0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

YANAYOHARAMISHWA KWA AJILI YA HEDHI NA NIFASI

SOMO LA FIQHI

Yanayoharamishwa kwa ajili ya hedhi na nifasi

1. KUJAMIANA

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

{وَيَسْأَلُونَكَ عَنِ الْمَحِيضِ ۖ قُلْ هُوَ أَذًى فَاعْتَزِلُوا النِّسَاءَ فِي الْمَحِيضِ ۖ وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ}

[Na wanakuuliza juu ya hedhi. Waambie, huo ni uchafu basi jitengeni na wanawake wakati wa hedhi.wala msiwaingilie mpaka watahirike. Wakisha twahirika basi waendeni alivyo kuamrisheni mwenyezi mugnu.]    [2: 222]

Na kwa kauli ya Mtume ﷺ ilipoteremka aya hii:

[اصنعوا كل شيء إلا النكاح]       رواه مسلم

[Fanyeni kila kitu isipokuwa kuundama]   [Imepokewa na Muslim.].

MAELEZO
1. Mwenye kumuingilia mkewe na hali yuko katika hedhi hupata dhambi na itamlazimu kafara na huyo mke pia atoe kafara iwapo aliridhia.

Na kafara ni kutoa sadaka kadiri ya dinari moja au nusu dinari ya dhahabu, kwa hadithi ya Ibnu Abbas kumpokea Mtume ﷺ juu ya mtu anayemuingilia mkewe na hali yuko kwenye hedhi kuwa alisema:

[يتصدق بدينار أو بنصف دينار]    رواه أبوداد والنسائي

[Atatoa sadaka Dinari moja au nusu dinari]     [Imepokewa na Abuu Dawud na Annisaai.].

Dinari moja ni grama nne na robo za dhahabu.

2. Aliyoko hedhini akiingia twaharani, haifai kwa mumewe kumuundama (kumuingilia) mpaka aoge, kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka

{وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّهُ}

[Wala msiwaingilie mpaka watahirike. (kutokana na damu) Wakisha twahirika]  (yaani: wakaoga.) [basi waendeni alivyo kuamrisheni mwenyezi mugnu.]    yaani: kuundama.   [2: 222]

2. KUSWALI

Kwa neno lake Mtume :

[فإذا أقبلت الحيضة فاتركي الصلاة . فإذا ذهب قدرها ، فاغسلي الدم عنك وصلي]

[Ikija hedhi yako acha kuswali, na ikiondoka Mda wake basi Jisafishe damu kisha uswali]  [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

MAELEZO

1. Mwanamke haimlazimu kulipa swala akitwahirika, Kwa hadithi iliyothubutu kutoka kwa Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake kuwa aliulizwa juu ya aliyekuwa na hedhi kulipa Saumu na kutolipa Swala, akasema:

[كنا نحيض عند رسول الله صلى الله عليه وسلم فيأمرنا بقضاء الصيام ولا يأمرنا بقضاء الصلاة]     رواه البخاري ومسلم

[Tulikuwa tukipatwa na Hedhi wakati tukiwa na Mtume    akituamrisha kulipa saumu na wala hakutuamrisha kulipa Swala]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

2. Iwapo mwenye hedhi atawahi rakaa nzima ya wakati wa Swala, itamlazimu aswali, iwe ni rakaa ya mwanzo ya wakati au ya mwisho wake. Ikiwa atawahi sehemu ya wakati ambayo haikundukii rakaa moja, basi haimlazimu kuswali, kwa kauli ya Mtume :

[مَنْ أَدْرَكَ رَكْعَةً مِنْ الصَّلَاةِ فَقَدْ أَدْرَكَ الصَّلَاةَ]      رواه البخاري ومسلم

[Mwenye kuwahi rakaa moja ya Swala amewahi Swala]      [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

3. KUFUNGA SAUMU

Kwa kauli yake Mtume :

[Kwani akiingia katika hedhi si ataacha kuswali na kufunga? Wakasema (wanawake): “Ndiyo”]    [Imepokewa na Bukhari.].

