0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

JE YESU NA ISSA (A.S) NI MTU MMOJA??

JE YESU NA ISSA (A.S) NI MTU MMOJA?

Mwanadamu anapoongozwa na uoga, mara nyingi hutoka katika mipangilio sahihi

na kuchukua muda wake mwingi akijaribu kubuni njia na mikakati ya kumkinga

asipoteze alichonacho na waliomzunguka. Kwa hivyo hujifanya kama ni tofauti na

wale wanaomsikiza kiakili, katika kuelewa na kwa njia hii hubuni uwongo wa

kumdumisha katika biashara ya pekee anayoijua yeye.

Waislamu hatukuamriwa kudharau, kuchukia au kubagua mtu yeyote kwa misingi

ya rangi, awe mke au mume kuwa tukuza Manabii hadi kiwango cha kusema

ili kujifurahisha tu kwa muda kuwa Yesu, Issa na Jesus ni watu tofauti, bali Quran

imetuamuru hivi:

“Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyoteremshiwa sisi, na

aliyoteremshiwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaqub na wajukuu zao na

aliyopewa Musa na Issa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao. Hatubagui

baina yao hata mmoja na sisi ni wenyekevu kwake.” (TMQ 3:84)

Sisi waislamu hatuna tabia ya baadhi ya wakristo kubagua Manabii, bali

tunawaamini, kuwataja kwa heshima yao pamoja na kuwahami kutokana na wale

ambao wana itikadi mbaya. Lakini kila wakati waislamu wanapokuja pamoja ili

waishi kwa undugu wa kibinadamu na wakristo, wako wanaotafuna changarawe

za fitna eti Yesu, Issa na Jesus ni watu tofauti!

Katika kurasa hizi hatulengi kuunga wala kupinga wale wakristo wanaosema Yesu

mwana wa maryamu ndiye mungu, mwana wa mungu au zote (mungu tena

mwana wa mungu) bali ni kukupeni mwelekeo ulio sahihi kwa atakaye maana,

hakuna kulazimisha mtu katika dini (Quran 2:256)

Ulimwengu umeweka vitu vinavyoitwa International Standards na huwezi kuleta

chochote kinyume chake, na kuwa umekileta na kinatumika sio dalili kuwa uko

sawa, bali wale waasisi wa ubaya huo wanafurahi kukuona ukididimia kwenye

lindi la upotovu.

Ni habari za kuaminika kuwa kuna vitu vinne kisheria ya uandishi havifanyiwi

tafsiri na utaona katika ramani ya biblia yako jina la mto Yordani halijafanyiwa

tafsiri, mto Nile, Tigris, Euphrates na mingineyo imebakia na jina asilia. Jina la

mto au jina la nchi, jina la mtu au mlima haliwezi kufanyiwa tafsiri lakini kwa

hawa ndugu wakristo katika Biblia yao majina ya watu yamefanyiwa tafsiri eti

Yesu ni Kiswahili na Jesus ni Kizungu lakini lugha yake ya asili usiijue?

Wengi hawajui kuwa jina “Issa” ni jina la ki israeli na kama waeza kufuatilia hebu

tafuta maana na namna jina hili linavyosomwa “ESSAU” na sina shaka utafahamu

Kwa sababu ya kudumisha utengano na maelewano, sote twajua kuwa “Issa”

ndiye huyo “Yesu” kama vile mkate ndio “Bread”

Quran na Biblia zimetuonyesha kuwa Mama Maryamu a.s. alizaa mtoto wa

kiume aliyetahiriwa siku ya nne kama ilivyo desturi ambaye alitukuzwa mno na

Mola s.w.t.

1. Quran 3:45 – Malaika waliotumwa kwa Mama Maryam.

2. Luka 1:26 – Mwezi wa sita Malaika Gabriel alitumwa kwa Maryam.

3. Quran 3:47 – Maryam ni Bikra hajui Mume.

4. Luka 1:34 – Maryam ni bikra hajui mume.

Quran inamtambua Yesu kuwa ni mwana wa Maryam sawa na andiko la Biblia,

sasa vipi mtu aseme Yesu na Issa ni tofauti?

