SOMO LA FIQHI
Amesema Mtume ﷺ:
[صَلُّوا كَمَا رَأَيْتُمُونِي أُصَلِّي] متفق عليه
[Swalini kama munavoniona mimi nikiswali] [Imepokewa na Bukhari na Muslim]
Aisha alipokewa kwamba alisema: [Mtume ﷺ alikuwa akifungua Swala kwa Takbiri na kisomo cha “Alhamdu lillaahi Rabbil ‘aalamiin”, na alikuwa akirukuu hakiinamishi kichwa chake na wala hakisimamishi sawa, bali alikikiweka baina ya hali hizo mbili. Na alikuwa akiinua kichwa chake kutoka kwenye rukuu, hasujudu mpaka alingane katika kusimama. Na alikuwa akisoma Atahiyatu katika kila rakaa mbili, na alikuwa akikalia mguu wake wa kushoto na akiusimamisha mguu wake wa kulia. Na alikuwa akikataza mkao wa Shetani (kukaa kama shetani) na alikikataza mtu kuiweka chini mikono yake katika kukaa kama vile mnyama wa kuwinda, na alikuwa akihitimisha Swala yake kwa kupiga Salamu] [Imepokewa na Muslim.]
Kuelekea Kibla na Takbiri ya kufungia Swala
Anayetaka kuswali atasimama hali ya kuelekea Kibla na kujihisi kuwa amesimama mbele ya Mwenyezi Mungu Aliyetukuka, hali ya kuwa ni mnyenyekevu katika kuswali kwake.
Kisha anuilia kuswali moyoni mwake.Na nia pahali pake ni moyoni, na haifai kuitemka nia kwani kufanya hivyo ni uzushi.Amesema Mtume ﷺ:
[إنَّمَا الْأَعْمَالُ بِالنِّيَّاتِ، وَإِنَّمَا لِكُلِّ امْرِئٍ مَا نَوَى] رواه البخاري ومسلم
[Hakika amali zote ni kwa nia na kila mtu hulipwa kwa alilo nuiliya] [Imepokewa na Bukhari na muslim.]
– Kisha ainue mikono yake mkabala wa mabega yake au masikio yake na aseme: ALLAHU AKBAR (Mwenyezi Mungu ni Mkubwa) [Imepokewa na Muslim.].
– Kisha aweke mkono wake wa kulia juu ya wa kushoto kifuani mwake au aushike mkono wa kushoto kwa wa kulia [Imepokewa na Ahmad.].
DUA YA KUFUNGULIA SWALA NA KUSOMA FATIHA
– Mwenye kuswali ainamishe kichwa chake, atazame mahali pa kusujudia, kisha aseme:
[سُبْحَانَكَ اللهُمَّ وَبِحَمْدِكَ، تَبَارَكَ اسْمُكَ، وَتَعَالَى جَدُّكَ، وَلَا إِلَهَ غَيْرُكَ]
SUB’HANAKA ALLAHUMMA WABIHAMDIKA, TABAARAKA IS’MUKA WATA’AALA JADDUKA WALAA ILAAHA GHAY’RUKA
[Kutakasika ni kwako na sifa njema ni zako. Lina baraka jina lako na uko juu utukufu wako, na hakuna mola asiyekuwa Wewe] [Imepokewa na Muslim.]
Kisha aseme baada ya hapo:
[أعوذ بالله من الشيطان الرجيم]
A’UDHU BILLAHI MINA SHEYTWANI RAJIIM
[Najilinda kwa Mwenyezi Mungu kutokana na Shetani aliyefukuzwa kutoka kwenye rehema ya Mwenyezi Mungu]
[بِسْمِ اللَّـهِ الرَّحْمَـٰنِ الرَّحِيمِ]
BIS’MILLAHI ARRAH’MAANI ARRAHIIM
[Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu] kwa siri [Imepokewa na Muslim.]
Baada ya hapo asome Suratul Fatiha [Imepokewa na Bukhari.]
Kisha aseme “Aamiin”, yaani: Ewe Mola! Takabali.
Baada ya kusoma Suratul Fatih, ni Sunna asome Sura au baadhi ya aya za Qur’ani zilizo sahali kwake kuzisoma katika rakaa mbili za mwanzo, na asome kwa sauti katika Swala ya alfajiri na katika rakaa mbili za mwanzo za Magharibi na Isha.
