunyoa au kupunguza,
kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

{لَتَدۡخُلُنَّ ٱلۡمَسۡجِدَ ٱلۡحَرَامَ إِن شَآءَ ٱللَّهُ ءَامِنِينَ مُحَلِّقِينَ رُءُوسَكُمۡ وَمُقَصِّرِينَ}   الفتح: 27

[Mtaingia Msikiti wa Haram mkiwa katika amani apendapo Mwenyezi Mungu, hali ya ya kunyoa vichwa vyenu na kupunguza]   [48: 27].

Sunna za Umra
Sizokuwa nguzo na wajibu ni sunna.

Matanabahisho

1. Mwenye kuacha nguzo moja miongoni mwa nguzo za Umra, ibada yake ya Umra haitatimia mpaka ailete.

2. Mweye kuacha tendo moja la wajibu miongoni mwa wajibu za Umra, itamlazimu achinje mnyama (mbuzi au kondoo, au fungu moja kati ya mafungo saba ya ngombe au ngamia.

3. Mwenye kuacha sunna ya umra haimlazimu chochote, na umra yake ni sahihi.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.