0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MAJIBU KWA BWANA FONDO NA WASABATO KWA JUMLA JE NI UPI MWONGOZO WA KWELI, BIBLIA AU QUR’ANI?

MAJIBU KWA BWANA FONDO NA WASABATO KWA JUMLA

Bwana Fondo, kijana wa kisabato [SDA] anapenda sana aitwe “Ustadh”, na ndivyo wanavyotaka wahubiri wote wa kisabato, lakini ni mapenzi tu wala haimgeuzi kuwa anavyotaka kwa kuwa mtume [Rehma na amani ziwe juu yake] asema Imani haiji kwa kutamani. Hatujapenda sana kuwajibu hoja zao zisizo kuwa na kichwa wala maguu, lakini kwa hili tutajaribu kuuzuia huu utapeli wa maandiko yake ili apate muradi wake. Hatuzuii haki yako kupata riziki, lakini ziwe ni za halali.

Katika kijitabu alichoandika kina mada tano kimsingi, na zote amezipinda ili zimfae binafsi, na kuwapotosha wanaokisoma hali hawana ujuzi, mada hizo ni:-

1. JE NI UPI MWONGOZO WA KWELI, BIBLIA AU QURAAN.
2. JE UANA WA YESU UNAOKOA.
3. JE YESU ALIKUFA MSALABANI.
4. JE NANI MWOKOZI WA ULIMWENGU MZIMA, MOHAMMAD[SAW] AU YESU.
5. JE NI IPI NJIA YA KWELI YA UZIMA, UKRISTO AU UISLAMU.
Tutajaribu kuiangazia kila mada kwa undani kidogo kwa kutoa baadhi ya maandiko ambayo Bwana Fondo hakutaka ujue kwa sababu zake, lakini ndugu msomaji yafaa ujue agano la mwisho, Qur’ani ilikwisha twambia ukweli umeshafika na uwongo lazima utoweke [Quraan 17:81], na sina shaka kuwa hata yeye mwenyewe ajua hayo aliyoyaandika si kweli.
Mada yake ya kwanza ni, JE NI UPI MWONGOZO WA KWELI, BIBLIA AU QUR’ANi?

Kosa lake la kwanza ni kule kujifanya kuweza kusoma anavyofikiri Muislam, na kuzua uwongo unaoendelezwa kuwa Waislamu hawakusoma, kwa hivyo hujipangia mambo bila dalili maalum kutoka kwa Allah [Subhana wata’ala], hii si kweli, bali kinyume chake Uislamu ndio Dini pekee duniani ambayo ambayo viongozi wake wamesoma na kumjua ALLAH [Alayhi Salaam] namna inavyotakiwa , na hawatowi hutuba zao ila zina ushahidi kamili wa Qur’ani na Hadith za Mtume [Rehma na amani zimfikie yeye], kinyume na madini mengine ambayo viongozi wake hudai eti wamefunuliwa na kufungua majumba ya ibaada!.

Hakuna ushahidi wowote kuwa Mwenyezi Mungu aliteremsha au kumfunulia Nabii yeyote kitabu kiitwacho BIBLIA, na wala Waislam hatusemi kamwe kama anavyodai Fondo, kuwa ni BIBI-LIA, bali twajua kihakika kuwa Mola Muumba aliteremsha Tourati kwa Nabii Musa [Alayhi Salaam], Zaburi kwa Nabii Daud [Alayhi Salaam], Injeel kwa Yesu [Alayhi Salaam] mwana wa Maryam na Qur’ani kwa Mtume Muhammad [Rehma na amani ziwe juu yake]. Haya maelezo ya Biblia yanayotolewa na bwana huyu yana mkanganya yeye mwenyewe. Neon Biblia asili ya kigiriki, BIBLOS, na maana yake ni Mkusanyiko wa vitabu, hapa lazima tuzingatie mno kuwa haikuja ‘ mkusanyiko wa vitabu vya Mola’, na kwake kujaribu kunukuu maandishi ya Biblia ya Union Version iliyoandikwa 1952, eti maandiko ya Mungu yaitwayo Biblia yaliyongezewa na waandishi kujaribu kuziba mapengo na mapungufu katika kitabu hicho chao ni uwongo wa ajabu.

Kwa wale wanaokikubali kitabu cha Biblia kuwa kitakatifu, ilikuwaje wagiriki ambao kiasili ni mapagani wawe ndio watakipeni jina kitabu chenu?, hakuna nabii mgiriki, kwanini Biblia ya kwanza iwe ni ya kigiriki?, unaposema eti Mungu aliwapa wakristu kitabu kilichokusanya vitabu manabii walio tangulia ni mawazo tasa, na ya uvunjivu mkubwa wa Haki yake Mwenyezi Mungu, na sina shaka kesho ataulizwa ni Nabii yupi aliye pewa kitabu cha Biblia?. Aya aliyoitoa ya Qur’ani 2:121 yasema hivi, ‘ wale katika ahlul kitabu, tuliyo wapa kitabu, tourat, Zaburi na Injeel, wakakisoma kama ipasavyo kukisoma bila ya kupotoa tafsiri, kwa kuongeza hili au kupunguza hili hao huiamini hii Qurani wakasilimu’, lakini Fondo kaamua kucheza na akili za wasabato kwa kujivika kofia ya UANDISHI, kumbe katu hayumo.

