0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAANA YA ADHANA NA IQAAM NA HUKMU YAKE

MAANA YA ADHANA NA IQAAM NA HUKMU YAKE

MAANA YA ADHANA

Adhana ni neno la Kiarabu lenye maana mbili; maana ya kilugha na maana ya kisheria Kilugha neno adhana lina maana ya “tangazo” kama lilivyotumika ndani ya Qur’ani Tukufu:

{وَأَذَانٌ مِّنَ اللَّهِ وَرَسُولِهِ إِلَى النَّاسِ يَوْمَ الْحَجِّ الْأَكْبَرِ أَنَّ اللَّهَ بَرِيءٌ مِّنَ الْمُشْرِكِينَ}    التوبة:3

[Na ni tangazo kutokana na Mwenyezi Mungu na Mtume wake kwa wote siku ya Hija Kubwa kwamba Mwenyezi Mungu na Mtume wake hawana jukumu lolote kwa washirikina] [Tawba:3]

Ama maana ya adhana kisheria: Ni (dhikri) utajo maalum iliyowekwa na Uislamu kwa ajili ya kutangaza kuingia kwa wakati wa swala ya fardhi na kuwaita waislamu kuja kuswali

MAANA YA IQAAMA

Ni kujulisha kuanza kuswaliwa kwa kuleta utajo (dhikiri) maneno maalumu.

HUKMU YA KUADHINI NA KUQIMU
1. Katika Swala za jamaa:
Ni faradhi ya kutosheleza, kwa Swala tano za faradhi peke yake, sawa mtu akiwa safarini au mjini, kwa kuwa hizo mbili ni miongoni mwa alama za Uislamu za waziwazi, hivyo basi haifai kuziacha. Amesema Mtume ﷺ:

[وإذا حضرت الصلاة فليؤذن لكم أحدكم، وليؤمكم أكبركم]   متفق عليه

[Ufikapo Wakati wa Swala, basi awaadhinie mmoja wenu, kisha awaswalishe mkubwa wenu]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Katika Swala ya anayeswali peke yake:
Ni sunna. Amepokewa kutoka kwa Uqbah bin Amir akisema: Nilimsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ akisema:

يعجب ربكم من راعي غنم في رأس شظية بجبل يؤذن بالصلاة ويصلي فيقول الله عز وجل انظروا إلى عبدي هذا يؤذن ويقيم الصلاة يخاف مني قد غفرت لعبدي وأدخلته الجنة     رواه أبوداود والنسائي

[Anamuonea ajabu Mola wako mchunga mbuzi aliye juu ya kilele cha jabali, anayeadhini kwa Swala kisha akaswali, hapo aseme Mwenyezi Mungu Aliyetukuka: “Mwangalieni mja wangu huyu, anaadhini kisha anakimu Swala, ananiogopa! Nishamsamehe mja wangu na nitamuingiza Peponi]     [Imepokewa na Abuu Dawud na Annasai.]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.