SOMO LA FIQHI
Sunna za Hijja
Lisilokuwa nguzo na wajibu ni Sunna, kama inavyofuata:
1. Kuoga wakati wa kuhirimia.
2. Kuhirimia kwa kikoi cheupe na shuka ya juu nyeupe.
3. Kuleta Labeka kwa sauti ya juu.
4. Kutufu twawafu ya kufika Makka kwa anayechanganya Hija na Umra na anayehiji peke yake.
5. Kwenda haraka katika mizunguko mitatu ya mwanzo twawafu ya kufika Makka (kwa ibada ya Hija) au Umra. Ramal ni kutembea kwa haraka.
6. Kufanya idhtibaa’ katika twawafu ya kufika Makka (kwa mwenye kuhiji) au Umra, nako ni kuiweka shuka yake ya juu chini ya kapwa la mkono wa kulia.
7. Kulala Mina usiku wa Arafa.
8. Kulibusu Jiwe Leusi.
9. Kukusanya swala ya Maghrib na isha katika Muzdalifa kwa kuchelewesh
10. Kusimama Muzdalifa kwenye mash’aril haraam kuanzia Alfajiri mpa karibu na kuchomoza jua akiweza kufanaya hivyo, asipo weza sehemu yoyote ya Muzdalifa ni sehemu yakisimamo.
Tanbihi
Sunna za Hijja
Mwenye kuiacha sunna moja miongoni mwa sunna za Hija, halazimiwi na kitu chochote, na Hija yake ni sahihi.