SOMO LA FIQHI
Suali: Ni ipi hukmu ya kufanga?
Jawabu: Hukumu ya kufunga saumu
Imegawanyika saumu ambayo Mwenyezi Mungu ameiweka katika sheria vigawanyo vifuatavyo:
1. SAUMU YA WAJIBU
Nayo iko sampuli mbili:
Sampuli ya kwanza: Ni Saumu aliyoiwajibisha Mwenyezi Mungu Subhanahu Wataala kwa waja wake. nayo ni saumu ya kufunga mwezi wa Ramadhani, na saumu hii ni nguzo moja wapo katika nguzo za Uislamu.Kama alivyo sema Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ} البقرة:183
[Enyi mlo Amini! Mmeandikiwa Saumu, kama waliyo andkikwa walio kuwa kabla yenu ili mpate kucha mungu.” [Al-Baqara:183]
Na kama ilivyo kuja kwenye hadithi ya Bwana Mtume ﷺ:
بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان رواه البخاري ومسلم
[Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kwa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani] [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]
Sampuli ya pili: Ni Saumu ambayo kwamba mja ndiye anayekuwa sababu ya kuwajibishwa yeye mwenyewe kuifunga, kama vile saumu ya nadhiri na saumu ya kafara.
2. SAUMU ZA SUNNA
Nayo ni kila saumu ambayo kwamba sheria ya kiislamu imependekeza saumu hiyo kufungwa, kama kufunga siku ya Jumatatu na Alhamisi, na kufunga siku tatu za kila mwezi, na kufunga siku ya A’shura, na kufunga masiku kumi ya mwanzo wa mwezi wa Dhilhijja, na kufunga siku ya A’rafah.
MASHARTI YA KUWAJIBIKA KUFUNGA
Suali: Ni yapi Mashrti ya mtu kuwajibika Kufunga:
Jawabu: Masharti ya mtu kuwajibika Kufunga ni haya yafuatayo:
1. Uislamu: Haimlazimu kafiri kufunga.
2. Kubaleghe: Sio lazima kwa mtoto mdogo kufunga, lakini huamrishwa kufunga akiwa anaweza ili kumpa mazoezi ya saumu naye azoee.
3. Kuwa na akili: Sio wajibu kwa mwendawazimu kufunga.
4. Uwezo wa kufunga: Sio wajibu kufunga kwa mtu ambaye hawezi kufunga (labda amekuwa mzee sana ama afya yake haimruhusu kuhimili saumu).
5. Kwa Mwanamke asiwe kuwa kwenye ada yake ya Mwezi, au damu yanifasi.