0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

SHIRKI NDOGO


 MAANA YA SHIRKI NDOGO

Shirki ndogo ni kila ambacho kimetajwa katika sheria kuwa ni shirki lakini hakimtoi mja katika wisilamu

HUKMU YAKE NA BAADHI YA MAMBO YANAYOIHUSU 

1. Shirki ndogo ndio asi kubwa sana baada ya shirki kubwa
2. Shirki ndogo haiharibu tauhidi lakini huipunguza isiwe kamili
3. Shirki ndogo haiharibu matendo yote ya mja lakini inaharibu lile tendo ambalo limeambatana nalo.
4. Mtu akifa akafanya shirki ndogo, hufa akiwa mwisilamu naye yuko chini ya amri yake Mwenyezi Mungu, akitaka atamsamehea, na akitaka atamwadhibu
5. Mwenye shirki ndogo ikiingia motoni hadumu humo milele bali atatolewa na kuingizwa peponi.

Amesema Mwenyezi Mungu s.w kuhusu shirki ndogo:

[ فَمَنْ كَانَ يَرْجُوا لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا}   [الكهف: 110}

[Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.]     [Suratul Kahf:110]

Naye Mtume amesema:

 وقوله صلى الله عليه وسلم: “يقول الله تعالى: أنا أغنى الشركاء عن الشرك، من عمل عملا أشرك معي فيه غيري تركته وشركه}    رواه مسلم

[Amesema Mwenyezi Mungu aliyetukuka: Mimi ndimi niliyejitosheleza na kuwa na mshirika, basi atakaefanya jambo akanishirikisha kwalo Mimi na asiyekuwa Mimi, nitamwacha na alichoshirikisha]     [Imepokewa na Musalim]

AINA ZA SHIRKI NDOGO 

Ya kwanza: Riyaa:
Nayo ni kufanya ibada (jambo jema) ili kuwaonyesha watu, au ili kujionyesha mbele ya watu ili wakusifu. Mfano wa mtu anaswali swala lakini anafanya hivyo ili watu wamwone na wamtukuze na wamsifu.

Hukumu yake
Ni jambo la haramu kama alivyosema Mwenyezi Mungu:

[ فَمَنْ كَانَ يَرْجُوا لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا}     [الكهف: 110}

[Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.]
Naye mtume amesema :

ألا أخبركم بما هو أخوف عليكم عندي من المسيح الدجال”؟ قالوا: بلى يا رسول الله. قال: “الشرك الخفي، يقوم الرجل فيصلي، فيزين صلاته لما يرى من نظر رجل      أخرجه إبن ماجة وحسنه الألباني

[Je, nisiwambieni kuhusu lenye kuniogopesha zaidi kuwahusu nyinyi kuliko Masihi Dajali? Wakasema kwa nini ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu Mtume akasema shirki iliyofichika na mtu asimame kuswali kisha akaipamba swala yake atakapojua kuwa kuna mtu amatizama]     [Imepokewa na Ibnu Maajah na kuhasinswa na Al Baaniy]

وقوله صلى الله عليه وسلم: إن أخوف ما أخاف عليكم: الشرك الأصغر؛ الرياء؛ يقول الله يوم القيامة إذا جزى الناس بأعمالهم: اذهبوا إلى الذين كنتم تراءون في الدنيا، فانظروا هل تجدون عندهم جزاء       أخرجه الإمام احمد في مسنده

[Hakika chenye kuniogopesha zaidi juu yenu (ni):shirki ndogo; riyaa;Atasema Mwenyezi Mungu siku ya kiyama atakapolita watu kwa matendo yao: Nendeni kwa wale mliokuwa mkiwaonyesha (matendo yenu) duniani, basi mwangalieni je, mnapata kwao malipo]   [Imepokewa na Imamu Ahmad katika Musnadi yake]

Na kauli yake Mtume :

وقوله صلى الله عليه وسلم:  من صلى يرائي فقد أشرك، ومن تصدق يرائي فقد أشرك ومن صام يرائي فقد أشرك    أخرجه الأمام أحمد في المسند

[Atakayeswali ili kuonyesha, basi atakuwa ameshirikisha,na atakayefunga ili kuonyesha, basi atakuwa ameshirikisha].  [Imepokewa na Imamu Ahmad katika Musnad yake]

Ya Pili: Asum`a
Nayo ni kufanya jambo jema kisiri kisha kuja na kulitaja mbele ya watu ili wasikie kuhusu hilo jambo ulilolitenda. Mfano wa mtu anayeswali usiku kisha mchana anakuja na kuanza kuelezea watu vile yeye ni mswali usiku.

