0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MTAZAMO WA UISLAMU JUU YA UTUMWA. (3)

SABABU MUHIMU ILIYOPELEKEA WAISLAMU KUMILIKI WATUMWA BAADA YA KUWATEKA VITANI.

Hii ni kutokana na kurudisha kisasi na itasaidia kwa waislamu kuwa na nguvu juu ya maadui zao. Pia itawapa uhuru mateka badala ya kuuawa wataachwa huru lakini wakiwa mateka na watumwa.

Lakini suala la mateka na utumwa litaangaliwa kama ifuatavyo:-
Endapo hao watu walioingia vitani kati yao na waislamu kama huwa wana tabia ya kuteka nao watatekwa bila ya kuachwa huru.
Kama huwa hawana tabia ya kuteka nao hawatatekwa.
Kama huwa wana tabia ya kuwafanya mateka watumwa nao watafanywa watumwa.
Na kama wakiwakamata mateka wanawauwa nao wakikamatwa mateka watauwawa.
Hebu jiulize?! : Mmarekani alipo mvamia Mjapan na akawapiga Wajapani kwa Kombora zito mwaka 1945 katika Mji wa Hiroshima. Je unadhani kama Wajapani nao wangekuwa na Kombora zito kama hilo waliliopigwa na Wamarekani unadhani Wajapani wasingerusha na wao Kombora hilo kuwapiga Wamarekani kwa kulipiza kisasi?. Jibu ni kwamba wangelipa kisasai tu.
Hapa ndio tunasema kwamba pale uislamu ulipo bakisha njia ya vita ndio njia pekee ya kupatia utumwa hii haimaanishi kuwa Uislamu unaendeleza utumwa na una upa nguvu bali Uislamu umeacha njia hii kwa ajili ya kulipiza kisasi.
Tena ukichukulia kipindi Uislamu unatangazwa hapo mwanzo kulikuwa na vita Vingi kati ya Waislamu na wasio kuwa Waislamu. Hivyo basi haingii akilini unapigana vita na watu wanaoteka wanajeshi wako na familia zako na watoto pia. Halafu wewe ukawa hauwateki wao hata kidogo.
Hivyo basi kwa hali kama hii tuliyoieleza ndio imefanya Uislamu ubakishe njia moja ya kuingia katika utumwa ambayo ni mateka wa kivita. Japokuwa ukiangalia utaratibu uliopo katika dini ya kiislamu katika kuwamiliki hao mateka utaelewa kwamba mateka waliotekwa na waislamu wanapewa haki zao za misingi zote za kibinadamu na kijamii, sio kama mateka waislamu wanapotekwa na maadui zao.

Soma katika aya hii Mwenyezi Mungu anaelezea Sifa za Waumini mingoni mwasifa hizo ni kuwalisha Mateka wakitaraji malipo kwa Allah.

{وَيُطْعِمُونَ الطَّعَامَ عَلَىٰ حُبِّهِ مِسْكِينًا وَيَتِيمًا وَأَسِيرًا إِنَّمَا نُطْعِمُكُمْ لِوَجْهِ اللَّهِ لَا نُرِيدُ مِنكُمْ جَزَاءً وَلَا شُكُورًا}    الأنسان:8-9

[Na huwalisha chakula, juu ya kukipenda kwake, masikini, na yatima, na wafungwa.Hakika sisi tunakulisheni kwa wajihi wa Mwenyezi Mungu. Hatutaki kwenu malipo wala shukrani.]     [Al Insaan:8-9]

Maadui wa Waislamu wanapo wateka wanawake huwafanyia vitendo vya unyama kwa kuwabaka na kuwadhalilisha kijinsia.

Lakini kwa waislam endapo watatekwa wanawake watakaa chini ya utawala wakiwa ni wake za watu maalumu.
Endapo waislamu watakuwa hawachukui mateka kwa maadui zao, lakini maadui zao wakawa wanateka waislamu, basi jambo hilo litatia unyonge katika nyoyo za wapiganaji wa kiislamu na litapelekeka jeshi kushindwa nguvu na kufeli kabisa, ndipo Uislamu kwa kuchunga hayo yote ukaweka sheria ya kuwepo mateka na watumwa katika njia ya vitani tu.
Mtume ﷺ alipopigana vita na kabila la Banii-Mustaliq, na akateka wanawake zao. hii ni kwa sababu kabila hilo lilikuwa na tabia ya kuteka watu pale wanapopigana nao vita.
Lakini kuna vita nyingine Mtume alipigana na Maqurayish na hakuwateka hata kidogo, hii ni kwa sababu wao walikuwa hawana tabia ya kuchukua mateka wanapo pigana na maadui zao.
Hata hivyo ukitizama vyema aya hii tukufu ndipo utaelewa kuwa Uislam haukuamrisha watu wawe na watumwa, pia hakuna hadithi iliyo amrisha moja kwa moja kumiliki watumwa, hata wakati wa vita hauja amrisha moja kwa moja kwa kusema (Wafanyeni adui zenu watumwa).
Anasema allah mtukufu:

