0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SUNNA ZA KUTAYAMAMU

SOMO LA FIQHI

Kumesuniwa katika kutayamamu mambo kadhaa, miongoni mwa mambo hayo ni haya yafuatayo :-

1. Kunasuniwa katika tayamamu yale yote ambayo ni suna katika udhu. Kuanzia na :

a. Kupiga “Bismillah” mwanzo wa kutayamamu

b. Kuanza kupangusa mkono wa kulia.

c. Kuomba dua baada ya kutayamamu.

2. Kupiga Ardhi kwa mara ya Pili.

عن عمار بن ياسر أنهم حين تيمموا مع رسول الله صلى الله عليه وسلم فأمر المسلمين فضربوا بأكفهم التراب ولم يقبضوا من التراب شيئا ، فمسحوا بوجوههم مسحة واحدة ، ثم عادوا فضربوا بأكفهم الصعيد مرة أخرى ، فمسحوا بأيديهم

Imepokelewa hadithi na Ammaar Ibn Yaasir Radhi za Allah ziwe juu yake [Kwamba wao walitayamamu wakiwa pamoja na Mtume wa Mwenyezi Mungu  akawamrisha Waislamu Wakapiga viganja vyao mchangani, wala hawakuchukua mchanga wowote kisha wakapangusa nyuso zao mara moja.Halafu wakarudia tena kupiga viganja vyao mchangani mara nyingine, wakapangusa mikono yao.]   [Imepokewa na Abuu Daawud na Ibnu Maajah]

3. Kutapanya vidole wakati wa kupiga viganja juu ya mchanga na kueneza uso kwa pigo moja tu la mchanga na kuieneza mikono kwa pigo jingine.

4. Kupunguza vumbi kwa kupuliza viganja baada ya kupiga.

Suna hii inapatikana katika hadithi iliyopokelewa na Swahaba Ammar Ibn Yaasir Radhi za Allah ziwe juu yake kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu ﷺ alimwambia

[إِنَّمَا كَانَ يَكْفِيكَ أَنْ تَقُولَ بِيَدَيْكَ هَكَذَا ، ثُمَّ ضَرَبَ بِيَدَيْهِ الأَرْضَ ضَرْبَةً وَاحِدَةً ، ثُمَّ مَسَحَ الشِّمَالَ عَلَى الْيَمِينِ وَظَاهِرَ كَفَّيْهِ وَوَجْهَهُ]

[Hakika si vinginevyo inakutosha kufanya hivi”. Akapiga (Mtume) viganja vyake juu ya ardhi pigo moja kisha akapangusa Mkono wa kushoto Mkono wa kulia na kwa akapangusa kwa (viganja hivyo) Uso wake]

Na katika riwaya nyingine ya Bukhari:

وفي رواية للبخاري : [ ونفخ فيهما]

[Na akapulizia ndani yake (viganja)]   halafu akapangusa kwa (viganja) hivyo.


Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.