0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

NJAMA ZA MAKURAISHI DHIDI YA MUHAJIRINA WA MWANZO

Makuraishi hawakuweza kuvumilia kuwaona Waislamu wakipata mapumziko yaliyo salama nchini Abyssinia, hivyo waliwatuma wajumbe wawili waaminifu kudai kurejeshwa kwao Makka. Wajumbe hao walikuwa Amr bin Al-‘As na Abdallah bin Al-Rabia, wakati huo walikuwa bado kusilimu.
Walichukua zawadi za thamani kwa ajili ya mfalme na makasisi wake, na walifanikiwa kuungwa mkono na baadhi ya watumishi wa kitala. Wajumbe wa Mushirikina walidai kuwa wakimbizi Waislamu wafukuzwe kutoka Abyssinia kwa sababu walikuwa Wameacha dini ya mababu zao, na kiongozi wao alikuwa akihubiri dini tofauti na yao na tofauti na ile ya mfalme.Mfalme aliwaita Waislamu katika kitala shake na akawataka waeleze mafudisho ya Dini yao. Waislamu waliamua kumweleza kila kitu kwa ukweli mtupu bila kujali matokeo yake. Jaafar bin Abi Talib (r.a) alisimama na kumwambia mfalme maneno yafuatayo:

أيها الملك، كنا قوما أهل جاهلية، نعبد الأصنام ونأكل الميتة، ونأتي الفواحش، ونقطع الأرحام، ونسيء الجوار، ويأكل منا القوي الضعيف، فكنا على ذلك، حتى بعث الله إلينا رسولا منا، نعرف نسبه وصدقه وأمانته وعفافه، فدعانا إلى الله لنوحده ونعبده، ونخلع ما كنا نعبد نحن وآباؤنا من دونه من الحجارة والأوثان، وأمرنا بصدق الحديث، وأداء الأمانة، وصلة الرحم، وحسن الجوار، والكف عن المحارم والدماء، ونهانا عن الفواحش، وقول الزور، وأكل مال اليتيم، وقذف المحصنات، وأمرنا أن نعبد الله وحده، لا نشرك به شيئا، وأمرنا بالصلاة والزكاة والصيام- فعدد عليه أمور الإسلام- فصدقناه، وآمنا به، واتبعناه على ما جاءنا به من دين الله، فعبدنا الله وحده، فلم نشرك به شيئا، وحرمنا ما حرم علينا، وأحللنا ما أحلّ لنا، فعدا علينا قومنا، فعذبونا، وفتنونا عن ديننا، ليردونا إلى عبادة الأوثان من عبادة الله تعالى، وأن نستحل ما كنا نستحل من الخبائث، فلما قهرونا وظلمونا وضيقوا علينا، وحالوا بيننا وبين ديننا، خرجنا إلى بلادك، واخترناك على من سواك، ورغبنا في جوارك، ورجونا ألا نظلم عندك أيها الملك.

“Ewe Mfalme tulikuwa tumezama katika lindi la ujinga na ushenzi, tulikuwa tukiabudu masanamu, tuliishi katika uchafu, tulikula nyamafu, na tulizungumza mambo ya kuchukiza mno, hatukuwa na hisia za kibinadamu, na wajibu wa kuwatendea mema majirani tuliutelekeza; hatukujua sheria, ila mwenye nguvu ndiye alikuwa na haki. Ndipo Allah (s.w.t) Akamtumila mtu miongoni mwetu ambaye kuzaliwa kwake, ukweli wake, uamimfu wake tulikuwa tunaufahamu. Alitulingania kwa Mungu Mmoja na_ akatufunza ‘ tusimshirikishe na kitu chochote. Alitukafaza kuabudu masanamu na alituamuru tuseme ukweli, tuwe waamimfu wa dhamana zetu, tuwe na huruma na tuzijali haki za majimni, jamaa na mamfiki; alitukataza kuzungumza maovu ya wanawake, na kula mali za mayatima; alituamrisha kuyakimbia maovu, na kuacha mambo machafu; kusali, kutoa Zaka na kufunga. Tumemwamini na tumeyakubali mafundisho yake na makatazo yake, tumekubali kumwabudu Allah (s.’w.t), na kutomshirikiasha na kitu chochote na tunafanya yale Aliyoturuhusu kufanya nu tumeyaacha Aliyotukataza.Kutokana na sababu hizo wenzetu wameamua kutupiga vita, wametutesa ili tuache kumwabudu Mwenyezi Mungu (s.w.t) na turejee kuabudu masanamu na mambo yanayochukiza. Wametutesa na kutujeruhi mpaka tukakosa usalama, tumekuja katika nchi yako na tunataraji utatulinda dhidi ya wakandamizaji.”

