0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

ULINGANIZI WA MITUME

ULINGANIZI WA MITUME

Kazi kubwa ya Mitume ni ulinganizi. Mitume wote walitumwa kuwalingania viumbe kushikamana na Tawhidi. Tawhidi ndio msingi wa ulinganizi.
Amesema Mwenyezi Mungu Subhaanahu wa Taala:

{وَلَقَدْ بَعَثْنَا فِي كُلِّ أُمَّةٍ رَّسُولًا أَنِ اعْبُدُوا اللَّهَ وَاجْتَنِبُوا الطَّاغُوتَ ۖ}    النحل:36

[Na kwa hakika kwa kila umma tuliutumia Mtume kwamba: Muabuduni Mwenyezi Mungu, na muepukeni Shetani.]    [Al-Nnahl:36]

Mitume ya Allâh ni watu waliochaguliwa walio bora ushahidi neno Lake Allâh Subhaanahu wa Taala:

{قَالُوا يَا صَالِحُ قَدْ كُنتَ فِينَا مَرْجُوًّا قَبْلَ هَٰذَا ۖ أَتَنْهَانَا أَن نَّعْبُدَ مَا يَعْبُدُ آبَاؤُنَا وَإِنَّنَا لَفِي شَكٍّ مِّمَّا تَدْعُونَا إِلَيْهِ مُرِيبٍ}   هود:62

[Wakasem a: Ewe Saleh! Hakika kabla ya haya ulikuwa unatarajiwa kheri kwetu. Je, unatukataza tusiwaabudu waliyo kuwa wakiwaabudu baba zetu? Na hakika sisi tuna shaka na wasiwasi kwa hayo unayo tuitia.]   [Huud:62]
Na Neno Lake Allah  Subhaanahu wa Taala:

{وَاذْكُرْ عِبَادَنَا إِبْرَاهِيمَ وَإِسْحَاقَ وَيَعْقُوبَ أُولِي الْأَيْدِي وَالْأَبْصَارِإِنَّا أَخْلَصْنَاهُم بِخَالِصَةٍ ذِكْرَى الدَّارِ  وَإِنَّهُمْ عِندَنَا لَمِنَ الْمُصْطَفَيْنَ الْأَخْيَارِ}    ص:45}

[Na wakumbuke waja wetu, Ibrahim na Is-haqa na Yaa’qubu walio kuwa na nguvu na busara.Sisi tumewakhusisha wao kwa sifa ya ukumbusho wa Akhera. Na hakika wao kwetu sisi ni wateuliwa walio bora. ]  [Swaad:45]
Mitume wote walikuja na ulinganizi mmoja. Wote waliwaambia wafuasi wao kufuata maamrisho ya Mwenyezi Mungu na kujiepusha na makatazo yake.

MFUMO WA ULINGANIZI

Kutanguliza Tawhidi kuliko ibada nyingine. ‘Abdullah bin ‘Abbass amesema: Mtume ﷺ alimwambia Mu’adh Ibn Jabal Radhi za Allah zimfikie yeye wakati alipomtuma kwenda Yemen:

إنك ستأتي قوما أهل كتاب، فإذا جئتهم فادعهم إلى أن يشهدوا أن لا إله إلا الله، وأن محمدا رسول الله، فإن هم أطاعوا لك بذلك فأخبرهم أن الله فرض عليهم خمس صلوات كل يوم وليلة، فإن هم أطاعوا لك بذلك، فأخبرهم أن الله فرض عليهم صدقة تؤخذ من أغنيائهم فترد على فقرائهم، فإن هم أطاعوا لك بذلك فإياك وكرائم أموالهم، واتق دعوة المظلوم فإنه ليس بينها وبين الله حجاب

[Hakika unawaendea watu ambao ni Ahlul-Kitâb. Utakapowaendea, walinganie washuhudie kuwa hakuna mola anayestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa Allâh, na kuwa mimi ni Mtume wa Allâh. Watakapokutii kwa hilo, wajulishe kuwa Allâh Amewafaradhia Swala tano kila mchana na usiku. Watakapokutii kwa hilo, wajulishe kuwa Allâh Amewafaradhia Zaka, inachukuliwa kutoka kwa matajiri wao na wanarudishiwa mafukara wao. Watakapokutii katika hilo, basi tahadhari mali yao yenye thamani. Na uogope dua ya mwenye kudhulumiwa, kwani hakuna pazia baina ya dua hiyo na Allâh].    [Imepokwea na Bukhary]

Kutumia Lugha inayo fahamika na walinganiwa. Ushahidi ni Neno Lake Allâh Subhaanahu wa Taala:

