0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UTANGULIZI DARAJA YA MASAHABA KATIKA UISLAMU

DARAJA YA MASAHABA KATIKA UISLAMU

Ni nani Sahaba?
Sahaba ni kila aliyekutana na Mtume ﷺ na akamuamini na akafa juu ya imani ya UIslamu.
Mwenyezi Mungu aliyetukuka amewasifu Masahaba katika Qur’ani Aliposema:

{وَالسَّابِقُونَ الْأَوَّلُونَ مِنَ الْمُهَاجِرِينَ وَالْأَنصَارِ وَالَّذِينَ اتَّبَعُوهُم بِإِحْسَانٍ رَّضِيَ اللَّهُ عَنْهُمْ وَرَضُوا عَنْهُ}

[Na wale waliotangulia wakawa wa kwanza katika UIslamu miongoni mwa Muhajirina (Watu. wa Makkah) na Maansari (watu wa Madinah) na wale waliowafuata kwa mwendo mzuri Allah (Jalla Jalaaluh) atawapa radhi na wao wamridhie. [9:100]
Na neno lake Mwenyezi Mungu Mtukuf:

{لَّقَدْ رَضِيَ اللَّهُ عَنِ الْمُؤْمِنِينَ إِذْ يُبَايِعُونَكَ تَحْتَ الشَّجَرَةِ فَعَلِمَ مَا فِي قُلُوبِهِمْ فَأَنزَلَ السَّكِينَةَ عَلَيْهِمْ وَأَثَابَهُمْ فَتْحًا قَرِيبًا}

[Hakika Mwenyezi Mungu amewapa radhi WaIslamu walipofungamana nawe chini ya mti, na Alijua yalio nyoyoni mwao. Basi Akateremsha utulivu kwao, na Akawapa ushindi kwa zama za karibu.]   [48:18]

Akasema tena Mwenyezi Mungu katika aya nyingine:

مُّحَمَّدٌ رَّسُولُ اللَّهِ ۚ وَالَّذِينَ مَعَهُ أَشِدَّاءُ عَلَى الْكُفَّارِ رُحَمَاءُ بَيْنَهُمْ ۖ تَرَاهُمْ رُكَّعًا سُجَّدًا يَبْتَغُونَ فَضْلًا مِّنَ اللَّهِ وَرِضْوَانًا ۖ سِيمَاهُمْ فِي وُجُوهِهِم مِّنْ أَثَرِ السُّجُودِ

[Muhammad ni Mtume wa Mwenyezi Mungu. Na walio naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya msksiiri na wen ye kuhurumiana baina yao. Utawaona wenye kuinama kwa kurukuu na kusujudu (pemojs) wakitafuta Isdhils za Mwenyezi Mungu na radhi Zeke, alama zao zi katiks nyuso zao kwa athariya kusujudu.]   [48:29]

Na amesema Mwenyezi Mungu katika Aya nyingine, katika Qur’ani:

{كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ}

[Nyinyi ndio Umma bore kuliko Umma zote zilizodhihirishiwa wetu.]    [3:110]

Na Mtume (s.a.w,) pia amewasifu Masahaba kama alivyopokea ‘Imraan bin Husweyn ,radhi za Allah ziwe juu yake

عن عمران بن حصين رضي الله عنهما قال: قال رسول الله صلى الله عليه وسلم: خير أمتي قرني، ثم الذي يلونهم، ثم الذين يلونهم

Mtume ﷺ amesema: [Bora katika Umati wangu, ni karne yangu, kisha ni ile karne inayofuata, kisha ni ile karne inayofuata. kisha ni ile karne inayofuata.]   [Bukhari, na Muslim,]

لا تسبوا أصحابي، لا تسبوا أصحابي، فوالذي نفسي بيده لو أن أحدكم أنفق مثل أحد ذهبا ما أدرك مُدّ أحدهم ولا نصيفه    أخرجه البخاري ومسلم

Imepokewa kutoka kwa Abu Said AI-Khudry radhi za Allah ziwe juu yake kuwa amesema Mtume ﷺ: [Musiwatukane Masahaba wangu. naapa kwaJule Ambaye nafsi yangu iko mkononi Mwake, lau angetoaj mmoja we nu dhahabu ukubwa wake kama jabali la Uhud, basi asingefrkia thawabu zake kibaba cha mmoja wao wala nusu yake.]   [Bukhari, No:3673 Muslim, No.-2541. Abu Deud, No.’4658]

Na makusudio ya Mtume ﷺ aliposema: “Mmoja wenu” katika Hadithi ni wale waliosilimu baada ya mapatano ya Hudaybia.

Ni wajibu kwa Waislamu kuwapenda Masahaba wote wa Mtume ﷺ na  kuwa na itikadi yakua kuwapenda Masahaba ni katika Imani ya Dini: na kuwachukia ni ukafiri na unafiki, na ni kukengeuka sheria za Dini.

Na mbora zaidi katika Masahaba ni Abu Bakar kisha ‘Umar kisha ‘Uthman kisha ‘Ali (r.a.). Hao ndio Makhalifa wanne walio waongofu. Wakafuatiliwa na wengine kwa ubora. Aliowataja Mtume ﷺ miongoni mwa Masahaba kumi waliobashiriwa Pepo. Miongoni mwa hao kumi ni

Makhalifa wanne waliotangulia kutajwa, sita waliobaki ni

Talhah ibn ‘Ubaydullah.

Zubayr ibn Al Awwam,

Sa’d ibn Abi Waqqas,

Sa’id ibn Zayd,
‘Abdur-Rahman ibn ‘Auf,

na Abu ‘Ubaydah ‘Amir ibn AlJarrah (r.a).

Masahaba wote wa Mtume ﷺ ni wadilifu, wa kutegemeka, waumini, tena ni wema. Wala si ma’ sumina (waliohifadhiwa na kufanya madhambi na maasi). Lakini wao wako mbali na madhambi, na wako karibu zaidi na kutubia kwa Mwenyezi Mungu. Basi yule atakayewataja kwa wema hao Masahaba na wakeze Mtume walio ‘tahara, pamoja na banati zake Mtume ﷺ hakika huyo ameepushwa na unafiki.

Waislamu hawajishughulishi na kila habari inayoelezea maovu ya Masahaba, bali huzichukulia habari hizo kuwa ni uongo na vitimbi vya Mayahudi na Majusi, pamoja na wafuasi wao katika wanafiki na watu wajinga.

Hakika walikuwa Masahaba ni Mwangaza wenye kung’aa katika zama hizo na walikuwa ni nuru iliyoangaza katika mistari ya tarekhe ya Kiislamu. Na haya ndiyo yaliyowafanya wapendwe na Waislamu na kuheshimika.

Amatofauti ay fitna au vita vilivyotokea kati yao zilikuwa ni jitihada zao kwa lengo la kutafuta radhi za Mola wao. Waliosibu wana malipo mara mbili na waliokosea basi wana malipo mara moja.

Na hapana shaka kwamba kuuwawa kwa MaKhalifa watatu: ‘Umar, ‘Uthman na ‘Ali (r.a.) ni kutokana na mipango na vitimbi vya Maadui wa uislamu katika Mayahudi, Majusi na wanafiki ambao Uislamu uliangamiza njama zao za uovu na ukafiri wao. Na Makhalifa hao wote waliuwawa wakiwa mashahidi, Insha-Allah.

*Makhalifa Waongofu Uk.12-14

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.