June 22, 2021
0 Comments
SOMO LA FIQHI
Masiku ya Tashriiq
Ni siku tatu, siku ya kumi na moja na siku ya kumi nambili na siku ya kumi na tatu katika Mwezi wa Mfungotatu zimeitwa kwa jina hilo kwa sababu nyama za Udh’hiya zikikatwakatwa na kuanikwa juani ili zikauke na Mtume ﷺ Alisema kuhusu masiku haya
[ أَلاَ وَإِنَّ هَذِهِ الأَيَّامَ أَيَّامُ أَكْلٍ وَشُرْبٍ وَذِكْرِ اللهِ عَزَّ وَجَلَّ] رواه أبوداود
[Jueni ya kuwa masiku haya ni masiku ya kula nakunywa na kumtaja Mwenyezi Mungu] [Imepokewa na Abuu Daud]