Na tofauti baina ya riyaa na sum`a ni kuwa riyaa huwa ni kwa ajili watu waone nayo sum`a huwa ni kwa ajili watu wasikie.
Hukumu yake
Ni jambo la haramu ambalo huharibu kitendo kilichoambatana nayo:

[ فَمَنْ كَانَ يَرْجُوا لِقَاءَ رَبِّهِ فَلْيَعْمَلْ عَمَلًا صَالِحًا وَلا يُشْرِكْ بِعِبَادَةِ رَبِّهِ أَحَدًا}   [الكهف: 110}

[Mwenye kutaraji kukutana na Mola wake Mlezi basi naatende vitendo vyema, wala asimshirikishe yeyote katika ibada ya Mola wake Mlezi.]

Riyaa na sum`a kubadilika kuwa shirki kubwa
Hubadilika riyaa na sum`a zikawa shirki kubwa kwa njia hizi:
1. Kujionyesha katika asili ya imani ili kuepuka madhara au kupata faida fulani.
2. Ikiwa riyaa itaingia kwa mengi ya matendo yake
3. Ikiwa atakusudia katika matendo yake hadhi au faida ya dunia pekee na wala hataki malipo ya Mwenyezi Mungu

Ya Tatu: Shirki ndogo katika irada (kutaka, kukusudia)
Nayo ni kwamba afanye mja mambo mema ambayo ni mambo ya ibada kwa kumkusudia Mwenyezi Mungu lakini pamoja na niya hii ana niya ya kupata hadhi(faida,cheo) ya duniani. Mafano mtu apigane jihadi kwa ajili ya Allah lakini pamoja na kutaka kumridhisha Allah ana niya ya kuwa kiongozi wa hicho kikundi cha jihadi. Au kutafuta elimu ya kisheria ili apate mali au apewe kazi fulani. Au kwenda kuswali msikitini ili apate cheo hapo msikitini n.k.
Nacho ni kitendo cha haramu. Amesema Mwenyzi Mungu (Subhaanahu wa Ta´ala):

 مَنْ كَانَ يُرِيدُ الْحَيَاةَ الدُّنْيَا وَزِينَتَهَا نُوَفِّ إِلَيْهِمْ أَعْمَالَهُمْ فِيهَا وَهُمْ فِيهَا لا يُبْخَسُونَ، أُولَئِكَ الَّذِينَ لَيْسَ لَهُمْ فِي الْآخِرَةِ إِلَّا النَّارُ وَحَبِطَ مَا صَنَعُوا فِيهَا وَبَاطِلٌ مَا كَانُوا يَعْمَلُونَ   هود: 15-16

[Wanao taka maisha ya dunia na pumbao lake tutawalipa humo vitendo vyao kamili. Na wao humo hawatopunjwa. Hao ndio ambao hawatakuwa na kitu Akhera ila Moto, na yataharibika waliyo yafanya, na yatapotea bure waliyo kuwa wakiyatenda.]     [Huud:15-16]

Naye mtume s.a.w amesema katika hadithi ya Abu Hureira radhi za Allah ziwe juu yake:

عن أبي هريرة رضي الله عنه أن رجلا قال:  يا رسول الله! رجل يريد الجهاد، وهو يبتغي عرضا من أعراض الدنيا؟ فقال رسول الله صلى الله عليه وسلم: “لا أجر له”. فأعاد عليه ثلاثا، والنبي صلى الله عليه وسلم يقول: “لا أجر له      أخرجه أحمد في مسنده

Kupitia kwa njia ya Abu Hauraira(Radhia Allahu anhu)amesema: [Mtu alisema: Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu: mtu anataka (kupigana)jihadi naye anataka hadhi katika hadhi za dunia? Basi akasema mtume wa Mwenyezi Mungu:”Hana ujira wowote”. Na akarudia mara tatu, naye mtume anamwambia “Hana ujiwa wowote”]      [Imepokewa na Imam Ahmad katika Musnadi yake]

Ya Nne: Kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu
Nayo hii shirki ni kuapa kwa kutaja jina la asiyekuwa Mwenyezi Mungu, kama wanavyoapa baadhi ya watu kwa kuapa na Alkaaba,au mzee wa kijiji, au mnyama anyeenziwa kwa kabila lao n.k

Hukumu yake
Ni haramu kuapa na asiyekuwa Mwenyezi Mungu kwani ni shirki. Amesema Mtume :