KURUKUU NA KUINUKA KUTOKA KWENYE RUKUU
Baada ya kusoma Suratul Fatiha na Sura nyingine atainua mikono yake na alete takbiri hali ya kuinama kwende kwenye rukuu, aiweke mikono yake juu ya magoti yake, huku amekunjua vidole vyake kama kwamba anayashika magoti, asawazishe mgongo wake na kichwa chake katika hali ya kuinama kisha aseme:
[سبحان ربي العظيم]
SUBHANA RABIYAL ADHIIM
[Kutakasika ni kwa Mola wangu Aliye Mkubwa] (mara tatu ) [Imepokewa na Tirmidhi.]
Kisha ainuke na aseme (awe ni imamu au mwenye kuswali peke yake):
[سمع الله لمن حمده]
SAMI’A LLAHU LIMAN HAMIDAH
[Mwenyezi Mungu Anamsikia yule anayemsifu] [Imepokewa na Tirmidhi.]
Na hapo wote waseme:
[رَبَّنَا لَكَ الْحَمْدُ مِلْءُ السَّمَاوَاتِ وَمِلْءُ الْأَرْضِ وَمِلْءُ مَا شِئْتَ مِنْ شَيْءٍ بَعْدُ]
RABANA WALAKAL HAMDUH MIL’A SAMAAWAAT,WA MIL’ALARDHI WAMIL’A MAASHI’TI MIN SHEYIN BA’ADU
[Mola wetu! Sifa njema zote ni zako, kujaa kwa mbingu na kujaa kwa ardhi na kujaa vilivyoko baina hizo na kujaa kwa vinginvyo baada ya hizo] [Imepokewa na Tirmidhi.].
Na imependekezwa kuweka mikono juu ya kifua kama alivyofanya katika kusimama kabla ya kurukuu.
KUSUJUDU NA KUINUKA KUTOKA KWENYE KUSUJUDU
Atatoa takbiri kisha apomoke hali ya kusujudu, na kitu cha kwanza cha kugusa ardhi kiwe ni magoti yake kisha mikono yake [Imepokewa na Abuu Daud.]
Kisha paja lake la uso na pua yake, Na akunjue vitanga vyake vya mikono juu ya ardhi mkabala wa mashikio yake na mabega yake.
Na avielekeze vidole vyake upande wa kibla na ainue mikono yake isiguse chini na aiepushe sehemu ya juu ya mikono iwe kando na mbavu zake , na pia matumbo yake ayaepushe na mapaja yake, na aseme:
[سبحان ربي الأعلى وبحمده]
SUBHANA RABIYAL A’ALAA
[Kutakasika ni kwa Mola wangu Aliye juu kabisa] [Imepokewa na Muslim.] (mara tatu), na akithirishe dua katika kusujudu kwake..
– Kisha atainua kichwa chake huku akileta Takbiri, na hatainua mikono yake na atakaa kwa kukalia mguu wake wa kushoto [Imepokewa na Muslim.],
na kusimamisha mguu wake wa kulia hali ya kuvielekeza vidole vyake upande wa Kibla, aiweke mikono yake juu ya mapaja yake ikiwa imekunjuliwa na vidole vyake vimeelekezwa Kibula na aseme:
[رب اغْفِرْ لِي وَارْحَمْنِي وَاجْبُرْنِي وَاهْدِنِي وَارْزُقْنِي]
RABBI GHFIRLIY WARHAMNIY WAJBURNIY WAHDINIY WARZUQNIY
[Mola wangu! Nisamehe, unirehemu, uniungeunge, uniongoze na uniruzuku] [Imepokewa na Tirmidhi.].
– Kisha atapiga takbiri na asujudu mara ya pili, kisha ainue kichwa chake hali ya kupiga takbiri na akae kikao kidogo kinachoitwa “kikao cha kujipumzisha” kwa hadithi iliyopokewa na Harith bin al-Huwairith Radhi za Allah ziwe juu yake katika kueleza namna ya Swala ya Mtume ﷺ kuwa yeye (alikuwa hainuki mpaka akilingana katika kukaa ) [Imepokewa na Bukhari.]
– Kisha ainuke huku akipiga Takbiri ya rakaa ya pili akijisaidia kwa mikono yake. [Imepokewa na Bukhari.]
– Kisha ataswali rakaa ya pili kama vile ya kwanza, lakini hatasoma dua ya kufungulia Swala.
