0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SWALA ZA FARADHI

SOMO LA FIQHI

Swala za fardhi ambazo Muislamu amefaradhiwa na Mola wake kuziswali kila siku, mchana na usiku ni swala tano.

Kila moja miongoni mwa swala tano hizi ina wakati wake maalum ambao muislamu anawajibikiwa kuiswali ndani ya wakati huo.

1.  ALFAJIRI.
2. ADHUHURI.
3. AL-ASIRI.
4. MAGHRIBI.
5. ISHAA.

Na dalili ya uwajibu wa kuswali mara tano kwa siku zimekuja aya kadha zikishiria nyakati hizi miongoni mwa aya hizo ni neno lake Mwenyezi Mungu aliyetukuka:

{فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ وَحِينَ تُصْبِحُونَ  وَلَهُ الْحَمْدُ فِي السَّمَاوَاتِ وَالْأَرْضِ وَعَشِيًّا وَحِينَ تُظْهِرُونَ}     الروم:18

[Basi Subhanallah! Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni na asubuhi,Na sifa zote njema ni zake katika mbingu na ardhi, na alasiri na adhuhuri.]    [Al-Rruum:18]

رَوَى لَيْثٌ عَنْ الْحَكَمِ عَنْ أَبِي عِيَاضٍ قَالَ : قَالَ ابْنُ عَبَّاسٍ : ” جَمَعَتْ هَذِهِ الآيَةُ مَوَاقِيتَ الصَّلاةِ : { فَسُبْحَانَ اللَّهِ حِينَ تُمْسُونَ } الْمَغْرِبَ وَالْعِشَاءَ { وَحِينَ تُصْبِحُونَ } الْفَجْرَ { وَعَشِيًّا } الْعَصْرَ { وَحِينَ تُظْهِرُونَ } الظُّهْرَ

Amepokea Al-layth kutoka kwa Al-Hakam kutoka kwa Abuu Iyaadh Amesema: Asema Ibnu Abbas: aya hii imekusanya nyakati za Swala zote “Mtakaseni Mwenyezi Mungu jioni” Maghribi na Ishaa “Mtakaseni Mwenyezi Mungu asubuhi,” Al-fajiri “Wa’ashian” Alasiri “Wahiina Tudh’hiruun” Adhuhuri.

Na neno lake Mwenyezi Mungu:

{أَقِمِ الصَّلَاةَ لِدُلُوكِ الشَّمْسِ إِلَىٰ غَسَقِ اللَّيْلِ وَقُرْآنَ الْفَجْرِ ۖ إِنَّ قُرْآنَ الْفَجْرِ كَانَ مَشْهُودًا}    الإسراء:7

[Shika Sala jua linapo pinduka mpaka giza la usiku, na Qur’ani ya al fajiri. Hakika Qur’ani ya alfajiri inashuhudiwa daima]         [Al-Israai:78]

Jua linapo pinduka ni Swala ya Adhuhuri na Alasiri, “mpaka giza la usiku” ni Swala ya Maghribi na Swala ya Ishaa “na Qur’ani ya Al-fajiri” ni Swala ya Al-fajri, kama ilivyo pokelewa na Ibnu Abbas na wengine katika Salaf Mungu awarehemu.

NA KATIKA SUNNA

عَنِ ابْنِ عَبَّاسٍ رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُمَا ، ” أَنَّ النَّبِيَّ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَسَلَّمَ بَعَثَ مُعَاذًا رَضِيَ اللَّهُ عَنْهُ إِلَى الْيَمَنِ  فَقَالَ : ادْعُهُمْ إِلَى شَهَادَةِ أَنْ لَا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ  وَأَنِّي رَسُولُ اللَّهِ ، فَإِنْ هُمْ أَطَاعُوا لِذَلِكَ فَأَعْلِمْهُمْ أَنَّ اللَّهَ قَدِ افْتَرَضَ عَلَيْهِمْ خَمْسَ صَلَوَاتٍ فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ     رواه البخاري ومسلم

Imepokelewa na Ibn Abbaas – Allah awaridhie kwamba Mtume ﷺ alimtuma Mua’adh – Allah amridhie – kwenda katika nchi ya Yemen (kulingania dini) akamwamiba:

[Walinganie (Waite) kutamka shahada kwamba hapana afaaye kuabudiwa kwa haki ila Allah na kwamba mimi Muhammad ni Mjumbe wa Allah, ikiwa wao watalitii hilo (watalikubali) basi wafahamishe kwamba Allah amefaradhisha juu yao swala tano mchana na usiku………]      [Bukhaariy na Muslim.]

Kauli yake Bwana Mtume – Rehema na Amani zimshukie – alipomwambia yule mkazi wa majangwani ambaye alimuliza swala zilizo faridhi juu yake.

فَقَالَ رَسُولُ اللَّهِ صَلَّى اللَّهُ عَلَيْهِ وَعَلَى آلِهِ وَسَلَّمَ : ” خَمْسُ صَلَوَاتٍ فِي الْيَوْمِ وَاللَّيْلَةِ ” ، قَالَ : هَلْ عَلَيَّ غَيْرُهُنَّ ؟ ، قَالَ : ” لا ، إِلا أَنْ تَطَّوَّعَ      رواه البخاري ومسلم

Akasema Mtume ﷺ :  [Swala tano kila mchana na usiku]  Yule mkazi wa majangwani akamuuliza (tena). Je, ninalazimika na swala nyingine zisizo hizo (tano) (Mtume) akamjibu [Hapana ila swala za suna]        [Imepokewa na Bukhaary na Muslim.]

Na neno lake Mtume ﷺ:

[فَرَضَ اللَّهُ عَلَى أُمَّتِي لَيْلَةَ الْإِسْرَاءِ خَمْسِينَ صَلَاةً، فَلَمْ أَزَلْ أُرَاجِعُهُ وَأَسْأَلُهُ التَّخْفِيفَ حَتَّى جَعَلَهَا خَمْسًا فِي كُلِّ يَوْمٍ وَلَيْلَةٍ]      رواه مسلم

[Amefaridhisha Mwenyezi Mungu Mtukufu juu ya umati wangu Lailati Israai, Swala khamsini, sikuwacha kumrejelea (Mwenyezi Mungu Mtukufu) na kumuomba kupunguziwa mpaka Akazijaalia tano kwa kila siku – mchana na usiku]       [Imepokelewa na Muslim]


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.