SOMO LA FIQHI
NGUZO ZA HIJA
1. Kuhirimia:
kwa neno la Mtume ﷺ:
[إِنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى .] رواه البخاري
[Hakika matendo mema yategemea nia, na hakika kila mtu atapata lile alilonuilia] [Imepokewa na Bukhari.].
2. Kusai baina ya Swafaa na Marwah:
kwa neno lake ﷺ:
[اسْعَوْا؛ فَإِنَّ الله كَتَبَ عَلَيْكُمْ السَّعْيَ]. [رواه أحمد]
[Fanyeni Sai, kwani Mwenyezi Mungu Amewafaradhia kusai] [Imepokewa na Ahmad.].
3. Kusimama Arafa:
kwa kauli ya Mtume ﷺ:
[الْحَجُّ عَرَفَةُ]. رواه الترمذي
[Hija ni Arafa] [Imepokewa na Tirmidhi.].
4. Twawafu ya Ifaadhah:
kwa neno la Mwenyezi Mungu Aliyetukuka:
[ وَلۡيَطَّوَّفُواْ بِٱلۡبَيۡتِ ٱلۡعَتِيقِ} الحج: 29
[Na ili waitufu Nyumba ya Zamani] [22: 29].
Tanabahisho
Mwenye kuacha nguzo moja miongoni mwa nguzo za Hijja, ikiwa ni kuhirimia basi ibada yake haikubaliki kwa sababu hakutia nia na ibada haikubaliki bila ya nia na ikwa ni nguzo nyingine ya Hijja haitatimia mpaka ailete.