AINA ZA IBADA YA HIJA
AINA ZA IBADA YA HIJA
Aina za ibada ya Hija ni Aina Tatu:
1. Tamattu:
Nayo ni ahirimie Umra katika miezi ya Hijja mpaka amalize na ajitoe kwenye ihramu yake, kisha katika mwaka huohuo ahirimie Hija.
Na mwenye kufanya tamattu’ anapo fika makka atafanya amali ya Umra nayo: Nikutufu, na kufanya sai kati ya Swafaa na marwa, na kunyoa au kupunguza, kisha atajitoa kwenye ihramu yake na avae nguo zake, ikifika tarehe nane mwezi wa mfungotatu, atahirimia hija kisha atafanya amali za hijja na atawajibika kuchinja kwa kupumzika kwake
2. Qiraan:
Nayo ni ahirimie Hijja na Umra kwa pamoja., au ahirimie Umra kisha anuilie kufanya hija kabla ya kuanza kufanya tawafu, na mwenye kufanya Qiraan atabaki kwenye ihramu yake mpaka amalize kufanya hija, na atalazimika kuchinja kwa kule kuhirimia pamoja kwa amali ya hija na umra.
3. Ifraad:
Nayo ahirimie Hijja peke yake.na mwenye kufanya ifraadi atabaki na ihramu zake mpaka amalize kuhuji na hatolazimika kuchinja.
Na nusuk bora katika hizo tatu ni tamattu kwa sababu Mtume ﷺ Aliwaamrisha maswahaba zake wafanye tamattu  [Kwa hadithi iliyopokewa na Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake iliyoko kwenye Sahihi ya Muslim.] Kisha ni Qiraan kisha ni Ifraad