0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UONGOZI DHALIMU 2 (KUZALIWA KWA MUSA ALAYHI SALAAM)

UONGOZI DHALIMU

KUZALIWA KWA MUSA (Alayhi salaam)

kuzaa au kuzaliwa nijambo lakawaida kwa binadamu wanyama na hata miti. Issa (Alayhi salaam) utukufu wake ulianza kwa jinsi mamake alivyopata mimba soma Qur’ani:

وَاذْكُرْ فِي الْكِتَابِ مَرْيَمَ إِذِ انتَبَذَتْ مِنْ أَهْلِهَا مَكَانًا شَرْقِيًّا  فَاتَّخَذَتْ مِن دُونِهِمْ حِجَابًا فَأَرْسَلْنَا إِلَيْهَا رُوحَنَا فَتَمَثَّلَ لَهَا بَشَرًا سَوِيًّا  قَالَتْ إِنِّي أَعُوذُ بِالرَّحْمَٰنِ مِنكَ إِن كُنتَ تَقِيًّا  قَالَ إِنَّمَا أَنَا رَسُولُ رَبِّكِ لِأَهَبَ لَكِ غُلَامًا زَكِيًّا  قَالَتْ أَنَّىٰ يَكُونُ لِي غُلَامٌ وَلَمْ يَمْسَسْنِي بَشَرٌ وَلَمْ أَكُ بَغِيًّا  قَالَ كَذَٰلِكِ قَالَ رَبُّكِ هُوَ عَلَيَّ هَيِّنٌ ۖ وَلِنَجْعَلَهُ آيَةً لِّلنَّاسِ وَرَحْمَةً مِّنَّا ۚ وَكَانَ أَمْرًا مَّقْضِيًّا    مريم:16-21

[Na mtaje Maryamu katika Kitabu, pale alipo jitenga na jamaa zake mahali upande wa mashariki.Na akaweka pazia kujikinga nao. Tukampelekea Roho wetu, akajifananisha kwake sawa na mtu.(Maryamu) akasema: Hakika mimi najikinga kwa Mwingi wa Rehema aniepushe nawe, ukiwa ni mchamngu.(Malaika) akasema: Hakika mimi ni mwenye kutumwa na Mola wako Mlezi ili nikubashirie tunu ya mwana aliye takasika.Akasema: Nitampataje mwana hali mwanaadamu yeyote hajanigusa, wala mimi si kahaba?(Malaika) akasema: Ndio hivyo hivyo! Mola wako Mlezi amesema: Haya ni mepesi kwangu! Na ili tumfanye kuwa ni Ishara kwa watu, na Rehema itokayo kwetu, na hilo ni jambo lilio kwisha hukumiwa.]     [Maryam:16-21]

na haya ndio yamewachanganya wenzetu wanaoona yesu ( ISSA Alayhi salaam) ni Mungu kwa kuwa hakuzawa kawaida.

Ama kwa Musa (Alayhi Salaam) utukufu wa mazazi yake yalianza kwa wahyi alopewa mamake musa wa kuwa na plan (A) myonyeshe soma Qur’ani suratul Qaswas Aya 7

{وَأَوْحَيْنَا إِلَىٰ أُمِّ مُوسَىٰ أَنْ أَرْضِعِيهِ ۖ }   قصص:7

[Tulimfunulia mama yake Musa kwa kumwambia: Mnyonyeshe.]

plan (B) mrushe kwa bahari ukiogopa soma Qur’ani:

{فَإِذَا خِفْتِ عَلَيْهِ فَأَلْقِيهِ فِي الْيَمِّ وَلَا تَخَافِي وَلَا تَحْزَنِي ۖ إِنَّا رَادُّوهُ إِلَيْكِ وَجَاعِلُوهُ مِنَ الْمُرْسَلِينَ}

Na utakapo mkhofia basi mtie mtoni, na usikhofu wala usihuzunike. Hakika Sisi tutamrudisha kwako na tutamfanya miongoni mwa Mitume.] 

