0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAANA YA MIIQATI NA AINA ZAKE

MAANA YA MIIQATI NA AINA ZAKE

Suali: Ni nini maana ya Miiqaat (Nyakati)
Jawabu: Nyakati kilugha ni kuweka mpaka baina ya vitu viwili.

Ama kwa istilahi ya sheria
Ni mipaka iliyowekwa na sharia kwa ajili ya ibada na yawakati na Namahali.

AINA YA NYAKATI

Kwanza: Nyakati za mahali
Nyakati za mahali
Ni sehemu zilizowekwa na Sheria kuhirimia kutoka hapo

Haifai kwa anyetaka kuhiji au kufanya Umra azipite sehemu hizo isipokuwa awe amehirimia. Nazo ni sehemu tano:

1. Dhul Hulaifah

Nayo ipo upande wa kusini wa mji wa Mtume wa Madina, na unaitwa «Abyaar ‹Ali». Iko mbali na Makka kwa masafa ya kilimita 420.

Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Madina.

2. Juhfah:

Nayo iko karibu ya mji wa Raabigh, na ina umbali wa kiasi cha kilomita 186 kutoka Makka.

Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Shaam, Masri na nchi za upande wa maghribi

3. Yalamlam:

Nayo ni bonde kubwa kwenye njia ya watu wa Yaman kwenda Makka.

Kwasasa inaitwa: Assa›diyyah, na iko mbali na Makka kwa kiasi cha kilomita 120.

Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Yaman.

4. Qarnul Manaazil:

Na sasa inaitwa ( Assaylul Kabiir), na iko mbali na Makka kwa kiasi cha kilomita 75.

Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa Najd na Twaif. Na juu yake, kwenye njia ya Twaif upande wa Hadaa kuna mahali panapoitwa Waadii Muharram.

Na pote pawili ni sehemu ya kuhirimia watu wa Najd na wale wanaokuja kupitia njia ya Twaif.

5. Dhaatu’Irq:

na sasa inaitwa (Dhariibah au Khuraibaat).

Napo ni mahali upande wa Mashariki ya Makka. Umbali wake na Makka ni kiasi cha kilomita 100. Na kwa sasa hapo mahali pamehamwa.

Nayo ni mahali pa kuhirimia watu wa upande wa Mashariki (Iraki, Irani na nchi za nyuma yake. Na dalili ya yaliyopita ni ni riwaya iliyopokewa kutoka kwa Ibnu Abbas radhi za Allah ziwe juu yake kuwa alisema:[Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ aliwawekea watu wa Madina Dhulhulaifah iwe ni mahali pa wao kuhirimia, akawawekea watu wa Sham hapo Juhfa. Akawawekea watu wa Najd hapo Qarnulmanaazil, Akawawekea watu wa Yaman hapo Qarnulmanaazil na akasema:

[هُنَّ لَهُنّ وَلِمَنْ أَتَى عَلَيْهِنَّ مِنْ غَيْرِهِنَّ]

[Sehemu hizo ni zao wao na wanaokuja hapo kati wa watu wa maeneo mengine wanaotaka kuhiji au kufanya Umra]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Ama Dhaatu ‘Irq haikutajwa kwenye hadithi iliyotangulia, na lililowekwa ni ‘Umar ibnu l- Khattaab [Imepokewa na Bukhari.].

MAELEZO 

– Mwenye kuvuka sehemu hizi za mikati bila ya kuhirimia ni lazima kurudi na kuhirimia ikiwezakana, na isipoweza kufanya hivyo basi atawajibika kutoa fidiya, nao ni mbuzi atakae mchinja makka na agawanye nyama yake kwa masikini wa makka.

– Mwenye kupita sehemu za Mikaati kwa mtu asie kuwa ni wasehemu hiyo basi atahirimi hapo, lau mtu wakutoka najdi amekuja kwa njia ya watu wa madina atahirimia sehemu ya watu wa madina (Abyaar Ali)

– Mtu ikiwa nymba yake iko ndani ya sehemu ya kuhirimia kwa upande wa makka basi Mtu huyu atahirimia hija na umra sehemu alipo Mfano wa watu wa Jiddah na Bahra na Ashraa’i.

– Mwenye kuja kwa njia ya anga na bara, na bahari, huyu atahirimia akiwamkabala na sehemu ya Mikati iliyo karibu. Kwa kauli ya umar binl-khatwab (angaliyani mkabala wake kutoka kwenye njia yenu)  [Imepokewa na Bukhari.]

– Mwenye kutia nia ya kuhiji kwa mtu wa makka au asie kuwa mtu wa makka huyu atahirimia makka, ama akitaka kufanya Umra atatoka kwenda tan’iim na Ji’iraan nazo ni sehemu ziko nje ya mipaka ya haram

Pili: Nyakati za kuhirimia
Nyakati za kuhirimia
Zama za kuhiji na kufanya Umra

A. Nyakati za Hijja

Ni miezi ya Hija nayo ni: Mfungomosi, Mfungopili na siku kumi za Mfungotatu.

kama alivyo sema Mwenyezi Mungu:

{الْحَجُّ أَشْهُرٌ مَّعْلُومَاتٌ ۚ فَمَن فَرَضَ فِيهِنَّ الْحَجَّ فَلَا رَفَثَ وَلَا فُسُوقَ وَلَا جِدَالَ فِي الْحَجِّ}   البقرة:197

[Hija ni miezi maalumu. Na anaye kusudia kufanya Hija katika miezi hiyo, basi asiseme maneno machafu wala asifanye vitendo vichafu wala asibishane katika Hija.]   [Al Baqara:197]

B. Nyakati za Umra

Ni mwaka mzima


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.