0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MASHARTI YA KUTAWADHA

SOMO LA FIQHI

Suala: Ni yapi Masharti ya kutawadha?

Jawabu: Masharti ya kutawadha ni kama yafuatavyo

1. Maji yawe twahara.

2. Maji yawe yafaa kutumiwa, yasiwe ya kuiba, kwa mfano.

3. Kuondoa chochote chenye kuzuia maji kufika kwenye ugozi, kama vile mafuta ya mshumaa na mfano wake.

4. Kumaliza na kukatika kinacho sababisha kutawadha, kwa mfano mtu kutawadha na huku bado hajamaliza kukidhi haja yake.

5. Kukatika kwa damu ya Hedhi na Nifasi kwa Mwanamke, lau atatawadha mwanamke mwenye Hedhi au Nifasi basi Udhu wake hautasihi.

6. Kuingia kwa wakati kwa mtu mwenye Hadathi ya daima kama mwenye ugonjwa wa kutokwa na mikojo au Mwanamke mwenye damu ya Istihadha (Damu ya ugonjwa).


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.