0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ITIKAADI YA MASHIA KUHUSU MAKHALIFA ABUBAKAR ,OMAR NA OTHUMAN

ITIKAADI YA MASHI KUHUSU MAKALIFA WA TATU

Mashia wanaitikadi kuwa Maswahaba Watukufu mfano Abubakar,Omar ,Othuman ni Watu waovu mno ,Makafiri,Wanafiki na Masanamu.

Amesema Al-Majilis :-

“وعقيدتنا أننا نتبرأ من الأصنام الأربعة :أبي بكر وعمر وعثمان ومعاوية ,والنساء الأربع عائشة وحفصة وهند وأم الحكم ,ومن جميع أتباعهم وأشياعهم وأنهم شر خلق الله على وجه الأرض وأنه لا يتم الايمان بالله ورسوله والأئمة إلا بعد التبرؤ من أعدائهم “

حق اليقين ص 519

“Na Itikaadi yetu (Sisi Mashia) ni kujiweka mbali na Masanamu wanne Abubakar,Omar,Othuman na Muaawiya,Vivile kujiweka mbali na Wanawake wanne ,Aisha,Hafswa,Hindu na Umu Hakam,na watu wote amabo ni wafusi wao na wanawafata,na hakika watu hao ni viumbe wa Allaah ambao ni waovu zaidi katika katika Ardhi,na kuwa hakika Imaani ya Kumuamini Allaah na Mtume wake(Salla Allaahu alayhi wasallam) na Maimamu (wao 12) haitimii ila kukaa mbali na Maadui zao”.

MAELEZO :-

Ndugu muislamu maneno alio yasema huyu mwanawachuoni wa Kishia ,hivi ndiyo ilivyo Itikaadi ya Dini ya Uishia ambayo ni Tofauti kabisa na Mafundisho Sahihi alio yafundisha Bwana Mtume Muhammad(Salla Allaahu Alayhi wasallam).

Itikaadi Sahihi ya Uislamu alio ifundisha Mtume Muhammad (ﷺ) ni kuitikadi kuwa Maswahaba wa Mtume ni Watu bora baada ya Mtume Mwenyewe ,na mtu mbora baada ya Mtume (Salla Allaahu alayhi wasallam) ni Abubakar Al-Swidiiq ,kisha Oma Bin Khatwaab,kisha Othuman Bin Afan,kisha Ali Bin Abi Twaalib(Allaah awaridhie wote) hivi ndio ambavyo anatakiwa muislamu aitikadi na aamini ,na wala si kama wanavyo itikaadi Mashia.

Kila muislamu ana wajibu wa kuwaheshimu na Kuwapenda Wake za Bwana Mtume Muhammad (ﷺ) akiwa Aisha Bint Abibakar,na Hafswa Bint Omar(Allaah awaridhie) ,Na kuamini kuwa ni Mama wa Waumini .

Kuwavujia heshima Wake za Bwana Mtume Muhammad (ﷺ) ni Kuvunjia heshima Mtume (ﷺ).

Ndugu msomaji maneno alio yataja huyu Sheikh wa Kishia Kuna Nukta kadhaa za Kuzingatia kama ifuatavyo :-

(i) Maishia wanaitikadi kuwa Maswahaba Kina Abubakar ,Omar ,Othuman ,Muawiya ,Aisha ,Haswa ni Makafiri si Waislamu .

(ii) Mashia wanaitikadi kuwa Maswahaba hao na wengine kuwa ni Masanamu ,bila shaka haya ni matusi kwa Maswababa.

(iii) Maswahaba wa Mtume (ﷺ) ndio viumbe waovu kuliko waote katika Dunia hii.Bila shaka haya ni maneno ya Ukafiri na Uzandiki.

(iv) Waislamu ambao wanawapenda Maswahaba hao na wengine ni Watu waovu mno kwa Allaah.

(v) Msingi wa Imaani na Itiaakadi ya Dini ya Ushia ni kuwa huwezi kuwa Mshia hadi kuitikadi kuwa Maswahaba kama Abubakar ,Omar,Othuman ,Aisha ,Hafswa na wale wote wanao wapenda na kuwanusuru watu hawa kuwa ni Makafiri na Wanafiki ,na uwe mbali nao hapo ndio umekuwa Shia.

Ndugu muislamu hayo alieo yasema huyo bwana hapo juu ni Sehemu tu ya Itikaadi ya Dini ya Ushia,hivyo chukua tahadhari na Ushia ni kundi lenye Itikaadi za Kikafiri.

Allaah atuepushe na balaa hili.

Wabillah Taufiiq

Muandishi :-
Ally Yahya Al-Qusheiry
Dar es Salaam,Tanzania


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.