Mfalme alivutiwa sana na maneno haya na akawataka Waislamu awasomee baadhi ya Yale Yaliyoteremshwa na Allah (ﷺ). Jaafar (r.a) alisoma mwanzo wa Sufatul Maryam (sura ya 19), ndani yake kumeelezwa kisa cha kuzaliwa Yahya (john) ha Issa (a.s). Alisoma mpaka Habari za Mariam alipolishwa chakula kimiujiza. Kwa sababu hii, mfalme pamoja na makasisi wa dola yake, waliemewa na kububujikwa na machozi ambayo yalitiririka mpaka kwenye mashavu na yakalowesha ndevu zake.

Najash alinadi: Inaelekea maneno haya na yale yaliyoteremshiwa kwa Issa (Yesu) ni miale ya mwanga ambayo ilinururishwa kutoka chanzo kimoja.’ Aliwageukia wajumbe wa Kikuraishi waliovunjika moyo na kusema, ”Nasikitika siwezi kuwarejesha wakimbizi hawa. Wako huru kuishi na kuaabudu katika dola yangu kama wapendavyo.”

Siku iliyofuata Wale wajumbe Walikwenda tena kwa mfalme na kumwambia kuwa Muhammad (s.a.w) na Wafuasi wake wanamkashifu Yesu Kristo. Mfalme aliwaita tena Waislam na aliwataka wamweleze wanavyomfahamu Yesu. Jaafar (r.a) alisimarna tena na akatoa majibu: “Tunamwelezea Yesu kama tulivyofundishwa na Mtume Wetu (ﷺ) ni kwamba yeye ni Mtumishi wa Mungu, Mjumbe Wake, Roho Yake na Neno Lake, vilipuliziwa kwa Bikira Maria (Mariam).” Mfalme alisema, “Hate sisi tunaamini hivyo Mbarikiwe nyinyi na Abarikiwe Bwana wenu.”

Kisha akawageukia wajumbe waliokasirika’ na makasisi wake ambao walikuwa wamekasirika, akawaambia: ‘Mnaweza kukasirika lakini mnajisumbua bure, Yesu si chochote zaidi ya vile Jaafar alivyomueleza.’ Kisha akawahakikishia Waislamu ulinzi kamili. Aliwarejeshéa Wajumbe wa Makuraishi zawadi walizomletea na akawataka warudi kwao. Waislamu waliishi Abyssinia bila kusumbuliwa kwa miaka mingi mpaka waliporejea Madina.

Kwa njia hii dhamira mbovu za Makuraishi ziliwarudia Wenyewe na njama zao hazikufanikiwa hata chembe. Walitanabahi kuwa kinyongo walichokuwa nacho dhidi ya Waislam kisingeweza kutekelezwa nje ya himaya yao ya Makka. Walianza kubuni njia mbalimbali za kuzima ulinganiaji wa Dini mpya kupitia njia mbalimbali za ukatili, ikiwemo ya kumwuua Mtume (s.a.w). Dhamira mbaya zilikuwa zikikatizwa na ammi yake, Abi Talib, na msimamo wake wenye nguvu katika jamii aliokuwa akiufurahia Alimuunga rnkono na kumpa ulinzi mpwa wake. Hivyo, walionelea bora wakutane na Abu Talib wazungumze naye

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM 163-166

Begin typing your search above and press return to search.