0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAMBO YANAYO CHUKIZA KATIKA SWALA (MAKRUHATI SWALAT)

 SOMO LA FIQHI

Suali: Ni nini Makruhi kisheria (jambo la kuchukiza)

Jawabu: Kisheria Makruhi ni jambo ambalo ukiliwacha unapata Thawabu na ukilifanya hupati Dhambi.

Suali: Ni yapi yanayo chukiza katika Swala?

Jawabu: Yanayo chukiza katika Swala ni haya yanayofuata:

1. Mtu kuswali akiwa na mawazo mengi yenye kumshawishi, ama mbele yake kuna jambo la kushugulisha na swala yake, kama kujizua na haja ndogo ama kubwa ama upepo, au akiwa na njaa au kiu ama kuwa mbele yake chakula anacho kipenda, au kutazama kitu kinacho mshughulisha na swala yake.Kwa neno lake Mtume:

[لا صلاة بحضرة طعام، ولا وهو يدافعه الأخبثان]    رواه مسلم

[Hakuna Swala kinapowekwa chakula na kwa mtu anaejuzuiya haja mbili]     [Imepokewa na Muslim]

Kwa sababu mtu atakuwa hana unyenyekevu katika Swala,na unyenyekevu ndi roho ya Swala.Nawanachuoni wakakisia kila jambo ambalo linalo mshgulisha mtu na khushuu kuwa jambo hilo ni Makruhi.

2. Kufanya jambo lenye kukutowa kwenye unyenyekevu na utulivu katika swala, mfano kufanya harakati nyingi bila ya haja, na kuchezacheza na ndevu na nguo na kilemba na saa na kuvialisha vidole na kuvishikanisha na mfano wa hayo.

Anasema Shu’uba kijakazi cha Ibnu Abbas radhi za Allah ziwe juu yake:

[صليت إلى جنب ابن عباس ففقَّعت أصابعي , فلما قضيت الصلاة قال : لا أمَّ لك ! تفقع أصابعك وأنت في الصلاة !]     ” رواه ابن أبي شيبة

[Niliswali ubavuni mwa Ibnu Abbas ni kavialisha vidole vyangu nilipo maliza kuswali akaniambia: wewe huna mama! unavialisha vidole vyako na wewe uko katika Swala!]    [Imepokewa na Ibnu Abishayba]

3. Kuzunguka kwa uso katika Swala bila ya haja kwa sharti mwili uwe umeelekea kibla, lakini mwili ukitoelekea kibla swala itaharibika.

Kwa hadithi iliyopokelewa na Bibi Aisha radhi za Allah ziwe juu yake asema:

[سألت النبي صلى الله عليه وسلم عن الالْتِفاتِ في الصلاة فقال: هو اخْتِلاس يَخْتَلِسُهُ الشيطانُ من صلاة العبد]   رواه البخاري والترمذي

[Nilimuliza Mtume ﷺ kuhusu kuzunguka katika swala akasema huo ni wizi Shetani anamuibia mja katika Swala yake]        [Imepokewa na Bukhari]

4. Nakushika kiuno kwenye swala kama wanavofanya mayahudi.

Kwa hadithi iliyopokelewa na Abuu Hurayra radhi za Allah zimfikie yeye asema:

[نهى أن يصلي الرجل مُتَخَصِّراً]         متفق عليه

[Amekataza Mtume ﷺ mtu kuswali na huku ameweka mikono kiunoni]    [Imepokelewa na Bukhari na Muslim]

5. kuufunga mdomo na pua katika swala.

Kwa Hadithi iliyopokelewa na Abuu Hureyra radhi za Allah ziwe juu yake amesema:

[أنَّ رسولَ اللهِ صلى الله عليه وسلم نهى عن السَّدل في الصَّلاةِ, وأنْ يُغطِّيَ الرَّجُلُ فَاهُ]    رواه أبو داود والترمذي، وحسَّنَهُ الألبانيُّ

[Amekataza Mtume ﷺ kuingiza mikono ndani yanguo wakati mtu anaswali,na mtu kufunika kinywa chake.]     [Imepokewa na Abuu Daud na Al Ttirmidhiy]

6. Kukunja nguo kama mikono ya kanzu na mfano wake.

Kwa hadithi iliyopokelewa na Ibnu Abbas radhi za Allah ziwe juu yake asema amesema Mtume ﷺ:

[أُمرت أن أسجد على سبعة أعظُمٍ ولا أكفَّ ثوبًا ولا شعرًا]      رواه البخاري ومسلم

[Nimearishwa kusujudu juu ya viungo saba, na nisikunje nguo au kuzifunga nywele]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

7. Kuzifunga nywele kwa anaekuwa na nywele nyingi ili anapo sujudu zi sisujudu pamoja na yeye.

Kwa Hadithi ya Ibnu Abbas iliyotangulia

8. Kutema mate ama kohozi mbele ya kibla au upande wake wa kulia.

Kwa Hadithi iliyopokelewa na Anasa radhi za Allah ziwe juu yake asema amesema Mtume :

[إذا كان أحدكم في الصلاة فإنه يناجي ربه، فلا يبزقن بين يديه ولا عن يمينه، ولكن عن شماله تحت قدمه]     متفق عليه

Mmoja wenu akiwa katika Swala huwa anamnogoneza mola wake,basi asiteme mate (au kohozi) mbele yake,wala upande wakulia,lakini ateme upande wa kushoto chini ya nyayo zake.]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Na hili ni mtu anapokuwa anaswali nje ya Msikiti na akawa amehitajia kufanya hivyo.

9. Kutizima mbingu.

Kwa hadithi iliyopokelewa na Abuu Hurayra radhi za Allah zaimfikie yeye amesema kuwa Mtume  ﷺ amesema:

[لَيَنْتَهِينًّ أقوام يرفعون أبصارَهم إلى السماء في الصلاة أو لَتُخْطَفَنَّ أبصارُهم]    رواه مسلم وأحمد

[Watu na wakomeke kutizama mbingu wakiwa katika Swala au watapofika macho yao.]     [Imepokewa na Muslim na Ahmad]

10. Kufumba macho bila ya haja.

Kwa sababu ni kujifananisha na Majusi katika Ibaada zao.

11. Kunyosha mikono wakati wakusujudu.

Kwa hadithi iliyopokelewa na Anas radhi za Allah ziwe juu yake asema amesema Mtume  :

[اعتدلوا في السجود، ولا يبسط أحدكم ذراعيه انبساط الكلب]    متفق عليه

[Linganeni kwenye sijda wala asinyoshe mmoja wenu mikono yake kama anavyo nyosha jibwa]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim]



Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.