0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

KUFUNGA MWEZI WA RAMADHANI NA FADHLA ZAKE

SOMO LA FIQHI

Kufunga mwezi wa Ramadhani ni nguzo mojawapo kati ya nguzo za Uislam, na ni lazima kufunga mwezi huu. Mwenyezi Mungu amewalazimisha waja wake kufunga.

Anasema Mwenyezi Mungu mtukufu:

{يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا كُتِبَ عَلَيْكُمُ الصِّيَامُ كَمَا كُتِبَ عَلَى الَّذِينَ مِن قَبْلِكُمْ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ}    البقرة:183

[Enyi mlioamini! Mmelazimishwa kufunga (Saumu) kama walivyolazimishwa waliokuwa kabla yenu ili mpate kumcha Mungu]        [Al-Baqarah –Aya 183].

Na amesema Mtume ﷺ:

بني الإسلام على خمس : شهادة أن لا إله إلا الله ، وأن محمدا رسول الله ، وإقام الصلاة ، وإيتاء الزكاة ، وحج البيت ، وصوم رمضان     رواه البخاري ومسلم

[Umejengwa Uislamu kwa mambo matano: Kushuhudia ya kwamba hapana mola apasaye kuabudiwa kawa hki isipokuwa Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni mja wake na ni Mtume wake, na kusimamisha Swala (tano za kila siku), na kutoa Zaka, na kuhiji nyumba tukufu (Al-ka’abah – ilioko Makkah), na kufunga Mwezi wa Ramadhani]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

FADHLA ZA MWEZI WA RAMADHANI

1. Kufunga na kusimama usiku katika mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa mtu ana imani na kutaraji malipo basi husamehewa madhambi yake yote yaliyopita. Amesema Mtume :

[مَنْ صَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ }  رواه البخاري ومسلم 

[Atakayefunga mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa ana imani na kutaraji malipo Atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia]    [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na akasema Mtume  ﷺ:

{مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ }     رواه البخاري ومسلم 

[Atakayesimama (kuswali usiku) funga mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa ana imani na kutaraji malipo Atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

2. Ndani ya mwezi wa Ramadhani kuna “Lailatu Al-Qadr”  Usiku wenye hishima kubwa’ ambao Mwenyezi Mungu aliyetukuka anamesema kuhusu usiku huu:

{إِنَّا أَنزَلْنَاهُ فِي لَيْلَةِ الْقَدْرِ  وَمَا أَدْرَاكَ مَا لَيْلَةُ الْقَدْرِ  لَيْلَةُ الْقَدْرِ خَيْرٌ مِّنْ أَلْفِ شَهْرٍ}

[Hakika Sisi tumeiteremsha Qur’ani katika Laylatul Qadri, Usiku wa Cheo Kitukufu.Na nini kitacho kujuulisha nini Laylatul Qadri?Laylatul Qadri ni bora kuliko miezi elfu.]      [Al-Qadr – Aya 3.]

Na mtu Atakayesimama usiku huu basi atasamehewa madhambi yake yote yaliyotangulia. Amesema Mtume Mtume :

[مَنْ قَامَ رَمَضَانَ إِيمَانًا وَاحْتِسَابًا غُفِرَ لَهُ مَا تَقَدَّمَ مِنْ ذَنْبِهِ ]     رواه البخاري ومسلم 

[Atakayesimama (kuswali usiku) funga mwezi wa Ramadhani hali ya kuwa ana imani na kutaraji malipo Atasamehewa madhambi yake yaliyotangulia]

3. Kufanya U’mrah ndani ya mwezi wa Ramadhani ni sawa na kuhiji pamoja na Mtume ﷺ. Amesema Mtume :

[عمرة في رمضان تقضي حجة معي]      رواه مسلم

[Kufanya U’mrah ndani ya Ramadhani ni sawa na kuhiji pamoja nami]     [Imepokewa na Muslim.]

4. Mwezi wa Ramadhani hufunguliwa milango ya peponi, na hufungwa milango ya motoni, na hutiwa minyororo (hufungwa) mashetani, na nafsi huelekea katika kufanya mambo ya kheri. Amesema Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtume ﷺ:

[إِذَا دَخَلَ رَمَضَانُ فُتِّحَتْ أَبْوَابُ الجَنَّةِ ، وَغُلِّقَتْ أَبْوَابُ جَهَنَّمَ ، وَسُلْسِلَتِ الشَّيَاطِينُ]      رواه البخاري ومسلم

[Unapoingia mwezi wa Ramadhani hufunguliwa milango ya Peponi, na hufungwa milango ya motoni, na hutiwa minyororo mashetani]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

5. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur’an, na ndiyo mwezi ulioteremshwa Qur’an, kwa hivyo inafaa kuzidisha kusoma Qur’an ndani ya mwezi huu, Anasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِي أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَىٰ وَالْفُرْقَانِ}      البقرة:185

[Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi.]       [Al-Baqarah: Aya 185]

 6. Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa ukarimu na kutoa sana sadaka. Imepokewa kutoka kwa Ibn Abbas radhi za Allah ziwe juu yake akisema:

كان رسول الله صلى الله عليهم وسلم أجود الناس وكان أجود ما يكون في رمضان حين يلقاه جبريل حين يلقاه جبريل وكان يلقاه في كل ليلة فيدارسه القران  فلرسول الله صلى الله عليه و سلم أجود بالخير من الريح المرسلة       رواه البخاري ومسلم

[Alikuwa Mtume ﷺ mkarimu sana kushinda watu wote katika kufanya mambo ya kheri, na alikuwa mkarimu zaidi wakati wa mwezi wa Ramadhani, hakika Jibril alikuwa akikutana na Mtume kila mwaka katika mwezi wa Ramadhani mpaka uishe mwezi, basi ikawa Jibril wakati kama huu anampitishia Mtume (anaregelea kusoma pamoja na Mtume) Qur’an, basi pindi Mtume anapokutana na Jibril alikuwa Mtume mkarimu sana katika mambo ya kheri kushinda upepo mkali uliotumwa]       [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.