0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SUNNA ZA UDHU (KUTAWADHA)

SOMO LA FIQHI

Suala: Ni zipi Sunna za udhu?

Jawabu: Sunna za udhu ni kama zifuatavyo:

1. Kupiga Bismillahi mwanzo wakutawadha, kwa Hadithi iliyopokelewa na Abuu Hurayra radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume :

[لَا وُضُوءَ لِمَنْ لَمْ يَذْكُرِ اِسْمَ اَللَّهِ علَيْهِ.]     أَخْرَجَهُ أَحْمَدُ, وَأَبُو دَاوُدَ, وَابْنُ مَاجَهْ

[Hana udhu kwa yule ambae hakutaja jina la Mwenyezi Mungu juu yake]

[Imepokelewa na Ahmad na Abuu Daud na Ibnu Maajah]

2. Kupiga Mswaki:
Kwa Hadithi iliyopokelewa na Abuu Hurayra radhi za Allah ziwe juu yake amesema: Amesema Mtume ﷺ :

[لَوْلَا أَنْ أَشُقَّ عَلَى أُمَّتِي لَأَمَرْتُهُمْ بِالسِّوَاكِ مَعَ كُلِّ وُضُوءٍ.]    أَخْرَجَهُ مَالِكٌ, وأَحْمَدُ, وَالنَّسَائِيُّ, وَصَحَّحَهُ اِبْنُ خُزَيْمَة

[Lau si kuwaonea uzito umati wangu,ningeliwaamrisha kupiga mswaki pamoja na kila udhu]   [Imepokewa na Malik na Ahmad na Annasaai na kusahihishwa na Ibnu Khuzaymah].
3. Kuosha vitanga viwili vya mikono mara tatu mwanzo wa kutawadha. kwa hadithi iliyopokelewa na Imamu Ahmad na Annasaai kutoka kwa Aws radhi za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake asema:

[رأيت النبي صلى الله عليه وسلم توضأ فاستوكف ثلاثا، أي غسل كفيه ثلاثا]

[Nimemuona Mtume ﷺ wakati wakutawadha anaosha viganja vyake viwili vya mikono mara tatu].

Isipokuwa kichwa na masikio mawili, havioshwi hupanguswa mara moja.

4. Kusukutua na kuvutia maji puwani, hivi ni kama ilivyoonekana akifanya Mtume na kauli yake Mtume aliposema [Mambo kumi ni katika Sunna] ikahisabiwa miongoni mwa kumi hayo ni kusukutuwa na kuvutia maji puwani. [Imepokewa na Muslim].

kwa mtu alie funga haipendekezi kwake kuzidisha jambo hili la kusukutuwa na kupandisha maji puani,kwa kukhofia maji yasipenye na akawa ni mwenye kuharibu saumu yake, na hili ni kwa mujibu wa hadithi iliyopokelewa na Abuu Daudi na Annisaai na Attirmidhi amesema Mtume :

[وبالغ في الاستنشاق إلا أن تكون صائما]

[Na zidisha kupandisha maji puani (wakati wa kutawadha) ila ukiwa umefunga.]

5.Kuanzia kuliani kabla ya kushoto: nako ni kuanza upande wa kulia katika kuosha viungo vya udhu.kwa neno lake Mtume ﷺ:

[ إذا توضأتم فابدأوا بميامنكم]     أخرجه الأربعة

[Mukitawadha anzieni kwa kuliani mwenu].  [Imehadithiwa na Abu Daud na Annasaai na Attirmidhiy, Ibnu Maajah, na Ibnu Khuzaimah na Ibnu Hibban wameipa darja ya Hadithi sahihi].

6. Kurefusha vingaja: yaani kupitisha zaidi ya vifundo vya mikono katika kuosha.

7. Kutoa mwanya kwenye ndevu ili kufikisha maji kwenye ngozi ya uso. Haya kama ilivyopokewa kutoka kwa Ibni ‘Abbas radhi za Allah ziwe juu yake ya kwamba Mtume wetu ﷺ alikuwa anapotia udhu hupapachua ndevu zake kwa vidole vyake. [Imepokelewa na Ibnu Majah].

8.Kufikisha maji baina ya vidole vya mikono na miguu, Haya ni kutokana na Hadithi ya Mtume ﷺ:

[إِذَا تَوَضَّأْتَ فَخَلِّلْ أَصَابِعَ يَدَيْكَ وَرِجْلَيْكَ]

[Ukitawadha papachua vidole vyako vya mikono na miguu]    [Imepokelewa na Ibnu Maajah na Al Tirmidhy]

9. Kutumia maji kwa kiasi, kwa kuwa Mtume ﷺ: amesema [Kutakuwa na watu katika umma huu watakaopitisha kiasi katika kujitwahirisha]  [Imepokewa na Abu Daud.]  Yaani watatumia maji ya kutawadhia kwa kupita kiasi

10.Dua baada ya kutawadha. Amesema Mtume ﷺ :

مَا مِنْكُمْ مِنْ أَحَدٍ يَتَوَضَّأُ, فَيُسْبِغُ اَلْوُضُوءَ, ثُمَّ يَقُولُ: أَشْهَدُ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اَللَّهُ وَحْدَهُ لَا شَرِيكَ لَهُ, وَأَشْهَدُ أَنَّ مُحَمَّدًا عَبْدُهُ وَرَسُولُهُ, إِلَّا فُتِحَتْ لَهُ أَبْوَابُ اَلْجَنَّةِ. أَخْرَجَهُ مُسْلِم ٌ وَاَلتِّرْمِذِيُّ, وَزَادَ:  اَللَّهُمَّ اِجْعَلْنِي مِنْ اَلتَّوَّابِينَ, وَاجْعَلْنِي مِنْ اَلْمُتَطَهِّرِينَ

[Hakuna yoyote miongoni mwenu atakayetawadha, akaeneza maji ya kutawadhia kwenye viungo, kisha akasema “Nakiri kwa moyo kibaini kwa ulimi kuwa hakuna anayestahiki kuabudiwa isipokuwa mungu moja na Muhammad ni mja wa Mwenyezi Mungu na Mtume wake. Isipokuwa atafunguliwa milango ya pepo minane, auingie autakao [Imepokewa na Muslim na Al Tirmidhiy na akazidisha “Ewe Mola! Nijaalie niwe miongoni mwa wenye kutubia na unijaalie ni miongoni mwa wenye kujitwahirisha]

11.Kuswali rakaa mbili baada ya kutawadha. Mtume ﷺ alisema:

[من توضأ مثل وضوئي هذا، ثم صلى ركعتين لا يحدث فيهما نفسه، غفر له ما تقدم من ذنبه]  أخرجه البخاري

[Mwenye kutawadha kama hivi ninavyotawadha, kisha akainuka akaswali rakaa mbili bila kusema na nafsi yake, atasamehewa dhambi zake zilizotangulia]

[Imepokewa na Bukhari].


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.