 ألا إن الله ينهاكم أن تحلفوا بآبائكم، من كان حالفا فليحلف بالله أو ليصمت ]    رواه البخاري]

[Hakika Mwenyezi Mungu anawakataza kuapa na baba zenu, atakayetaka kuapa, basi aape kwa Mwenyezi Mungu au anyamaze.]  [Imepokewa na Bukhari]

جاء رجل إلى عبد الله بن عمر – رضي الله عنهما-، فقال:  احلف بالكعبة؛ فقال:أحلف برب الكعبة، فإن عمر كان يحلف بأبيه، فقال له النبي صلى الله عليه وسلم: “لا تحلف بأبيك، فإنه من حلف بغير الله فقد أشرك        اخرجه الإمام أحمد وأبوداود

Alimjia mtu Ibn Umar (Radhia Allahu anhum)kisha akasema: Je, niape kwa Al-Kaaba? Kisha akasema Ibn Umar: Apa kwa Mola Mlezi wa Al-Kaaba, kwa hakika Umar alikuwa akiapa kwa baba yake, basi mtume akamwambia: “Usiape kwa baba yako, kwa hakika atakayeapa kwa asiye Mwenyezi Mungu basi atakuwa ameshirikisha”]     [Imepokewa na Imam Ahmad na Abuu Daud]

Amesema Ibn Mas`ud radhi za Allah ziwe juu yake:

لأن أحلف بالله كاذبا، أحب إلي من أن أحلف بغيره صادقا]    أخرجه عبدالرزاق الصنعاني]

[Kuapa kwa Mwenyezi Mungu huku nikiwa muongo ni bora zaidi kwangu kuliko niape kwa asiye Mwenyezi Mungu huku nikiwa mkeli.]

Faida:
Kwa nini Ibn Mas`ud kapendelea kuapa kwa Allah kwa kitu cha uongo kuliko kuapa kwa asiye Allah huku akiwa mkweli?
Kuapa hakufai illa kwa jina la Mwenyezi Mungu au Sifa zake, si kwa jina la chochote kile. Na pia haifai kuapa kwa Mwenyezi Mungu huku ukijua kuwa unachoapa juu yake ni uongo. Lakini Ibn Mas`ud alichagua kuapa kwa jina la Mwenyezi Mungu huku kwa kitu cha uongo kwa sababu kuapa kwa Allah huku akiwa mwongo ni tauhidi kwani kitendo hiki hakimtoi kwa wisilamu. Nayo kuapa kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu akiwa mkweli ni shirki.
Je kiapo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu kinashikisha na kulazimisha kukitimiza?
Kiapo kwa asiyekuwa Mwenyezi Mungu ni haramu na ni shirki ndogo, hakifai kabisa. Na akiwa mtu atafanya hivyo, maulamaa wote wamekubaliana kwamba hicho kiapo hakimlazimu wala hakishikishi.

Ya Tano:Kusema 
Kama hangekuwa Mwenyezi Mungu na wewe basi….)

Nayo ni kusema kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na uwezo wako, huku ukimwambia mtu kuhusu jambo ambalo alikufanyia au kusema lau hangekua Mwenyezi Mungu na wewe, jambo faulani halingefanyika,au aseme sima msaidizi illa Mwenyezi Mungu na wewe.
Hii ni shirki ndogo:

عن ابن عباس -رضي الله عنهما- أن رجلا قال للنبي صلى الله عليه وسلم:  ما شاء وشئت. قال: “أجعلتني لله ندا، بل ما شاء الله وحده    أخرجه الإمام أحمد

[Mtu alimwambia mtume : Kwa kupenda kwa Mwenyezi Mungu na kwa kupenda kwako. Mtume akamwambia: Umenijalia muungu pamoja na Mwenyezi Mungu? Bali, kwa kupenda kwa Mwenyezi Mungu peke yake.]    [Imepokewa na Imamu Ahmad]

قول رسول الله صلى الله عليه وسلم: “إذا حلف أحدكم فلا يقل: ما شاء الله وشئت؛ ولكن ليقل: ما شاء الله ثم شئت     أخرجه إبن ماجة

Amesema mtume [Atakapoapa mmoja wenu, basi asiseme kwa kupenda kwake Mwenyezi Mungu na kwako lakini aseme kwa kupenda kwake Mwenyezi Mungu kisha kwako.]   [Imepokewa na Ibnu Maajah]    (1)


  SIKILIZA SHEREHE YA MADA HII NA SHEIKH SALIM KHATIB



(1) Chanzo: Tauhidi. Daktari Hajj Makokha Maulid


Begin typing your search above and press return to search.