hapa kwa plan (B) mrushe au muweke kwa bahari ndio ushindi na utukufu wa musa juu ya udhalimu waanza.
Mazazi ya musa yafungamana na bahari na yaashiria uongozi Dhalimu utaangamizwa na bahari ,kama inavyoashiria kuwa musa alipofikiwa kuangamizwa akiwa na miezi mitatu Allah alitumia bahari kumnusuru na alipokuwa akimbia ataka angamizwa akiwa mtu mzima Allah pia alitumia bahari kumnusuru, na kwa utawala wake alitumia bahari kuangamiza upotofu wa Firaauni.Kwa maana kama kwamba plan (B) ambao ilikuwa bahari inaashiria makubwa kwa Musa Alayhi salaam kuanza kuzaliwa.

Musa bin imraan yashikana nasaba yake na yaakub (Alayhi salaam) , na asli ya musa kuzaliwa misri ni natija ya maonevu na uhasidi walofanya nduguze Yussuf Alayhi salaam. kwa Yusuf walipomtupa kwa kisimani kisha kusingizia kuliwa na mbwa mwitu soma Qur’ani suratu Yusuf aya ya 17

{قَالُوا يَا أَبَانَا إِنَّا ذَهَبْنَا نَسْتَبِقُ وَتَرَكْنَا يُوسُفَ عِندَ مَتَاعِنَا فَأَكَلَهُ الذِّئْبُ ۖ وَمَا أَنتَ بِمُؤْمِنٍ لَّنَا وَلَوْ كُنَّا صَادِقِينَ}

[Wakasema: Ewe baba yetu! Hakika tulikwenda kushindana na tukamwacha Yusuf penye vitu vyetu. Basi mbwa mwitu akamla. Lakini wewe hutuamini ijapo kuwa tunasema kweli.]

alafu kuokotwa na msafara kutoka misri na kuuzwa kama mtumwa kwa mtukufu wa misri (wengine waona ni mfalme) kama kinavyo julikana kisa cha Yusuf Alayhi salaam.

MAFUNGAMANO YA YUSSUF NA MUSA (A.S)

1) Yussuf alitupwa kwa kisima alipokuwa kijibarobaro kwa malengo yakuangamizwa na nduguze wawe bora na kupendeza kwa baba yao, Musa alitupwa kwa bahari kwa malengo ya kumkimbiza kuchinjwa na jeshi la firaaun

2) mke wa firauun matarajio yake yalikuwa huenda Musa Alayhi Salaam atawafaa au wamfanye mtoto wamlee, Ama kwa Yussuf mtukufu wa misri ndie alimnumua yussuf na kumpelekea mkewe kwa malengo yale yale ya mke wa firaaun.

MAFUNZO KATIKA KISA CHA KUZALIWA MUSA ALAYHI SALAAM

1)Musa ambae alizaliwa huku uoga na hadhari umetanda nyumba na familia yake kwa kuwa akijulikana atachinjwa Allah alimpangia aishi kwa Qasri ya ufalme ili apate malezi yakutoogopa na kujuana na wengi ambao wako kwa utawala wa misri pamoja na kujua siri ya serekali dhalimu.

2)Musa kuwa kwa Qasri ya utawala kuanzia udogoni mwake ilimpatia nguvu na uwezo wa kupambana na dhulma kwa sababu malezi ya banii israeel yalikuwa yaunyonge na kunyanyaswa na uongozi wahitaji malezi yakujiamini zaidi , haya hayangepatikana nyumbani kwao.
3) maskini na wanyonge hawafai kujidharau Musa aliandawa kukomboa banuu israeel wakati watu wake wamekata tamaa hata ya uhai wake , hivyo ndivyo alivyokuwa Yussuf A.S utukufu ulikuja baada ya dhiki na mitihani mikubwa na hata kufungwa jela .

Dr.Majid Hobeni
College of islamic studies mombasa

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.