0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAELEZO MUHIMU KWA MAHUJAJI KUHUSU KUTUPA VIJIWE

SOMO LA FIQHI

Maelekezo
Muislamu ajiepushe na kuwaudhi ndugu zake Mahujaji wakati wa kutupa vijiwe jamaraat, nawakati wakufanya ibada nyinginezo za hija.

Ahakikishe kuwa kijiwa kimeingie kwenye ndani ya birika, baadhi ya watu wanakosea wakidhani kuwa unapo rusha kijiwe ni kulenga kiguzo na kijiwe kisingie kwenye birika, na baadhi hutupa kijiwa akiwa mbali na birika na kijiwe kisingie kwenye birika basi mwenye kutupa namna hiyo huwa hakutekeleza wajibu wa kutupa.

– Na ni juu ya Muislamu asivuke mipaka katika kurusha vijiwe asitupe jiwe kubwa au kurusha viatu, sunna ni kijiwe kiwe kikubwa kidogo kuliko dengu kwa Hadithi ya Jaabir bin Abdillah Radhi za Allah zimfikie yeye Nakasema:

[ رَأَيْتُ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ رَمَى الْجَمْرَةَ بِمِثْلِ حَصَى الْخَذْفِ]    رواه مسلم

[Nimemuona Mtume ﷺ Akilitupia jamara kwa kijiwe kidogo mfano wa koko ya tende]        [ Imepokewa na Muslim.]

Na vjiwe vyakutupa ni vidogo atavishika kwa vidole viwili na kutupa].

– Na akitupa vijiwe vyote kwa mara moja hahisabiwi ila kijiwe kimoja, na lau ataviweka kwenye kitu avirushe vyote kwa pamoja haitasihi bali ni lazima kupatikane kurusha.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.