فَإِذَا لَقِيتُمُ الَّذِينَ كَفَرُوا فَضَرْبَ الرِّقَابِ حَتَّى إِذَا أَثْخَنْتُمُوهُمْ فَشُدُّوا الْوَثَاقَ فَإِمَّا مَنًّا بَعْدُ وَإِمَّا فِدَاءً حَتَّى تَضَعَ الْحَرْبُ أَوْزَارَهَا}     محمد:4}

[Basi mnapo wakuta walio kufuru wapigeni shingoni mwao mpaka mkiwadhoofisha wafungeni pingu Tena waachilieni kwa hisani au wajikomboe mpaka vita vitulie…”.]        [Muhammad:4]

Ukitazama aya hii tukufu haija amrisha kuwepo watumwa hata kidogo japokuwa imeeleza kukaa na mateka kwa muda kisha kiongozi akitaka awachie huru au wajikomboe baada ya kumalizika vita, na wala aya haisemi mkiwateka basi moja kwa moja hao ni watumwa wenu.
Hapo ndipo utakapojua vyema kuwa Uislamu haukuunga mkono mwendelezo wa utumwa, bali umesapoti njia za watu kutokuwa watumwa, ingawa tabia ya utumwa ilikuwepo tangu na tangu kabla ya kuja Uislam alioueneza Mtume wetu Mohammad ﷺ.
Ukizingatia kuwa utumwa ilikuwa ni tatizo kuu la kijamii ambalo lilihitaji kulitatuliwa na kuondolewa katika jamii hadi liishe kabisa. Kwa kuwa tatizo hili liliota mizizi sana katika jamii mbalimbali lilihitaji ustaarabu wa hali ya juu katika kuliondosha kwa watu, na wala sio kukurupuka na kulikemea mara moja kwa nguvu moja tu, bali lilihitaji hatua kwa hatua.
Kwa mfano : Mwaka 1861 Rais wa Marekani Bwana ABRAHAM LINKULIN ambaye alikuwa Rais wa Nchi hiyo kuanzia mwaka 1861 hadi 1865. Mara tu baada ya kuwa Rais aliamuru kuwa watu wote nchi nzima wanao miliki watumwa wanatakiwa wawaachie huru, baada ya Rais ABRAHAM kutoa amri hiyo watu wote walitii na kuwaacha huru watumwa wote. Lakini cha kushangaza baada ya watumwa hao kuwa waendelee na mambo yao wamekuwa huru, walirudi kwa mabosi wao walokuwa watumwa kwao!
Sasa tujiulize ni kwanini warudi na wakati tayari walishaachwa huru??.
Jawabu:
Jambo la kwanza: lililo wafanya wao wenyewe waamue kurudi kwa mabosi wao na kutaka waendelee kuwa watumwa, ni kutokana na jamii ilikuwa ina wanyanyapaa. Kwa sababu jamii ilishazoea kuwaona wao wakiwa utumwani nabado haijapewa elimu ya kuwa ona wao nao ni watu wanaostahiki kuwa huru na kuishi na jamii.
Mfano: Hii ikumbukwe kuwa mwaka 1992 ulipoanza ugonjwa wa Ukimwi mkoani Kagera watu walikuwa wana wanyanyapaa wagonjwa hao wa UKIMWI hadi serikali ilipoanza kutoa eliku kwa jamii kuwa hawa ni watu kama sisi na wala ukiwa nao sio kwamba atakuambukiza ndipo jamii ikawakubali na ikaondoa unayanyapaa baada ya taaluma kutolewa.
Hivyo basi Rais wa Marekeni IBRAHAM yeye alitoa amri ya kuachwa huru watumwa wote mara moja kabla ya kuifundisha jamii iwaozee kuwa nao ni watu wanaostahiki uhuru kama wenzao.
Jambo la pili: lililo wafanya watumwa kurudi kwa mabosi wao baada ya Amri ya Rais ABRAHAM. Ni jambo la kisaikolojia na hali ya mazoea ya mazingira. Yaani watumwa wenyewe akili zao zilikuwa sio akili huru tena, ni akili ambazo zimekwisha athirika kuamrishwa kila siku, akili ambazo hazijazoea kupanga na kuamua mambo kutoka kwenye vichwa vyao.
