0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO YANAYOHARIBU UDHU

SOMO LA FIQHI

1. Kila chenye kutoka kwenye mojawapo ya njia mbili, mfano wa mkojo, choo, upepo (kushuta) kwa neno lake Mwenyezi Mungu :

{أو جاء أحد منكم من الغائط }   النساء: 43

[Au mmoja wenu ametoka chooni, au mmewagusa wanawake]    [Al Nnisaa:43]

Na kwa Neno lake Mtume ﷺ:

[لَا يَقْبَلُ اللَّهُ صَلَاةَ أَحَدِكُمْ إِذَا أَحْدَثَ حتى يتوضأ ]    متفق عليه

[Mwenyezi Mungu hakubali Swala ya mmoja wenu akitokwa na hadathi mpaka atawadhe]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Kulala usingizi mzito ambao mtu hafahamu chochote. Na hi inaingia hapa, kama kukosa fahamu, na kupotezwa fahamu kikamilifu.

Kwa neno lake Mtume ﷺ:

[العين وكاء السه فمن نام فليتوضأ،]   رواه أحمد وابن ماجه بإسناد حسن

[Macho mawili ni kifuniko cha Duburi (tupu ya nyuma) kwa yoyote atakae lala basi atawadhe]   [Imepokewa na Ahmad na Ibnu Maajah kwa Isnaad mzuri]

3. Kugusa tupu ya mbele au ya nyuma kwa mkono bila ya kizuizi, kwa hadithi iliyo pokelewa na Busra binti Swafawan Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alimsikia mtume ﷺ akisema:

[من مس فرجه فليتوضأ ]  رواه النسائي  وابن ماجه  وصححه الألباني في صحيح النسائي 

[Mwenye kugusa tupu yake na atawadhe]      [Imepokewa na Annasai na Ibnu Maajah na kusahihishwa na Al Bani katika Swahihi Al Nnasai ]

4. Kumgusa Mwanamke wa kando kwa matamanio,kwa neno lake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{أو لا مستم النساء}    النساء: 43

[Au mmewagusa wanawake]    [Annisaa:43]

5. Kula nyama ya ngamia, kwa hadithi ya Jabir bin samurah kwamba mtu alimuuliza Mtume ﷺ:

 [أنتوضأ من لحوم الإبل؟ قال: نعم توضأ من لحوم الإبل ].    رواه مسلم 

[Je, tutawadhe kwa kula nyama za ngamia? Akasema: Ndio]     [Imepokewa na Muslim.]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.