0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SHIRKI KUBWA


Shirki kubwa ni kuamini kwamba mtu au kitu kama vile: Jiwe, mti, nyota, jua, mwezi, mtume, jini, mtu mtakatifu (Saint) au malaika wana uwezo unaofanana na Mwenyezi Mungu kama vile kuruzuku, kutibu, au kulinda na kwamba kinastahiki kuadhimishwa na kuombwa na kuabudiwa.

Au ni kumfanyia Mwenyezi Mungu visawazishi katika Uungu wake au ibada yake au majina yake na sifa zake nzuri.

HUKMU YAKE 

Shirki kubwa ndilo dhambi kubwa sana, humtoa mtu katika Wisilamu na damu yake huwa halali kuichukua pamoja na mali yake. Amesema Mtume :

 أمرت أن أقاتل الناس حتى يشهدوا أن لا إله إلا الله وأن محمد رسول الله، ويقيموا الصلاة، ويؤتوا الزكاة؛ فإذا فعلوا ذلك عصموا مني دماءهم إلا بحق الإسلام، وحسابهم على الله

[Nimeamrishwa kuwa niwapige vita watu mpaka washuhudie kwamba hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki illa Mwenyezi Mungu na kwamba Mohammad ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu….]

Ni dhambiambayo Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta´ala) haisamehi. Amesema Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta´ala):

[ إِنَّ اللَّهَ لا يَغْفِرُ أَنْ يُشْرَكَ بِهِ وَيَغْفِرُ مَا دُونَ ذَلِكَ لِمَنْ يَشَاءُ وَمَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ افْتَرَى إِثْمًا عَظِيمًا]    [النساء 48]

[Hakika Mwenyezi Mungu hasamehi kushirikishwa; na husamehe yasiyokuwa haya kwa amtakae. Na anaemshirikisha Mwenyezi Mungu bila shaka amebuni dhambi kubwa (kabisa).]    [Suratun-Nisaa ya 48]

Luqmaan alijaaliwa na Mwenyezi Mungu Mtukufu kuwa na hekima sana, naye aliifananisha SHIRKI kuwa sawa na DHULMA KUBWA. Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Subhanau Wata’ala kwa kauli ya Luqmaan:

    [ لقمان : 13]  [إِنَّ الشِّرْكَ لَظُلْمٌ عَظِيمٌ] 

[Hakika shirki ni dhulma kubwa.]

Pia shirki humsababishia mja kuharamishiwa Pepo kwa uthibitisho wa Qurani tukufu. Mwenyezi Mungu (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

  [المائدة : 72]  [ إِنَّهُ مَنْ يُشْرِكْ بِاللَّهِ فَقَدْ حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ وَمَأْوَاهُ النَّارُ]      

[Kwani anaemshirikisha Mwenyezi Mungu, hakika Mwenyezi Mungu atamharamishia Pepo, na mahali pake (patakuwa) ni Motoni.]    [Al Maaida:72]


SIKILIZA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB




Begin typing your search above and press return to search.