0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA UTUMWA. (4)

KANUNI ZA KIISLAMU ZA KUMWACHA HURU MTUMWA

Uislamu umeweka kanuni maalumu kuwa endapo imetokea bwana anae mmiliki mtumwa akawa amempiga mtumwa wake mpaka akamjeruhi, basi ni lazima kwake kisheria kumwacha huru na sio hiari. Kama alivyo sema Mtume ﷺ katika hadithi sahih aloipokea Imamu Ahmadi kuwa : kuna mtu mmoja alimumiza mtumwa wake pua yake, Mtume akasema : “Wewe tayari uko huru” kisha Yule aliyekuwa Mtumwa akauliza nitakuwa chini ya usimamizi wa nani mimi ewe Mtume. Mtume akajibu utakuwa chini ya usimamizi wa Allah na Mtume wake.

Endapo watu wawili wali mnunua mtumwa mmoja kwa ushirika, kisha mmoja wao akaamua kumwaacha huru nusu ya malipo yake yote aliyo yatoa, basi na nusu nyingine ya mwenzake nayo atalazimika kisheria nae kumwacha huru ili awe huru kilamilifu. Kwa mujibu wa hadithi ya mtume isemayo: “Mtu yeyote atakaeshirikiana na mwenzake katika mtumwa mmoja kisha mwenzake akamwacha huru kwa nusu ya mali waliyo shirikiana, basi ni lazima kwa mshirika mwingine nae amwache huru mtumwa huyo”.
Kama mtu alimiliki mtumwa katika maharimu zake basi ni lazima kwake bila hiyari kumwacha huru.

NJIA ZA HATUA KWA HATUA KATIKA KUMWACHA HURU MTUMWA:

Uislamu umehimiza kupitia njia hii ya hatua kwa hatua watu wanaomiliki watumwa wawachie huru ili waweze kuokoka kutokana na siku nzito ya Qiyama, na kama wanataka kuokoka na mazito ya siku hiyo, basi cha kuwaokoa wao ni kuwaacha watumwa huru. Ni siku ambayo Mitume wenyewe watakosa majibu ya kumjibu Allah. Siku mtu atakapo mkimbia baba yake na mama yake, siku ambayo mtu dhalimu atang’ata vidole vyake kwa hasara aliyo ipata, Siku ambayo mtu aliye kufuru atasema: Bora mimi ningekuwa mchanga tu (kuliko kuwa mtu)!!.

Allah mtukufu amesema katika aya ya 11-13 Surati Balad:

{فَلَا اقْتَحَمَ الْعَقَبَةَ , وَمَا أَدْرَاكَ مَا الْعَقَبَةُ , فَكُّ رَقَبَةٍ}

[Je! Ameukata huo Mlima, Ni nini kitakacho kujulisha huo Mlima ni nini?, Ni kumkomboa Mtumwa]

Na Mtume ﷺ amesema : “mtu yoyote atakaye mwachia huru mtumwa mwislamu allah atamwachia huru kila kiungo chake kutokana na moto” amepokea bukheri na musimu.
Amesema tena Mtume ﷺ :

[وأيما امرئ مسلم أعتق امرأتين مسلمتين كانتا فكاكه من النار….]     رواه الترمذي

[…..Na mtu yeyote mwislamu atakae waachia huru wanawake wawili wa kiislamu basi wana kuwa hao kwake yeye ni fidia yake kutokana na moto]    [Imepokewa na Al Tirmidhiy]
Na swahaba mtukufu wa Mtume Abuudhari Allah amaridhia amesema: Nilimuuliza mtume ﷺ juu ya yapi matendo yaliyo na fadhila kubwa?, Akasema: ‘Ni kumwamini Allah na kupigania jihadi katika njia ya Allah, Kisha nikamuuliza ni zipi shingo zilizo na malipo makubwa kwa kuachwa huru?, Akasema: Ni zile zilizo nunuliwa kwa gharama kubwa na zenye ubora mkubwa kwa wanazo zimiliki, (Yaani ni wale watumwa walio nunuliwa kwa gharama kubwa na wenye kuthaminiwa sana na mabosi wao (Massayidi).
NJIA YA ubinabadamu
Kwa kuzingatia ubinatamu (utu) wa mtumwa kuwa naye anastahiki haki zote kama binadamu wengine, uislamu umemwamrisha Bwana anae miliki watumwa asiwanyanyapae kifikira wala kimazingira, bali anacho takiwa ni kuamiliana nao kwa upole, ustaarabu na huruma ya kweli kwa kipindi cha muda wote watakapokuwa chini ya miliki yake.
Amesema Mtume ﷺ :

إِخْوَانُكُمْ خَوَلُكُمْ، جَعَلَهُمُ اللّه تحْتَ أيْدِيكُمْ. فَمَنْ كَانَ أخُوهُ تَحْتَ يَدِهِ فَلْيُطْعِمْهُ مما يأكُلُ وَلْيُلْبِسْهُ مِما يَلْبَسُ. ولا تُكَلِّفُوهُمْ ما يَغْلِبُهُمْ فإنْ تكلَّفوهُمْ فأعِينُوهُمْ      متفق عليه

