0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SASA NIMEFAHAMU!! (1)- Sheikh Yusuf Abdi

SASA NIMEFAHAMU!!

Wengi huniuliza (SASA NIMEFAHAMU!!) umefahamu nini ?? Na wamanisha nini? na wapo walio tafsiri wanavyo taka wao walivyo dhania bila kuniuliza nilicho kikusudia.
Kwa wanao taka kujua nilicho kikusudia katika msamiati huu (SASA NIMEFAHAMU) nawambia hivi:
Nimefahamu mengi nilio kua siyajui na ata niliokua nayajua, tena SASA wala sio leo kumanisha ni jambo ninalo endelea nalo paka mwisho wa maisha yangu, sababu inawezekana nilio wambia kua nimefahamu ikawa bado sijafahamu lakini sina khofu kwakua nasoma nafanya utafiti nafikiria nauliza na mwanadamu heshi kusoma hivyo basi daima anatakiwa kufahamu kila anacho kisoma, na hapo nitakapo fahamu lolote lile wakati huo pia nitawambia yakua SASA NIMEFAHAMU, kufahamu ndilo lengo kuu kwa tunayo soma na kujifunza, na ndipo nikaufanya msemo hu SASA NIMEFAHAMU kua ni project yangu katika kuleta mabadiliko ya kifikra katika jamii na kusahihisha baadhi ya mambo yanao hitajia kusahihishwa na kufahamika katika imani, ibada, akhlaq, matangamano, Dunia na mengineo. Na nimeandaa programmes tofauti chini ya msamiati huu,
Kufahamu ndilo lengo kuu la yoyote anae taka kujua, na mjuzi alie fahamu, Hawi sawa na asie fahamu, japo wote wamesoma sababu wa kwanza kafikia lengo, na wapili hakufikia.

Mwenyezi Mungu s.w  ameiteremsha hii Qur’ani ili watu waizingatie Aya zake na wapate kuwaidhika wenye akili kama alivyo sema:

{كِتَابٌ أَنزَلْنَاهُ إِلَيْكَ مُبَارَكٌ لِّيَدَّبَّرُوا آيَاتِهِ وَلِيَتَذَكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ}    ص:29

[Na hiki Kitabu, tumekuteremshia wewe, kimebarikiwa, ili wazizingatie Aya zake, na wawaidhike wenye akili.]       [Swaad:29]

Na Mwenyezi Mungu ameashira katika aya nyingi kuhusu jambo hili lakufiri na kutafakari Aya za Qur’ani, ama Visa vilivyo simuliwa ndani ya Qur’ani, mfano wa aya hizi:

{فَاقْصُصِ الْقَصَصَ لَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ}  الأعراف:176

[Basi simulia hadithi, huenda wakatafakari.]     [Al-A’araaf:176]

{كَذَٰلِكَ نُفَصِّلُ الْآيَاتِ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ}    يونس:24

[Namna hivi tunazipambanua Ishara zetu kwa watu wanao fikiri.]    [Yunus:24]

{إِنَّ فِي ذَٰلِكَ لَآيَاتٍ لِقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ}  الرعد:3

[Hakika katika haya zimo Ishara kwa watu wanao fikiri.]    [Ar raa’d:3]

{وَأَنْزَلْنَا إِلَيْكَ الذِّكْرَ لِتُبَيِّنَ لِلنَّاسِ مَا نُزِّلَ إِلَيْهِمْ وَلَعَلَّهُمْ يَتَفَكَّرُونَ}  النحل:44

[Nasi tumekuteremshia wewe Ukumbusho ili uwabainishie watu yaliyo teremshwa kwao, wapate kufikiri.]     [An Nah’l:44]

Hizi ni baadhi za aya zilizo kuja katika kutuhimiza kufikiri,na Aya zilizokuja kinamna hii ni Aya nyingi.

Inatakiwa mwenye kuisoma Qur’ani awe ni mwenye kuzingatia na kutafakari aya zake wala sio kusoma tu bila ya kuzigatia japo kuwa ni mwenye kupata thawabu.

Hii Qur’ani yataka izingatiwe na wenye akili busara na wenye kufikiria, kumanisha wasio tumia akili zao hawataeza kufahamu, hatimae hawezi kua na uwamuzi wowote zaidi ya kufwata yalio fahamika na wengine bila kujali hali au zama au mazingira ya hao walio fahamu wakati huo,kwa namna nyengine twaeza sema wasio fahamu hawaezi jitahidi wakapata hukumu inayo endana na zama wanazo ishi, sababu wamezoea kuiga kusema yalio Semwa na kufwata yalio fwatwa bila kuzingatia zama wanazo ishi. Huo ni upeo wa kufungika Akili na watu aina hiyo mara nyingi hudhuru jamii kuliko kunufaisha ata iwapo wanashiriwa kua wamesoma lakini hawakufahamu.

Asema Mtume ﷺ:

[مَنْ يُرِدِ اللَّهُ بِهِ خَيْرًا يُفَقِّهْهُ فِي الدِّينِ]   رواه البخاري ومسلم

[Mwenyezi Mungu s.w anapo mtakia mja kheri humpa ufahamu wa dini.]   [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Tuna haja sana leo kueza kufahamu Uislamu wetu kama mfumo kamili wa Maisha yetu katika nyaja zote ndipo tue mfano duniani kama watu wenye Katiba ilio kamilika Mzuri inayo muitikia Mwanadamu juu ya mahitajio yote bila yakua ni yenye kumnyima baadhi yanaoendana na maumbile, endapo tutafahamu UISLAMU wetu ipasavyo hapo tutaweza kuongoza Ulimwengu nakua mfano bora zaidi sababu ndio Mfumo wa Mwenyeezimungu (s.w) wa haki.

{إِنَّ الدِّينَ عِندَ اللَّهِ الْإِسْلَامُ}    آل عمران:19

[Bila ya shaka Dini mbele ya Mwenyezi Mungu ni Uislamu.]     [Al-Imraan:19]

Sasa nimefahamu.

Imeandikwa na Sheikh Yusuf Abdi

Mombasa-Kenya

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.