KIKAO CHA ATTAHIYATU
Amalizapo mwenye kuswali rakaa mbili za kwanza atakaa kikao cha Atahiyatu ya kwanza, akikalia mguu wake wa kushoto hali ya kusimamisha mguu wake wa kulia na kuiweka mikono yake juu ya mapaja yake, na aukunjue mkono wake wa kushoto na akikunje kidole chake kidogo ni kidole cha mwisho cha mkono. na kile kinachokifuatia vya mkono wa kulia, na akikunje kile cha kati pamoja na gumba, na akiinue kidole cha shahada na aashirie kwa kidole chake cha shahada wakati wa kikao cha Atahiyatu, na akitazame kwa macho yake na aseme:
التحيات لله والصلوات والطيبات، السلام عليك أيها النبي ورحمة الله وبركاته، السلام علينا وعلى عباد الله الصالحين، أشهد أن لا إله إلا الله وحده لا شريك له، وأشهد أن محمداً عبده ورسوله
ATTAHIYATU LILLAH WASWALAWATU WATWAYYIBAAT,ASSALAMU ALAYKA AYYUHA NNABIYU WARAHMATULLAH WABARAKAATUHU,ASSALAMU ALAYNAA WA’ALAA IBAADILLAHI SWALIHINA,ASH’HADU ANLAA ILAHA ILLA ALLAH WAHDAHU LAA SHARIKALAHU,WA’ASH’HADU ANNA MUHAMMAD ABDUHU WARASULUHU
[Kila jinsi ya maamkuzi mema ni ya Mwenyezi Mungu, na rehema na mazuri yote. Amani ikushukie wewe, ewe Nabii, na rehema ya Mwenyezi Mungu na baraka Zake. Amani itushukie sisi na iwashukie waja wema wa Mwenyezi Mungu. Ninaakiri kwamba hapana mola anaestahiki kuabudiwa kwa haki isipokuwa mwenyezi Mungu Asiekuwa na mshirika, na ninakiri kwamba Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake] [Imepokewa na Bukhari.].
– Kisha atainuka huku akipiga Takbiri, iwapo Swala ni zaidi ya rakaa mbili, na ainue mikono yake apigapo Takbiri, na hatosoma katika rakaa zisaliezo isipokuwa Fatiha.
– Na atakaa kikao. cha tawarruk [Imepokewa na Abu Daud.]
Na Tawarruk: Ni kuutoa mguu wa kushoto upande wa kulia na kuutaza na akalie matako yake, na mguu wa kulia usimamishwe.
Katika Atahiyatu ya mwisho.Na aseme matamko yaliyokuja kwenye Atahiyatu ya kwanza na azidishe juu yake:
اللهم صل على محمد وعلى آل محمد كما صليت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد، اللهم بارك على محمد وعلى آل محمد كما باركت على إبراهيم وعلى آل إبراهيم إنك حميد مجيد
ALLAHUMMA SWALLI ALAA MUHAMMAD WA’ALAA AALI MUHAMMA,KAMAA SWALLAYTA ALAA IBRAHIM WA’ALAA IBRAHIM INNAKA HAMIIDUN MAJIID,ALLAHUMMA BAARIK ALAA MUHAMMAD WA’ALAA AALI MUHAMMAD,KAMAA BAARAKTA ALAA IBRAHIM WA’ALAA IBRAHIM INNAKA HAMIIDUN MAJIID
[Ewe Mola! Mrehemu Muhammad na jamaa za Muhammad, kama ulivyomrehemu Ibrahim na jamaa za Ibrahim, wewe ni Mwingi wa kuhimidiwa, ni Mwingi wa kusifiwa na kutukuzwa. Ewe Mola Mbarikie Muhammad na jamaa za Muhammad kama ulivyombarikia Ibrahim na jamaa za ibrahim, hakika wewe ni Mwingi wa kuhimidiwa, ni Mwingi wa kusifiwa na kutukuzwa] [Imepokewa na Bukhari.]
– Kisha aseme:
[اللهم إني أعوذ بك من عذاب جهنم ومن عذاب القبر ومن فتنة المحيا والممات ومن فتنة المسيح الدجال]
ALLAHUMMA INNIY A’UDHUBIKA MIN ADHABI JAHANNAM,WAMIN ADHAABIL QABRI WAMINFITNATULMAHYAA WALMAMAATI WAMINFITANATUL MASIIH DAJJAL
[Ewe Mola! Mimi najilinda kwako na adhabu ya Jahanamu na adhabu ya kaburi na maonjo ya uhai na umaiti na shari ya fitna za Al-Masih Al-Dajjal] [Imepokewa na Bukhari.].
KUTOA SALAMU
Mwisho wa Swala atatoa Salamu upande wake wa kulia na aseme:
[السلام عليكم ورحمة الله]
ASSALAMU ALAYKUM WARAHMATULLAH WABARAKAATUH
[Amani iwe juu yenu na rehema ya Mwenyezi Mungu] [Imepokewa na Muslim.],
na upande wa kushoto kadhalika.