0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

VITISHO VYO MAKUREISH KWA ABUU TWALIB

AR-RAHEEQ AL-MAKHTUM


Mapagani wa Makka hawakuacha kumrai Abu Talib kwa mara ya pili na wakasisitiza kuwa asitishe harakati za mpwa wake vinginevyo mapambano makali yangetokea. Ujumbe wa-Mabwana wa Makka walikwenda kumwona Abu Twalib na kumwambia, “Ewe Abu Twalib weye ni mtu mzima mwenye kuheshimika na mwenye utukufu mbele yetu. Tulikuonya kuhusu suala la mtoto wa ndugu yako, lakini hukufanya kitu, Wallahi, sisi hatuwezi kusubiri tena kwa yule ambaye anawatukana baba zetu, na kutufanya sisi hatuna akili, na kuwakosea miungu yetu, ila kutangaza vita naye au nanyi wenye kumuunga mkono.

Abu Twalib aliemewa na vitisho hivyo vya wazi na akachelea kuachana na watu wake. Lakini kwa upande mwengine asingeweza kumuacha mkono Mtume (ﷺ) Alimtumia mpwa wake ujumbe kuhusu yale waliyoyaserna Mkuraaishi. Alimwambia Mtume (ﷺ), ”Nihurumie na jihurumie mwenyewe na usinibebeshe mzigo nisiouweza.”

Baada ya kupata ujumbe huo Mtume () alidhani kuwa ammi yake atamwacha na hatomwunga mkono tena hivyo alijibu:

يا عمّ، والله لو وضعوا الشمس في يمينى والقمر في يساري على أن أترك هذا الأمر حتى يظهره الله، أو أهلك فيه ما تركته

Ewe ammi yangu Naapa kwa jina la Mwenyem Mungu, endapo wataliweka jua katika mkono wangu wa kulia na Mwezi katika mkono  wangu wa kushoto kwa sharti la kuacha kulingania Dini, mpaka Allah Atakaponipa ushindi an nife humo, sitoacha abadan.”:

Mtume (ﷺ) alisimama na alipogeuka na kuanza imondoka, ammi yake alimwita na kumwambia, ”Rudi mpwa  wangu,” na aliporejea, alimwambia, “Nenda kahubiri kama utakavyo, Naapa kwa Iina la Mwenyezi Mungu ; sitokutelekeza.” Kisha akasoma mashairi yaliyojaa maana ya kumuunga mkono.

وَاللَهِ لَن يَصِلوا إِلَيكَ بِجَمعِهِم
حَتّى أُوَسَّدَ في التُرابِ دَفينا
فَاِصدَع بِأَمرِكَ ما عَلَيكَ غَضاضَةٌ
وَاِبشِر بِذاكَ وَقَرَّ مِنهُ عُيونا

Wallahi hawataweza kukudhuru pamoja na mkusanyiko wao,  Hadi nitakapofizkiwa ndani ya mwanandani. Tangaza jumbo Iako wala usijali kitu,  Wabashirie na udumu katika msimamo wako


 Arraheeq Al Makhtuum Uk 166-168


Begin typing your search above and press return to search.