0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

UKATI NAKATI KATIKA QUR’ANI NA SUNNA

UKATI NAKATI KATIKA QUR’ANI NA SUNNA

Makusudio ya Ukati na kati ni mfumo na njia ya kufuata Qur’an na Sunna za Mtume Swalla Llahu ‘alayhi wasallam bila ya kuzidisha au kupunguza. Na huo ndio mfumo wa Mtume na Masahaba zake na watu wema walio tangulia. Dini ya Kiislamu imekamilika, hakuna mtu ambae atakuja baada ya Mtume na kudai ana mambo ya ziada katika dini. Na vile vile, hakuna mtu ambae atadai ya upungufu wa Dini. Njia zote mbili hazikubaliki, kwasababu, Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala) Amesema:

{الْيَوْمَ أَكْمَلْتُ لَكُمْ دِينَكُمْ وَأَتْمَمْتُ عَلَيْكُمْ نِعْمَتِي وَرَضِيتُ لَكُمُ الْإِسْلَامَ دِينًا}    المائدة:3

[Leo nimekukamiliishieni Dini yenu, na nimekutimizieni neema yangu, na nimekupendeleeni UISLAMU uwe ndiyo Dini. ]   [Al-Maaida:3]
Na Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Taala)

{إِنَّا نَحْنُ نَزَّلْنَا الذِّكْرَ وَإِنَّا لَهُ لَحَافِظُونَ}     الحجر:9

[Hakika Sisi ndio tulio teremsha Ukumbusho huu, na hakika Sisi ndio tutao ulinda.]     [Al-Hijr:9]
Kwa hivyo, Mfumo na Manhaj ya dini ya Kiislamu ni moja nayo ni kufuata Qur’an na Sunna bila ya ziada wala kupunguza.

UKATI NAKATI KATIKA QUR’ANI

Maelezo ya neno lake Allah Subhaanahu wa Taala Aliposema:

{وَكَذَٰلِكَ جَعَلْنَاكُمْ أُمَّةً وَسَطًا لِّتَكُونُوا شُهَدَاءَ عَلَى النَّاسِ وَيَكُونَ الرَّسُولُ عَلَيْكُمْ شَهِيدًا ۗ}      البقرة:143

[Na vivyo hivyo tumekufanyeni muwe Umma wa wasitani, ili muwe mashahidi juu ya watu, na Mtume awe ni shahidi juu yenu.]    [Al-Baqara:143]

Kwa sababu Allah amewaeleza vizuri katika Qu’rani Aliposema Subhaanahu wa Taala:

كُنتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ ۗ وَلَوْ آمَنَ أَهْلُ الْكِتَابِ لَكَانَ خَيْرًا لَّهُم ۚ مِّنْهُمُ الْمُؤْمِنُونَ وَأَكْثَرُهُمُ الْفَاسِقُونَ   آل عمران:110

[Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.]    [Al-Imraan:110]

Ulinganizi wa Mitume wote ulikuwa Mfumo wake na Wakati Na kati
Ushahidi wake ni neno la Mtume lililopokewa kwa Abu Huraira Radhi zaAllah ziwe juu yake amesema Amesema  Mtume ﷺ:

[إن الدين يسر، ولن يشاد أحد الدين إلا غلبه، فسددوا وقاربوا وأبشروا]     رواه البخاري

[Hakika dini ni nyepesi wala mtu hatoifanyia dini mkazo isipokuwa itamshinda fanyeni usawa na karibisheni na mubashirie mazuri].    [Imepokewa na Bukhari]
Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

{قُلْ إِنَّ صَلَاتِي وَنُسُكِي وَمَحْيَايَ وَمَمَاتِي لِلَّهِ رَبِّ الْعَالَمِينَ}      الأنعام:162

[Sema: Hakika Sala yangu, na ibada zangu, na uhai wangu, na kufa kwangu, ni kwa ajili ya Mwenyezi Mungu, Mola Mlezi wa viumbe vyote.]    [Al-An’aam:162]

Ndugu Muislamu, Hapana shaka Mwenyezi Mungu anawaamrisha kati ya watu kuhukumu kwa uadilifu. Hapana shaka Allah anawapa mawaidha mazuri, hapana shaka Allah ni mwenye kusikia, kuona.
Na amesema Allah Subhaanahu wa Taala:

وَابْتَغِ فِيمَا آتَاكَ اللَّهُ الدَّارَ الْآخِرَةَ ۖ وَلَا تَنسَ نَصِيبَكَ مِنَ الدُّنْيَا ۖ وَأَحْسِن كَمَا أَحْسَنَ اللَّهُ إِلَيْكَ ۖ وَلَا تَبْغِ الْفَسَادَ فِي الْأَرْضِ ۖ إِنَّ اللَّهَ لَا يُحِبُّ الْمُفْسِدِينَ   القصص:77

[Na utafute, kwa aliyo kupa Mwenyezi Mungu, makaazi ya Akhera. Wala usisahau fungu lako la dunia. Nawe fanya wema kama Mwenyezi Mungu alivyo kufanyia wema wewe. Wala usitafute kufanya ufisadi katika ardhi. Hakika Mwenyezi Mungu hawapendi mafisadi.]   [Al-Qaswas:77]

Ukati na kati wa Ahlu Sunnah wal Jamaah katika Itikadi na Kufuata Twaa
Amesema Allah Subhaanahu wa Taala:

يَا أَهْلَ الْكِتَابِ لَا تَغْلُوا فِي دِينِكُمْ وَلَا تَقُولُوا عَلَى اللَّهِ إِلَّا الْحَقَّ ۚ إِنَّمَا الْمَسِيحُ عِيسَى ابْنُ مَرْيَمَ رَسُولُ اللَّهِ وَكَلِمَتُهُ أَلْقَاهَا إِلَىٰ مَرْيَمَ وَرُوحٌ مِّنْهُ ۖ فَآمِنُوا بِاللَّهِ وَرُسُلِهِ ۖ وَلَا تَقُولُوا ثَلَاثَةٌ ۚ انتَهُوا خَيْرًا لَّكُمْ ۚ إِنَّمَا اللَّهُ إِلَٰهٌ وَاحِدٌ ۖ سُبْحَانَهُ أَن يَكُونَ لَهُ وَلَدٌ ۘ لَّهُ مَا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ ۗ وَكَفَىٰ بِاللَّهِ وَكِيلًا     النساء:171

[Enyi Watu wa Kitabu! Msipite kiasi katika dini yenu, wala msimseme Mwenyezi Mungu ila kwa lilio kweli. Hakika Masihi Isa mwana wa Maryamu ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, na neno lake tu alilo mpelekea Maryamu, na ni roho iliyo toka kwake. Basi Muaminini Mwenyezi Mungu na Mitume wake. Wala msiseme: Utatu. Komeni! Itakuwa kheri kwenu. Hakika Mwenyezi Mungu ni Mungu mmoja tu. Ametukuka Yeye na kuwa na mwana. Ni vyake Yeye vyote viliomo katika mbingu na katika ardhi. Na Mwenyezi Mungu ni Mtegemewa wa kutosha]    [Al-Nnisaa:171]

Kutoka kwa Anas Ibn Malik Radhi za Allah ziwe juu yake. alisema: “Walikuja watu watatu mpaka kwa nyumba za wakeze Mtume wakauliza namna ya ibada za Bwana Mtume ﷺ. Walipoambiwa walisema sisi tuko wapi na Mtume na yeye amekwisha samehewa madhambi yake yaliyotangulia na yatakayo kuja. Akasema mmoja wao ama mimi nitaswali usiku siku zote. Na mwingine akasema mimi nitafunga siku zote na na sitoacha kufunga na akasema mwingine na mimi nitajiepusha na wanawake sitooa kabisa. Mtume akawajia akawambia:

أَنْتُمْ الَّذِينَ قُلْتُمْ كَذَا وَكَذَا !! أَمَا وَاللَّهِ إِنِّي لَأَخْشَاكُمْ لِلَّهِ وَأَتْقَاكُمْ لَهُ ، لَكِنِّي أَصُومُ وَأُفْطِرُ ، وَأُصَلِّي وَأَرْقُدُ ، وَأَتَزَوَّجُ النِّسَاءَ ، فَمَنْ رَغِبَ عَنْ سُنَّتِي فَلَيْسَ مِنِّي

[Nyinyi ndio mliosema kadha wa kadha naapa kwa Allah mimi ni mnyenyekevu mno kwa Allah kuliko nyinyi na mimi numuogopa Allah kuliko nyinyi lakini nafunga na siku nyingine sifungi na naswali usiku na siku nyingine nalala na mimi huoa wanawake basi mwenye kuacha mwenendo wangu si miongoni mwa watu wangu].    [Imepokelewa na Bukhari na Muslim]

MANENO YA WANAVYONI KUTHIBITISHA UKATI NA KATI WA AHLU SUNNA

Amesema ibn Jarir At-Twabary Mungu Amrehemu kwamba Allah Subhaanahu wa Taala Amewasifu Umma huu ya kwamba wao ni watu wakati na kati, kwa ajili ya ukati na kati wao katika dini hawakupita mpaka katika dini. Kama walivyofanya wakristo ambao wamepita mipaka katika (tarhib) na wakasema kuhusu nabi issa ambaye nabii issa hakuyasema wala wao si watu (watakasirika) na kama (taksira) ya mayahudi ambao wamebadilisha kitabu cha Allah na wameuwa Mitume yao na wakamsingizia uongo mola wao (Waislamu) ni watu wa kati na kati na wamelingana katika hilo, wakasifu Allah kwa hilo, likawa jambo linalo pendeza zaidi kwa Allah ni lililo kati na kati.
Na Amesema Imam Shatwiby.Mungu Amrehemu ‘Ukiangalia katika kitendo cha sheria na ukazingatia utapata ndani yake kuna ukati na kati, na ukipata umelemea sehemu katika sehemu zake hilo ni kutoka na kukabiliana na ile hali ilivyo au ni kutokea katika sehemu nyingine. Sehemu (upande) uliomgumu sana ni kwa kulihofisha na kuhimiza na kukataza. Na upande au sehemu yenye ukhafifu sana inakuwa katika kutoa ruhusa na kuhimiza inakuwa mara nyingi ni uzito kulifanya jambo kuwa gumu, isipokuwa hivi au vile utaona Na upande wa usawa uko wazi nao ni msingi ambao wenye kurejelewa na mwenye akili ni yule ambaye atauelekea”.

KWA FAIDA ZAIDI SIKILA MADA HII NA AHMAD M.MUSALLAM

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.