0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MIUJIZA YA YESU

MIUJIZA YA YESU

Miujiza imetajwa tukio linalo enda kinyume na taratibu tuzijuazo kama wanadamu, na ni Dalili kutoka kwa Allah[swt] ili waja wajue na kumtambua alowaumba, pia kupitia miujiza Allah[swt] huwatia nguvu Mitume na Manabii wake ili kuwabainisha hao Mitume na Manabii kuwa ni wakweli [Yohana 11:38-44] kinyume na leo ambapo kila mmoja katika jumuiya ya wakristu anauza ‘miujiza ‘ kwenye radio, runinga,magazeti na hata kwenye mitandao.

Mitume wengi na Manabii waliotimilizwa, Allah[swt] aliwajaalia miujiza mbali mbali, na Yesu mwana wa Mariam ni mmoja wao na kabla yake walikuweko Manabii wengi tu na Miujiza mikubwa wala hawakuitwa waungu au wana wa mungu ila walifahamika kwa vyeo vyao tu …Manabii!.

Wana wa Israeli waliletewa Manabii wengi tu, lakini wakawafanyia vitimbi vikubwa kwa kuwaaua baadhi yao, kuwatesa na wengine kuwatoa mijini kwao, na Yesu mwana wa Mariam si wa kwanza, na ukisoma Kumbu Kumbu la Torati 31:27-30, yaonyesha malalamishi ya Nabii Musa Ibn Imran kuwa pindi atakapoondoka wana wa Israeli watageukia ibaada ya masanamu, na kuwaua waliotumwa kwao na Yoshua mwana wa Nun naye aliwaapiza wana wa Israeli wote na shahidi wake ni JIWE lisilokuwa na uhai machoni pao na wakamuona kama mtu aliyetokwa na akili, Yoshua 24:24-28.

Yesu mwana wa Mariam aliwasuta wana wa Israeli kuwa wamefanana na makaburi yaliyo pambwa kwa nje, lakini kwa ndani ni uozo na mifupa ya watu waliomuasi Allah [swt] na Manabii wake, Mathayo 23:27,na Mathayo 23:34-37. Kumhusu Yesu mwana wa Mariam, ushahidi ulioko ni wazi kuwa ni Mtume kwa wana wa Israeli tu, wala si kwako ndugu mkristu,Mathayo 15:21-26, Mtahayo 10:23, Matendo 5:31, na Quraan iliyo teremshwa na Allah[swt] kwa Mtume[saw] takriban miaka mia sita [600] yasadikisha hayo sasa huo ujanja wa kikristu mtaupata wapi?.

Allah [swt] anapolitaka jambo lake huliambia  “kua na hua”  Quraan 36:82, Zaburi 33:6,9,na Quraan 19:35, na Yesu mwana wa Mariam alijaaliwa muujiza wa kutengeza kwa udongo mfano wa ndege akampuliza mara akaruka kwa idhini ya Allah [swt] na ukawa ni muujiza kwa wana wa Israeli kama vile Mama yake alivyofanywa muujiza kwa kumzaa mwanawe Yesu bila kuingiliwa na mume yeyote ila kwa mapenzi yake Allah[swt].

Tafsir ya Ibn Abbass na Qurtubi katika aya hii Quraan 3:48-49, zasema kuwa huo mfano wa ndege alikuwa ni ‘ khufash ‘ popo ambaye japo huruka kama ndege ,hatagi mayai bali hunyonyesha.

Twatoa mfano huu kwa sababu wakristu wengi kama wayahoodi hawakumwamini Yesu mwana wa Mariam kama Nabii,kwa hivyo wakampa masharti afanye ndio wapate kuamini, kwetu Waislamu ni kuwa tumesikia na tumetii.

Katika maelezo sahihi ya Uislamu ni kuwa Yesu mwana wa Mariam aliwafufua watu watatu pekee, nao ni: Aadhir, Ibn ajuzi [mtoto wa ajuza mcha Mungu na Sam Ibn Nuhu aliyekuwa amekufa karne kadhaa. Wakwanza wawili baada ya kufufuliwa waliishi miaka mingi hata wakawa na familia zao, ama Ibn Nuhu kama angeweza kufufua kimiujiza mtu aliyekufa karne nyingi zilizopita, na kwa uwezo wa Allah [swt] yote yakawezekana na ningependa kusizitiza kuwa kabla ya miujiza yote hii Yesu mwana wa Mariam alikuwa akiswali rakaa mbili kwa Muumba.

Japo Waislam wanazo habari zote hizi kamwe hatuja tokwa na akili na kudai Yesu mwana wa Mariam ni Mungu, na hata kitabu cha wakristu, biblia,chakubali kuwa Yesu mwana wa Mariam si Mungu bali ni Mtumishi tu; Yohana 5:30, Matendo 2:22, Yohana 14:28, Luka 11:20. Bibilia kwa upande wake imeonyesha muujiza wa kwanza wa Yesu mwana wa Mariam alitengeza ‘ Divai ‘ watu wakanywa na kulewa [ Yohana 2:1-11. Kwa maelezo sahih, wako Manabii wengi walio fanya miujiza ya ajabu lakini wao si waola, soma miujiza ya Nabii Musa Ibn Imran, Nabii Yona, Nabii Ezekieli n.k.

Zama za Nabii Yesu mwana wa Mariam kulikuwa na ujuzi mkubwa wa tiba, na matabibu walikuwa wakishindana katika tiba, lakini mambo matatu yaliwashinda nayo ni kufufua waliokufa, mbalanga na upofu wa tangu kuzaliwa. Zama za Mtume[saw] ni zama za ufahamu, balagha na elimu ya hali ya juu na Mtume [saw] akapewa Muujiza mkubwa kuliko yote nayo ni QURAAN, imebakia katika asili ile ile namna ilivyoteremshwa [Quraan 15:9] kinyume na bibilia ambayo ina chapa zaidi ya mia [100]!

IMETAYARISHWA NA :
ADAM AMBETSA
MWEMBE TAYARI TABLIGH GROUP
MOBILE NO. 0723 17 41 54
MOMBASA, KENYA.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.