SOMO LA FIQHI
KITATA: Ni kile kinachofungwa mahali palipovunjika kiwe ni tambara zito au vipande vya mti au mfano wake
BENDEJI: Ni kitu kinachotatiwa kwenye jaraha au mahali palipochomeka au kinginecho kwa kitambaa au mfano wake ili kujitibu nacho.
PLASTA: Ni kile kinachobandikwa kwenye jaraha na mfano wake kwa kujitibu.
DALILI YA KUSIHI KUPANGUSA JUU YA KITATA
Amepokewa kutoka kwa Jabir Radhi za Allah ziwe juu yake alisema:
خَرَجْنَا فِي سَفَرٍ فَأَصَابَ رَجُلًا مِنَّا حَجَرٌ فَشَجَّهُ فِي رَأْسِهِ ثُمَّ احْتَلَمَ فَسَأَلَ أَصْحَابَهُ فَقَالَ هَلْ تَجِدُونَ لِي رُخْصَةً فِي التَّيَمُّمِ فَقَالُوا مَا نَجِدُ لَكَ رُخْصَةً وَأَنْتَ تَقْدِرُ عَلَى الْمَاءِ فَاغْتَسَلَ فَمَاتَ فَلَمَّا قَدِمْنَا عَلَى النَّبِيِّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ أُخْبِرَ بِذَلِكَ فَقَالَ قَتَلُوهُ قَتَلَهُمْ اللَّهُ أَلَا سَأَلُوا إِذْ لَمْ يَعْلَمُوا فَإِنَّمَا شِفَاءُ الْعِيِّ السُّؤَالُ إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيهِ أَنْ يَتَيَمَّمَ وَيَعْصِرَ أَوْ يَعْصِبَ عَلَى جُرْحِهِ خِرْقَةً ثُمَّ يَمْسَحَ عَلَيْهَا وَيَغْسِلَ سَائِرَ جَسَدِهِ رواه أبوداود
[Tulitoka kwenda safari, na mmoja wetu akagongwa na jiwe kichwani mwake likampasua. Kisha akaota (kuwa amelela na mwanamke). Akawauliza wenzake: “Je mnanipatia ruhusa yoyote kisheria ya mimi kutayamam?” Wakasema “Hatukupatii madamu wewe unaweza kutumia maji”. Akaoga na akafa. Tiliporudi kwa Mtume ﷺ alielezwa habari hiyo akasema: [Wamemuua! Mwenyezi Mungu Awaue. Si wangeuliza ikiwa hawajui? Kwani dawa ya kutojua ni kuuliza.” Hakika ingalimtosha yeye kutayamamu na kufunga kitamba kwenye jaraha lake, kisha akapukusa juu yake, na kuosha sehemu zisaliezo za mwili wake] [Imepokewa na Abu Daud.].