0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SOMO LA FIQHI

Suali: Ni zipi Faradhi za udhu?

Jawabu: Faradhi za Udhu ni sita
1. Kutia nia. kwa neno lake Mtume ﷺ:

[إنَّما الأَعمالُ بالنِّيَّات]    رواه البخاري

[Hakika (kusihi) ibada ni kwa (kupatikana) nia]   [Imepokewa na Bukhari]

Na mahali pake ni moyoni, wala haitamkwi. Na lau mtu afanya matendo ya kutawadha kwa lengo la kujiburudisha au kujinadhifisha, bila ya nia ya kutawadha, basi hilo halimtoshelezi.

2. Kuosha uso. Na miongoni mwa huko ni kusukutua na kupaliza puani.

3. Kuosha mikono miwili pamoja na vifundo viwili.

4. Kupangusa kichwa chote, pamoja na masikio mawili

5. Kuosha miguu miwili pamoja na vifundo viwili.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا إِذَا قُمْتُمْ إِلَى الصَّلَاةِ فَاغْسِلُوا وُجُوهَكُمْ وَأَيْدِيَكُمْ إِلَى الْمَرَافِقِ وَامْسَحُوا بِرُءُوسِكُمْ وَأَرْجُلَكُمْ إِلَى الْكَعْبَيْنِ}   المائدة:6

[Enyi mlio amini! Mnapo simama kwa ajili ya Sala basi osheni nyuso zenu, na mikono yenu mpaka vifundoni, na mpake vichwa vyenu, na osheni miguu yenu mpaka vifundoni]   [Al Maaida:6]

6. Kufuatanisha beina ya viungo.

haya yamethibitika kutokana na hii Aya iliofunza juu ya udhu – Al Maida : 6, kwani “wau” iliomo kwenye Aya hii ni yenye kueleza juu ya mpangilizio. Pia haikupokewa kuwa Mtume wetu ﷺ amewahi kutawadha bila ya mpangilizio kama ulivyokuja kwenye Aya hii.

Vilevile ameeleza Mtume wetu ﷺ alisema baada ya kukamilisha kutia udhu maneno yenye maana kama hivi:

[هَذَا وُضُوءُ مَنْ لا يَقْبَلُ اللَّهُ مِنْهُ صَلاةً إِلا بِهِ]    رواه البخاري

[Huu ndio udhu, hakubali Mwenyezi Mungu Mtukufu Sala ila kwa udhu kama huu]  [Imepokewa na Bukhari]

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.