[Hao watumwa ni ndugu zenu, Allah ndie alie kadiria wakawa chini ya miliki yenu, Basi hakikisheni kuwa mnawalisha chakula mnachokula nyinyi wenyewe, (wala msiwabague) na wavalisheni mavazi mazuri kama mnavyovaa nyinyi, Na wala msiwape kazi ngumu zinazowashinda wao, ama ikitokea mumewapa kazi nzito zaidi ya uweo wao basi wasaidieni]     [Imepokewa na Bukhari na Muslim]

Ukiangalia hadithi hii tukufu ndipo utakapoona mtumwa katika miliki ya kiislamu hana tofauti na mtu alie huru ispaokuwa majina tu, kwamba huyu ni mtu huru na huyu ni mtumwa, lakini ukija katika mavazi, chakula, kazi wanazofanya n,k , hautoona tofauti.
Hivyo basi uislamu pekee ndio ulio anzisha njia nyingi za kuwatoa watu utumwani na ukabakisha kwa dharura tu njia moja ya utumwa, ambayo ni vitani.

SABABU YA YA UISLAMU KUFUNGUA NJIA NYINGI ZA KUWATOA WATU UTUMWANI:

Uislamu umefungua njia nyingi za kuwatoa watu katika utumwa. Ili uislamu ubakie kuwa haumiliki mtumwa hata mmoja katika mgongo wa ardhi. Na kweli wakati Mtume wetu Mohammad ﷺ amefariki hakukuwa na nyumba yoyote ya waislamu inayo miliki hata mtumwa mmoja, bali watu wali waachia huru watumwa wao wote kupitia njia mbalimbali zilizo wekwa na uislamu.
Hivyo tutaendelea kusema kwamba uislamu pekee ndio ulio unga mkono kuachwa huru watu na ukadhibiti kabisa njia na sababu za watu kuwa watumwa.
Swali : kama kweli uislamu umeunga mkono jambo la kudhibiti utumwa kwanini umeendelea kuwa na watumwa kwa njia ya vita?!
Jawabu : Uislamu umebakisha utumwa katika jambo la vita tu kama tulivyoeleza huko nyuma kwa sababu kuu ifuatayo:- Wakati watu wanapopigana vita kuwa kuwa kuna mambo makuu mawili: Ima kuuwa au kuuwawa.
Inapotokea Jeshi la Kiislamu limewakamata mateka wa Makafiri, inakuwa ni halali juu yao kuwauwa kwa sababu wao walikuja kwa nia ya kuwauwa waislamu.
Lakini kwa uzuri na huruma ya dini ya kiislamu unamwambia yule mtu badala ya kukuuwa nitakuacha hai lakini utakuwa chini ya usimamizi wangu ukiwa ni mtumwa.
Kwa mfano: Waislamu wanapowakamata mateka wanawauliza mateka hao, Je tukuuweni tukufanyeni watumwa?! Hakuna shaka kwamba watachagua utumwa kuliko kifo kwa sababu utumwa utawabakisha wao kuwa hai.
Pia kitendo cha kubakishwa utumwa katika mateka wa kivita ndani ya dini ya kiislamu ni njia kuu vile vile ya kuzuia umwagaji damu ya binadamu. Hata kama mtu huyu si mwislamu kwa sababu Allah amempa mwanadamu heshima ya kipekee kwa kumfadhilisha juu ya viumbe wengine hata kama ni kafiri, japo uislamu hautaridhika nae mtu huyo kama uhai wake utakuwa ni kipingamizi kikuu cha kuzuia uislamu usiendelee mbele huyo ata uwaa kwa kuwa yeye atakuwa ni mtu pekee aliye fanya uovu mkubwa na uadui dhidi ya uislamu na waislamu.
Jambo jingine ni kwamba mateka wakivita kuwa chini ya waislamu baada ya kutekwa ndani yake kuna manufaa makubwa kwa waislamu.
Wataweza kutumika katika kubadilishana mateka kwa mateka
Pili wataweza kutumika katika kutoa fidia ya mali ambazo zitawasaidia waislamu.
Swali; Kwanini uislamu umeruhusu mwanaume wa kiislamu kumiliki watumwa wanawake zaidi ya wanne na kuendelea kuwatumia kama wake zao bila kikomo, lakini ukaweka sheria kwa wanawake wasio kuwa watumwa mwisho wanne tu?
Je hamuoni kuwa kutokuweka kikomo maalumu kwa watumwa wa kike kumilikiwa na mtu mmoja ni sehemu katika kuwadhalilisha wao kijinsia?
Jawabu : kitendo hicho hakina udhalilishaji hata kidogo, bali tambua kuwa hii ni njia nyingine ya kipekee katika zile njia tulizozitaja kule mwanzo, ni njia mojawapo ya kudhibiti utumwa usiendelee kama ifuatavyo:-
Kama mwanamke huyu mtumwa akiachwa na bwana anaemmiliki akawa hamwingilii kimwili. Na ikatokea akaolewa na mtu mwingine kinyume na bwana wake mmiliki, basi watoto ambao atazaa mtumwa huyo na mtu mwingine kinyume na bwana wake watakuwa ni watoto watumwa kwa mujibu wa sheria ya kiislamu, isipokuwa endapo mwanamke huyo ataingiliwa kimwili na bwana wake anaemiliki basi watoto atakao wazaa watakuwa ni watoto huru sio watumwa kwa sababu wametokana na miliki halisi tu.
Endapo huyo mwanamke mtumwa atazaa na asie kuwa mmiliki wake halisi, hata kilichozaliwa kitakuwa ni mali ya huyo bwana wake anaye mmiliki, kwa sababu mtu anapokuwa mtumwa kila jambo analolifanya linakuwa ni mali ya bwana wake mmiliki. Hivyo mtoto nae ataingia kwenye umiliki wa bwana wake kwa kuwa ametokana na chumo la mama yake ambae ni mtumwa wa mtu.
Bila shaka hii itafanya ongezeko la watumwa kuzidi na kujaa tena, tofauti kama angezaa na bwana wake mmiliki watoto wasingelikuwa watumwa, naye angekuwa mama watoto wa bwana wake (mmiliki wake), Na endapo mwanae atakuwa na akamkuta mama yake ni mtumwa basi hatomfanya mtumwa bali atamwachia huru. Mtume ﷺ amesema katika hadithi :

