0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ZAKA ZA MALI YA BIASHARA

SOMO LA FIQHI

Suali: Ni nini Maana ya Mali ya biashara?

Jawabu: Mali ya biashara ni kila kilichoandaliwa kwa lengo la kuuzwa na kununuliwa ili mtu apate faida.

Na bidhaa za biashara zimekusanya vitu vyote vya sampuli zote za mali ambayo sio pesa zinazotumika kununulia vitu, kama vile magari, nguo, vitambaa, vyuma, mbao, na vyenginevyo vilivyoandaliwa kwa biashara.

Suali: Ni ipi Hukumu ya zaka ya Mali ya biashara.?

Jawabu: Hukmu ya zaka ya mali ya biashara ni lazima; kwa kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu:

{أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا أَنفِقُوا مِن طَيِّبَاتِ مَا كَسَبْتُمْ وَمِمَّا أَخْرَجْنَا لَكُم مِّنَ الْأَرْضِ}    البقرة:267

[Enyi mlioamini! Toeni katika vile vizuri mlivyovichuma, na katika vile tulivyokutoleeni katika ardhi] [Al-Baqarah: 267].

Jumla ya wanavyuoni wametaja kwamba makusudio ya aya hii ni: Zaka ya mali ya biashara, na kwa kauli ya Mwenyezi Mungu mtukufu:

{خُذْ مِنْ أَمْوَالِهِمْ صَدَقَةً}    التوبة:103

[Chukua kutoka kwa mali zao sadaka]  [At-Tawbah: 103] ,

Na mali ya biashara ni katika mali zilizo dhahiri, basi Kwa ajili hii ikawajibika kutolewa zaka.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.