UVUKAJI MIPAKA YA MASHIA KWA MAIMAMU WAO
• Mashia wanaitikadi kuwa Maimamu wao 12 ni Bora kuliko Manabii ,Mitume na Malaika Wote na huu ndio Msingi wa Dini yao.
• Amesema Ayatollah Al-Khomein:-
“وإن من ضروريات مذهبنا :أن لأئمتتا مقا لا يبلغه ملك مقرب ولا نبي مرسل”
الحكومة الاسلامية ص 54
“Na kwa hakika miongoni mwa misingi ya Madhehebu yetu( ya Kishia) ni kuwa Maimamu wetu wana Nafasi ambayo haifikii Malaika Mtukufu wala na Nabii alie tumwa”.
MAELEZO :-
• Ndugu muislamu hayo maneno alio yataja huyo Mwanachuoni wa Kishia ndio Msingi wa Dini ya Ushia ,Bila shaka ni Maneno ya Sharki ,Kufuru na Uvukaji wa Mipaka wa hali ya Juu ,na hii inaonesha Upotevu wa Kundi hili linalo jinasibisha na Uislamu .
• Kauli hii inajulisha kuwa Maimamu 12 wa Kishia akiwemo Ali ,Hassan ,Hussein na wengine wanajua Mambo yalio fichikana(Ghaibu) na wanashirikiana Sifa na Allaah (Azza wajallah) katika Sifa za Uungu,!!
• Mafundisho Sahihi ya Uislamu alio ufundisha Bwana Mtume Muhammad(Salla Allaahu alayhi wasallam) ni kuwa Hakuna ane jua Ghaibu ispokuwa Allaah pekee au yule alie mridhia katika Mitume.
• Itikadi Sahihi ya Uislamu ni hakuna Mtu ni Bora Kuliko Malaika,Mitume na Manabii,Ndugu muislamu chukua tahadhari sana na Ushia kwani una itikadi za Kikafiri .
• Pengine mtu anaweza jiuliza huyo Khomeini ni nani katika Dini ya Ushia!!?,Jawabu la Swali hili linajibiwa kwa kueleza historia fupi ya Bwana huyu .
• Khomeini jina lake ni Ruhollah Bin Mustafa Bin Ahmad Al-Musawi Al-Khomeini alizaliwa 1320 H, sawa na 24 Septembar 1902 AD,Huko Khomein ,Iran ni Kingozi wa Mapinduzi ya Uajemi(Iran )11February 1979,kwa kuung’oa Utawala wa Kifalme wa Shaah Muhammad Ridhaa ,na kuanzisha kile alicho kiita Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
• Bwana Khomeini alikuwa Kiongozi Mkuu wa Kidini (Roho) na Marejeo ya Dini ya Ushia kuanzia mwaka 1979 hadi alipo fariki 3 Juni Mwaka 1989,Tehran ,Iran.
Katika picha hapo chini ndio Bwana Khomeini
• Kwa makala mbali mbali zenye kuelemisha kuhusu Uislamu Sahihi alio ufundisha Bwana Mtume Muhammad(Salla Allaahu alayhi wasallam)tembelea Kurasa zetu za Facebook,Instagrm na Twitter kwa jila la (Ally Al-Qusheiry )
Wabillah Taufiq.
Muandishi:-
Ally Yahya Al-Qusheiry
Dar es Salaam,Tanzania
+255652082775