0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

AINA ZA SHIRK

Aina za shirki
Shirki ina aina mbili: kubwa na ndogo. Na tofauti baina yazo ni kama ifwatavyo:
1. Shirki kubwa ni ukafiri, nayo shirki ndogo si ukafiri lakini ndilo kosa kubwa baada ya shirki kubwa.
2. Shirki kubwa humtoa mtu katika Wisilamu nayo shirki ndogo haitoi lakini hupunguza tauhidi yake.
3. Shirki kubwa huharibu vitendo vyema vya mtu vyote, nayo shirki ndogo haiharibu illa kile kitendo ambacho hii shirki imeingia pekee.
4. Ikiwa mwenye shirki kubwa atakufa bila kutubia, basi yeye ataishi milele motoni, naye atakayekufa na shirki ndogo ataingia motoni lakini hatadumu humo milele.
5. Shirki kubwa huhalalisha kuuawa mtu, au kuchukua mali yake au familia yake, nayo ndogo sio hivyo.
6. Mwenye shirki kubwa hasamehewi ikiwa atakufa bila kutubu, naye mwenye shirki ndongo hupimwa mambo yake, ikiwa kutapatikana mambo mema ambayo yanashinda hilo kosa la shirki ndogo, basi ataingizwa peponi na illa ataingia motoni lakini hatadumu humo milele.(1)


(1) Chanzo: Tauhidi. Daktari Hajj Makokha Maulid


Begin typing your search above and press return to search.