0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAANA YA IHARAM

MAANA YA IHARAM

Suala: Ni nini Maana ya ihram (Kuhirimia)

Jawabu: Maana ya Ihram kilugha: Ni kuzuia

Ama maana ya Kuhirimia kisheria:

“Ni nia ya kuingia kwenye ibada ikifungamana na mojawapo ya matendo ya Hijja”

Na haifungamani Iharamu ila kwa nia, Mtu hahisabiwi kuwa amehirimia kwa kule kuazimia kwenda hijja au Umra kwa sababu toka aliposafiri mji wake huwa ameazimia kuhiji au kufanya umra, na wala hawi ni mwenye kuhirimia kwa kuvaa ihram au kuleta talbiya bila kutia nia ya ibada ya hijja kwa neno lake Mtume ﷺ :

[إنما الأعمال بالنيات وإنما لكل امرئ ما نوى]       متفق عليه

[Hakika amali zote ni kwa nia na kila mtu hulipwa kama alivyo nuiya]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.