0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

DAMU YA NIFASI MUDA WAKE NA HUKMU ZAKE

SOMO LA FIQHI

MAANA YA NIFASI

Nifasi: Ni damu inayotoka kwenye uzao wa mwanamke kwa sababu ya kuzaa

Muda wa Nifasi
Hakuna mpaka wa uchache wa nifasi. Ama wingi wake kwa kawaida ya wengi ni siku arubaini, isipokuwa akiona utwahara kabla ya hapo, Basi ataoga na aswali.

MIONGONI MWA HUKMU ZA DAMU YA NIFASI

1. Mwanamke akizaa na asione damu- na hii ni hali ya nadra sana- atatawadha na ataswali, na halazimiki kuoga.

2. Damu ikipita siku arubaini, na ikawa ada yake ni kukatika kwa kumalizika siku ya arubaini, au zikadhihiri alama za kukaribia kukatika, atangojea mpaka ikatike. Iwapo damu itaendelea, basi yeye ana istihadhah na itamthibitikia yeye hukumu za istihadhah.

3. Akitwahirika kabla ya siku ya arubaini, kisha damu ikamrudia ndani ya siku arubaini itamlazimu aangalie: .

a. Akijua kuwa ni damu ya nifasi, basi ni damu ya nifasi.

b. Na akijua kuwa si damu ya nifasi, basi hukumu yake ni kuwa yuko katika twahara.

4. Haithubutu damu kuwa ni ya nifasi isipokuwa akiwa amezaa kitu chenye umbo la binadamu, akiwa amezaa tisha- naye ni mtoto aliyetoka kwenye uzao wa mwanamke kabla ya umbo lake kukamilika- ambalo halijafafanuka kwake umbile la binadamu. Nalo lina hali tatu:

a. Iwe ni kabla ya siku arubaini za kwanza (za kushika mimba). Bila ya hivyo, hii itakuwa ni damu iliyoharibika, hivyo basi ataswali na atafunga.

b. Iwe ni baada ya siku thamanini. Na hii ni damu ya nifasi.

c. Iwe muda wake wa kukaa matumboni ni baina ya siku arubaini na thamanini. Na hii itatazamwa: Iwapo imeonesha alama ya kuwa ni kiumbe, basi hiyo ni damu ya nifasi. ikitokuwa hivyo, basi ni damu iliyoharibika

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.