[لا يَجزي ولدٌ والدًا، إلا أن يجده مملوكًا فيشتريه فيعتقه]    رواه مسلم

[hawaezi kumlipa mtoto mzazi wake malipo ya hali ya juu kabisa kuliko atakapomkuta ni mtumwa kisha akamwacha huru].   [Impokewa na Muslim]

Si hivyo tu huenda bwana (mmiliki) watumwa akaamua kumwacha huru tu kwa ajili ya kuogopa uzito wa siku ya kiama, au kwa kulipa fidia ya kosa miongoni mwa makosa aliyo yafanya kisheria yanayomtaka ajikomboe kwa kuacha huru mtumwa.
Uislam pia unakusudia kunyanyua heshima ya ubinadamu (utu) wake na kutunza heshima ya mwanamke, hasa anapo kuwa yeye ni mtumwa lakini bwana wake mmiliki anafanya tendo la ndoa bila ya shaka wala kumnyanyapaa na ilihali ana wake zake walio huru. Hivyo ataona kwamba hakuna utofauti kati yake na wanawake huru katika tendo la ndoa na starehe ya kimwili.
Uislamu kumruhusu bwana amwingilie mtumwa wake wa kike kimwili pia litamsaidia mtumwa huyu wa kike kutokuwa na tabia mbovu za uzinzi, kwa muda wote atakuwa katika hifadhi ya bwana wake katika mahitaji yake muhimu ya chakula malezi mavazi na tendo la ndoa.
Swali : Ni lipi lengo kuu la kuwekwa sheria ya kukamata mateka katika dini ya kiislamu wakati wa vita?
Jawabu: Kuwekwa sheria ya kukamata mateka katika vita kati ya waislamu na wasio kuwa waislamu lengo kuu ni kuhifadhi damu za watu zisimwagike ovyo bila ya sababu ya msingi.
Kwa sababu Allah alipoweka sheria ya kukamatwa mateka katika vita ameihami damu ya mtu kafiri anae tupiga vita na yule asie tupiga vita, kwamba yeye Allah akuhalalisha watu hawa makafiri kuuwawa ovyo tu kwa kuwa waislamu wanao uwezo wa kufanya hivyo. ni bora wakawateka na kukaa nao badala ya kuwauwa ovyo.
Pia kitendo hicho cha kutowauwa binadamu walokuwa wamekusudia kuuwa, ni fundisho kwa wao mateka na wengineo watambue kuwa uislamu ni dini ya haki, na ndiyo dini ya mungu aloiridhia, kwasababu inachunga usalama wa binadamu, hairuhusu kumbughudhi mtu katika nafsi yake, mali yake, heshima yake n.k ispokuwa kwa mambo ya kisheria yatakayolazimisha kufanya hivyo.
Ukifuatilia historia ya uislamu utakuta kuna mateka wengi waliingia katika dini ya kiislamu na wakawa waumini wazuri sana wa dini ya kiislamu baada ya kukamatwa mateka wakafanyiwa wema na muamala mzuri mpaka wakaupenda uislamu kwa mazuri waliyo yaona kwa waislamu.

MAKALA YAENDELEA

IMEANDIKWA NA SHEIKH: ABDULQADIR AL-AHDAL

TAFSIRI:

BASHIRU SHABANI & AMRY SHAMBULA.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.