Hivyo amri ilipotolewa na Rais IBRAHAM kuwa watumwa waachwe huru kipindi hicho ilikuwa akili zao hazikuandaliwa kitaaluma kwamba wajijue kuwa wao ni watu huru ambao wanaweza kufanya kazi kwa kuamua na kupanga wenyewe vichwani mwao.
Kwa hiyo hali halisi ikaonesha walipata uhuru wa mwili kabla ya uhuru wa akili na ndio maana walirudi tena kwa mabosi wao kuomba waendelee kuwa ni watumwa.
Hivyo basi ndio maana Uislamu kwa kutambua athari kama hizo hauku kurupuka tu kutoa katazo mara moja la kutomiliki watumwa, bali uliweka njia ambazo zitawatoa watu katika utumwa kidogo kidogo mpaka waishe kabisa.
Kama ulivyo fanya Uislamu katika kuikataza pombe kidogo kidogo hadi mwishowe kuiharamisha kabisa, na hii ni kwa sababu unywaji pombe ulikuwa ni kama kitu cha kawaida sana katika jamii ya waarabu, ilikuwa ni vigumu kuiharamisha mara moja kwa kauli moja tu ya (acheni kunywa pombe) bali hekima ikapelekea kukatazwa hatua kwa hatua.
Utumwa na haukukatazwa mara moja tu kwa kauli moja kwa sababu utumwa ulikuwa unatumika katika nchi nyingi kipindi hicho kama sehemu ya pato la nchi. Na pia ilikuwa ni biashara kuu ya mataifa ya Marekani ya sasa na Uingereza ya sasa na baadhi ya nchi zingine.
Hivyo ilikuwa ni muhali kwa dini ya kiislamu kutoa kauli moja ya kuacha utumwa jambo ambalo lisingewezekana kwa uharaka wa namna hiyo na ndio maana ukatoa njia za utaratibu zinazolimaliza tatizo hilo.
Kwa sababu ingetolewa kauli moja ingesababisha mporomoko mkubwa sana katika uchumi wa mataifa kwa kipindi hicho jambo ambalo madhara yake yange wagusa hadi wananchi wa hali ya chini kabisa kwa kipindi hicho na watu wengi wangepata hasara kwa siku moja tu. Na sio lengo la Uislam kuwapatisha watu hasara duniani.
Kwa sababau hizo tulizo zitaja hapo zinatufahamisha kwamba Uislam uliangalia mbali sana katika jambo zima la kuharamisha utumwa , badala yake zikawekwa kanuni mbalimbali zitakazoteketeza utumwa.
Uislamu pekee ndio umeweka njia na namna nzuri ya kutatua au kutibu tatizo sugu la utumwa. Na njia hizo ni
Njia za Kikanuni
Njia ya hatua kwa hatua
Njia ya Utu (Ubinadamu)
Na lengo kuu la kuwekwa njia hizi ni kupatikana binadamu huru kikamilifu kiakili, kimwili na kijamii.
Kiakili: Yaani akili yake ijitambue kuwe yeye ni mtu huru na ana uhuru wa kutoa maamuzi sahihi na kufanya kwa mujibu wa kile anachokiamua.
Kimwili: Yaani mwili wake pia uwe sehemu huru isije ikawa akili yake iko huru na mwili wake bado unatumikia utumwa.
Kijamii: Yaani jamii nayo ielewe kuwa maana ya mtu kuwa huru, ni kujikomboa utumwani na kuwa na maamuzi yake sahihi ya kiakili na kivitendo, na anahaki ya kushirikiana na jamii kama binadamu wengine. hivyo inakubali kwamba ni mtu huru katika mujitamaa.

MAKALA YAENDELEA

IMEANDIKWA NA SHEIKH: ABDULQADIR AL-AHDAL

TAFSIRI:

BASHIRU SHABANI & AMRY SHAMBULA.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.