0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MASHARTI YA KUPANGUSA JUU YA VITATA, BENDEJI NA PLASTA

SOMO LA FIQHI

1. Imesharutishwa katika bendeji au vitata visizidi sehemu inayotakikana kutibu pamoja na sehemu za kandokando yake zinazohitajika kuthibitisha vitu hivi.

2. Haisharutishwi katika kufunga bendeji au vitata awe mtu yuko kwenye twahara, vilevile haisharutishwi muda maalumu, madamu vinahitajika kusalia basi yafaa kupukusa juu yake wakati wakujitwahirisha na tukio kubwa na dogo la ukosefu wa utwahara. Na wakati wowote ule mahitaji yake yameondoka ni lazima kuvivua na kukiosha kiungo husika wakati wa kujitwahirisha.

3. Kuhusu mabendeji na vitata na mfano wahivyo ambavyo ni rahisi kuzirudisha itatazamwa:

a. Ikiwa kuvitoa na kuosha sehemu za chini yake ni sahali bila madhara au kusababisha jaraha kuchelewa kupoa, basi atavitoa aoshe sehemu za chini yake, kisha avirudishe.

b. Iwapo si rahisi kuvitoa na kuosha sehemu za chini yake bila kudhurika au kuchelewa kupoa, atapukusa juu yake wakati wa kuosha kiungo kile ambacho vitu hivyo viko juu yake.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.