{وَمَا أَرْسَلْنَا مِن رَّسُولٍ إِلَّا بِلِسَانِ قَوْمِهِ لِيُبَيِّنَ لَهُمْ ۖ فَيُضِلُّ اللَّهُ مَن يَشَاءُ وَيَهْدِي مَن يَشَاءُ ۚ وَهُوَ الْعَزِيزُ الْحَكِيمُم}   إبراهيم:4

[Na hatukumtuma Mtume ila kwa ulimi wa kaumu yake ili apate kuwabainishia. Basi Mwenyezi Mungu humuacha akapotea amtakaye, na akamwongoa amtakaye. Naye ni Mtukufu Mwenye nguvu na Mwenye hikima.]   [Ibrahim:4]

Amesema Mtume ﷺ :
[Atakapowajia mkarimu wa watu basi mkirimuni]. [Imepokewa na Ibu Majah.]

Mwangalie Nabii Nuh aliwaambia watu wake: Wala mimi si wa kuwafukuza Waumini. Mimi si chochote ila ni Mwonyaji wa dhahiri shahiri. Wakasema: Ikiwa huachi, ewe Nuhu, bila ya shaka utapigwa mawe. Akasema: Mola wangu Mlezi! Hakika watu wangu wamenikanusha. Basi Hukumu baina yangu na wao kwa Hukumu Yako, na Uniokoe na walio pamoja nami, Waumini.
Kuchagua washirika wazuri katika kusaidiana kulingania watu. Ushahidi ni Neno Lake Allâh(Subhaanahu wa Taala)Alipomfanya Musa waziri wake kuwa ni Harun:

{وَاجْعَل لِّي وَزِيرًا مِّنْ أَهْلِي هَارُونَ أَخِي اشْدُدْ بِهِ أَزْرِي وَأَشْرِكْهُ فِي أَمْرِي كَيْ نُسَبِّحَكَ كَثِيرًا وَنَذْكُرَكَ كَثِيرًا}   طه:29-34

[Na nipe waziri katika watu wangu, Harun, ndugu yangu. Kwake yeye niongeze nguvu zangu. Na umshirikishe katika kazi yangu. Ili tukutakase sana. Na tukukumbuke sana.]  [Twaha:29-34]

{قَالَ يَا قَوْمِ أَرَأَيْتُمْ إِن كُنتُ عَلَىٰ بَيِّنَةٍ مِّن رَّبِّي وَآتَانِي مِنْهُ رَحْمَةً فَمَن يَنصُرُنِي مِنَ اللَّهِ إِنْ عَصَيْتُهُ ۖ فَمَا تَزِيدُونَنِي غَيْرَ تَخْسِيرٍ}    هود:63

[Akasema: Enyi watu wangu! Mwaonaje ikiwa ninazo dalili zilizo wazi kutokana na Mola wangu Mlezi, naye akawa kanipa rehema kutoka kwake – je, ni nani atakaye ninusuru kwa Mwenyezi Mungu nikimuasi? Basi nyinyi hamtanizidishia ila khasara tu.]   [Huud:63]
Mwangalie Mtume Muhammad ﷺ, Aliposema Allah Subhaanahu wa Taala:

وَإِن كَادُوا لَيَفْتِنُونَكَ عَنِ الَّذِي أَوْحَيْنَا إِلَيْكَ لِتَفْتَرِيَ عَلَيْنَا غَيْرَهُ ۖ وَإِذًا لَّاتَّخَذُوكَ خَلِيلًا وَلَوْلَا أَن ثَبَّتْنَاكَ لَقَدْ كِدتَّ تَرْكَنُ إِلَيْهِمْ شَيْئًا قَلِيلًا إِذًا لَّأَذَقْنَاكَ ضِعْفَ الْحَيَاةِ وَضِعْفَ الْمَمَاتِ ثُمَّ لَا تَجِدُ لَكَ عَلَيْنَا نَصِيرًا   الإسراء:73-74

[Na hakika walikaribia kukushawishi uache tuliyo kufunulia ili utuzulie mengineyo. Na hapo ndio wangeli kufanya rafiki , Na lau kuwa hatukukuweka imara ungeli karibia kuwaelekea kidogo. Hapo basi bila ya shaka tungeli kuonjesha adhabu mardufu ya uhai, na adhabu mardufu ya kifo. Kisha usinge pata mtu wa kukunusuru nasi.]   [Al-Israai:73-75]
Aya na Hadithi zinabainisha wazi mfumo wa Mitume ya Allah katika kulingania wanadamu. Na haya ni mafundisho kwa kila Muislamu atakaye fanya kazi hii ya mitume. Ni lazima afuate mfumo sahihi wa kulingania nayo ni mfumo wa Mitume.

KWA FAIDA ZAIDI SIKILA MADA HII NA SHEIKH ABUU HAMZA

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.