1. Quran 3:45 – Jina lake ni Issa mwana wa Maryam.

2. Marko 6:3 – Yesu, mwana wa Maryam.

Kuna katika wakristo wanaodhani kuwa kwa mujibu wa Quran mwana wa

Maryam hakufanya miujiza na wakawadanganya wakristo hivyo lakini Quran

yaonyesha baadhi ya miujiza yake japokuwa wanadamu hawataki kuukubali

1. Quran 3:49 – Isa mwana wa Maryam aliwaponya baadhi ya vipofu, wenye

ukoma, na kufufua baadhi ya waliokufa kwa idhni ya Mwenyezi Mungu.

2. Yohana 11:38 – 44 – yesu amuomba Mwenyezi Mungu amfufue lazaro ili

wale wa Izraeli wajue kuwa Yesu alitumwa na Mungu. Kando na kumfufua

Lazaro, aliwaponya viwete, vipofu, mabubu n.k.

Ili kutukinga na shirki, Quran ikatuonyesha kuwa mfano wake Yesu ni kama Adam

a.s. wote waliumbwa kwa udongo na Mola s.w.t na hawastahiki kuabudiwa kwa

vyovyote na yeyote.

1. Quran 3:59 – Issa ana asili kutokana na Adam.

2. Mathayo 26:64 – Yesu ni mwana wa Adam.

3. Mathayo 19:27 – Yesu ni mwana wa Adam.

Kihakika ni masikitiko kwa baadhi ya wakristo kudai leo eti wa Izraeli hawamjui

Yesu ilhali Maryam aliyemzaa ametokana na wana wa Izraeli. Sasa wewe mkenya

utamjua Yesu kulikoni mama yake?

1. Quran 3:49 – Issa ni mtume kwa wana wa Izraeli tu.

2. Quran 61:6 – Issa ni mtume kwa wa izraeli tu.

3. Mathayo 10:5 – Yesu atuma wanafunzi wake kwa kabila za wa Izraeli.

4. Mathayo 10:23 – Wao wanafunzi hawataimaliza miji ya Izraeli

5. Mathayo 15:21 – 26 – Yesu ametumwa kwa wa Izraeli pekee.

6. Matendo 2:22 – Yesu amedhihirishwa kwenu (Waizraeli) na Mungu.

7. Matendo 5:31 – Yesu ameleta toba kwa waizraeli tu.

8. Matendo 11:19 – wanafunzi walifundisha habari za Yesu kwa waizraeli tu.

9. Yohana 17:9 – Yesu anawaombea hao, haombei ulimwengu.

Kama “Issa”, “Yesu” naye hawezi kuokoa na hajui siku ya Qiyama na hawezi

kufanya lolote ila aamriwe na Mungu.

1. Quran 31:34 – habari za kiama ni zake Mola tu.

2. Taurati 32:39 – Mwenyezi Mungu tu ndiye anayeokoa.

3. Yohana 5:30 – Yesu hawezi kufanya lolote ila aamriwe.

4. Mathayo 20:20 – Yesu asema uzima wa milele watapewa waliowekewa

tayari na Mola.

5. Yohana 14:28 – Mungu ni mkuu kuliko Yesu mwana wa Maryam.

Quran imesimama msimamo mmoja na ndio mwafaka wa jamhuri ya Maulamaa

kuwa mwana wa Maryam hakufa msalabani.

