June 22, 2021
0 Comments
SOMO LA FIQHI
Nguzo za Umra
1. Kuhirimia:
kwa kauli ya Mtume ﷺ:
[إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى ] رواه البخاري
[Hakika matendo yanazingatiwa kwa nia, na hakika ni kwamba kila mtu atapata lile alilonuilia] [Imepokewa na Bukhari.]
2. Kusai baina ya Swafaa na Marwah:
kwa kauli ya Mtume ﷺ:
[اسْعَوْا؛ فَإِنَّ الله كَتَبَ عَلَيْكُمْ السَّعْيَ] رواه أحمد
[Fanyeni Sai, kwa kuwa Mwenyezi Mungu Amewafaradhia kusai] [Imepokewa na Ahmad.]
3. Alkaaba:
kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
{ وَلۡيَطَّوَّفُواْ بِٱلۡبَيۡتِ ٱلۡعَتِيقِ} الحج: 29}
[Na waitufu Nyumba ya Zamani] [22: 29]