MAELEZO
Akitwahirika mwenye hedhi kabla ya Alfajiri na akafunga, basi Saumu yake itakuwa sahihi, ingawa hakuoga mpaka baada ya Alfajiri

4. KUSHIKA MSAHAFU

Kwaneno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

{لَّا يَمَسُّهُ إِلَّا الْمُطَهَّرُونَ}     الواقعة:79

[Hawaigusi isipokuwa walitwahirishwa]   [56: 79]

Na kwa neno lake Mtume :

[لا يمس القرآن إلا طاهر]     رواه مالك في الموطأ

[Hagusi Qur’ani ila aliye twahara]    [Imepokewa na Malik katika Muwatta’]

5. KUTUFU AL KAABA
Kwa neno la Mtume  kumwambia Aisha Radhi za Allah ziwe juu yake

[افعَلي ما يفعَلُ الحاجُّ، غير ألَّا تطوفي بالبيتِ حتى تطهُرِي]    متفق عليه

[Fanya kile anachokifanya mwenye kuhiji isipokuwa usitufu Alkaaba mpaka uwe twahara]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

Na Asema Ibn ‘Abbas Radhi za Allah za Allah ziwe juu yake :

[أُمر الناس أن يكون آخر عهدهم بالبيت، إلا أن أنه خفف عن المرأة الحائض]      رواه البخاري ومسلم

[Wameamrishwa watu iwe mwisho wa kukutana kwao na Alkaaba ni kutufu, isipokuwa mwanamke mwenye hedhi amehafifishiwa hilo]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim.]

6. KUKAA MSIKITINI ISIPOKUWA KWA MPITA NJIA.

Kwa neno lake Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَقْرَبُوا الصَّلَاةَ وَأَنتُمْ سُكَارَىٰ حَتَّىٰ تَعْلَمُوا مَا تَقُولُونَ وَلَا جُنُبًا إِلَّا عَابِرِي سَبِيلٍ حَتَّىٰ تَغْتَسِلُوا}  النساء:43}

[Enyi mlioamini! Msikaribie swala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema, wala hali mna janaba isipo kuwa mmo safarini mpaka muoge]   [4: 43]

Na kwa neno la Mtume :

[لا أحل المسجد لحائض ولا لجنب]    رواه أبوداود بسند ضيف

[Mimi simhalalishii msikiti mwenye hedhi wala mwenye janaba]       [imepokewa na Abuu Daud kwa Isnadi dhaifu]

MAELEZO

1. Si makosa kwa mwenye hedhi kupita msikitini akijihifadhi na asichelee kuuchafua msikiti, kwa ujumla wa maneno ya Mwenyezi Mungu Aliyetuka: {Isipokuwa wapita njia} [4: 43]

2. Ni haramu kwa mwenye hedhi kukaa kwenye eneo la kuswalia Idi, kwa neno lake Mtume :

[وَيَعْتَزِلُ الحُيَّضُ المُصَلَّى]     رواه البخاري ومسلم

[Na wajiepushe na kuhudhuria mahali pa kuswali Idi]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim.].

7. TALAKA
Ni haramu kwa mume kumuacha mkewe akiwa na hedhi, kwa neno lake mwenyezi Mungu Aliyetukuka:

يَا أَيُّهَا النَّبِيُّ إِذَا طَلَّقْتُمُ النِّسَاءَ فَطَلِّقُوهُنَّ لِعِدَّتِهِنَّ وَأَحْصُوا الْعِدَّةَ}    الطلاق:1}

[Ewe Nabii! Mtakapo wapa talaka wanawake, basi wapeni talaka katika wakati wa eda zao. Na fanyeni hisabu ya eda]  [65: 1].

Yaani waelekee kwenye eda maalumu wakati wa kuachwa.

Na talaka ya mwenye hedhi inapita ingawa ni haramu na ni uzushi katika Dini.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.