1. Quran 4:157 – hakufa msalabani, ila wao wanafuata dhana.

Ikiwa Yesu alikufa msalabani na ndiye Mungu wa baadhi ya wakristo basi

yasikitisha kwa kuwa yaonyesha udhaifu wa Mungu huyu hata auwawe na viumbe

vyake. Kwa hakika maandiko ya Biblia yameachana sana kuhusu kifo cha Yesu

msalabani na ni vigumu kwetu kuamini na mifano ni mingi tu: –

1. Mathayo 27:27 – Yesu kavishwa vazi jekundu.

2. Marko 15:16 – Yesu kavishwa vazi la rangi ya zambarau.

3. Marko 15:25 – saa tatu asubuhi Yesu amesulubiwa.

4. Yohana 19:14 – Saa sita Yesu yuko mahakamani.

5. Mathayo 27:3 – 5: Je Yuda alijinyonga?

6. Matendo 1:18 – 20: Au Yuda alianguka akapasuka tumbo?

Ikiwa wafuasi wa Yesu ni wakristo (Christians) Je Yesu mwenyewe alikuwa na dini

gani na je jina la mtu laweza kuwa dini ya watu?

1. Quran 61:14 – Mtume Issa alikuwa na wanafunzi wake.

2. Mathayo 10:2 – Majina ya wanafunzi wa Yesu.

Kama ni kweli kuwa Yesu aliyezaliwa na Maryam ni Mungu na kuwa anao ndugu

zake kama munavyotuonyesha basi mna bahati kuwa mungu mwenye ndugu na

ukoo. Sisi waislamu hatuna.

Mathayo 1:1

Uislamu umetuonyesha kuwa baada ya kumzaa “Issa”, Maryam hakuolewa,

hakuingiliwa na mtu yeyote hadi alipokufa, yaani ndiye mwanamke pekee aliyezaa

pasina kuingiliwa na akafa bila kuingiliwa.

Yesu alifundisha njia ya Mungu akisema “utuongoze katika njia iliyonyooka.”

1. Mathayo 6:9

2. Luka 20:21

Kasema kuwa kuna utatu ni kumtukana Mola, ni kumtukana Nabii Yesu, Yesu ni

mtume tu.

1. Yohana 17:3

2. Yohana 5:30

3. Yohana 7:16 – 18

4. Marko 12:28 – 31

5. Mathayo 4:10 – “Huo utatu watoka wapi hali Yesu mwenyewe

alimuabudu Mola, vipi wewe unamuabudu Yesu na udai kuwa Nabii Isaya

alihakikisha, hali Isaya alisema “tumepewa mtoto mwanamume” vipi

Mungu awe mtoto tena wa “kiume” kumbuka kuwa Mola hana mfano

wowote.

Yesu mwenyewe alisema waache wafu wazike wafu wao, tena angoje wafe ili

awahubirie, kuongea na wafu huu si ushetani!utafute jina Issa kwa Biblia na hao

waandishi wa biblia wamesema katika dibaji ya union version 1952 kuwa:-

…Hio kazi yenyewe haikuwa rahisi. Matumizi mbali mbali yametokea katika

Janibu mbali mbali za nchi hii. Kwa mfano ilikuwa hapana budi kufikiri kwamba

hilo jina la Mungu katika agano la kale litaandikwa “Jehova Mwenyezi Mungu

au Bwana Mungu…pia maendelezo ya majina yote ya watu nay a mahali ilikuwa

lazima yafikiriwe tena na mengine kutengenezwa. Jambo hili lilikuwa kazi

kubwa sana kwa sababu yako majina zaidi 3500. Tena jina la kitabu chenyewe

lilifikiriwa, kama kiitwe “Maagano mapya” au agano jipya.

Ndugu msomaji, bado wataka kuona neno “Issa” katika Biblia? Hizi ndizo taratibu

ya Iman kama ilivyoeleza Quran:

“Hiki ni kitabu kisichokuwa na shaka ndani yake, ni muongozo kwa wacha

Mungu ambao huyaamini mambo ya ghaib na hudumisha sala na hutoa katika

vile tulivyowapa.” (TMQ 2:2 – 3)

Naye Yesu akasema:

“si kila mtu aniambiaye Bwana, bwana, atakayeingia katika ufalme wa

mbinguni, bali ni Yule afanyaye mapenzi ya baba yangu aliye mbinguni.”

(Mathayo 7:21)

Amua, utamuita “Yesu simba” au utafanya mapenzi ya Mungu?

Imetayarishwa na

Adam Ambetsa

Tel No: 0723 – 174 154

Mombasa.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.