Qur’ani haikuja kijanja, na kamwe haifai kutumiwa kijanja. Waislam sote tumelazimishwa kuwakubali Manabii wote aliyo wataja Allah Sub’hanahu Wat’ala katika aya kadhaa za Qur’ani, mfano [2:136,]

[Semeni nyinyi: Tumemuamini Mwenyezi Mungu na yale tuliyo teremshiwa sisi, na yaliyo teremshwa kwa Ibrahim na Ismail na Is-hak na Yaakub na wajukuu zake, na waliyo pewa Musa na Isa, na pia waliyo pewa Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi; hatutafautishi baina ya yeyote katika hao, na sisi tumesilimu kwake.]

na [3:84]

[Sema: Tumemuamini Mwenyezi Mungu, na tuliyo teremshiwa sisi, na aliyo teremshiwa Ibrahim, na Ismail, na Is-haak na Yaakub na wajukuu zao, na aliyo pewa Musa na Isa na Manabii wengine kutoka kwa Mola wao Mlezi. Hatubagui baina yao hata mmoja, na sisi ni wenye kusilimu kwake]

na zingine nyingi zinazowaamuru waislam kuwapa heshima na kuwahami Manabii wote waliotajwa.

Ibraheem [Alahi salaam] hakuwa myahoodi wala mkristu bali alikuwa mwongofu mtii wala hakuwa miongoni mwa washirikina, Waislamu tunamtambua kama Baba wa Mitume na Baba wa Imani, na wanawe wawili Nabii Ismail [Alahi salaam], na Nabii Isaack [Alahi salaam] ambao wote Allah [Subhana wata’ala] aliwajaalia kuwa Manabii watukufu. Kasha kuna Nabii Yakoob [Alahi salaam] na kizazi chake [Banu Israel], na aliyopewa Nabii Musa [Alahi salaam], na Issa Yesu [Alahi salaam] Mwana wa Maryam ambao ni ujumbe mtukufu kwa wana wa Israeli tu wala si kwa watu wengine [ambao ni watu wa mataifa wasiyo tahiri].

Anapouliza ndugu yetu Fondo, nani walioandika Biblia, kisha akatoa andiko la kutoka 31:18, torati iliandikwa na chanda cha Mungu, na hapo hapo akageuza hapo ili kuleta dhana kuwa mwandishi wa biblia ni Mungu ni kumsingizia Mola uwongo, tena uliyo dhahiri, na mwanadamu aliye fikia kiwango cha kusema uwongo juu ya Mwenyezi Mungu huwa kavuka mipaka yote, na ameanzisha vita na Mola wake nasi hatuna shaka kuwa atashindwa vibaya sana .

jambo linguine la kudhibitisha alikuwa hamaanishi kwa yale aliyo andika , ni matumizi ya N/B. Hii inampa nafasi ya kuongeza au kupunguza yale atakayo ili apate muradi wake. Waislamu twajua kuwa asili ya ilmu zote ni Allah [Subhana wata’ala], kama alivyo sema mwenyewe katika Qur’ani  [96:1-5,]

[Soma kwa jina la Mola wako Mlezi aliye umba,Amemuumba binaadamu kwa tone la damu, Soma! Na Mola wako Mlezi ni Karimu kushinda wote!Ambaye amefundisha kwa kalamu.Kamfundisha mtu aliyo kuwa hayajui.]

na katika ilmu hizi zote ni za uhakika, lakini pindi mwanadamu atakapo kuanzisha kidini chake au kujitukuza mwenyewe, basi aya zote hizi huzigeuza sharubati ili apate utamu wa dunia,atambuliwe, apate cheo kuwa huyu ndiye mpinzani mkuu wa Mola, lakini angalia mwisho wa Firaun [aliye laaniwa].

Kile Fondo anawaficha wasabato wenzake na wakristu kwa jumla ni kuwa Biblia ina mamia ya waandishi walioiandika zama hizo, kama vile Luka aliyekuwa mganga [upo ushahidi wa biblia ya Imprimatur Bible], Paulo [zamani akiitwa saulo] aliyeandika nyaraka nyingi mno katika biblia, [filemoni 1:19] , na hata lile koti [joho] alilolisahau huko troa akaomba aletewe, na bado yakaitwa ‘ maandiko matakatifu ya mungu yaitwayo biblia’. Kufikia hapa napenda kusizitiza kuwa Biblia ni kitabu yatima kisichokuwa na Mtume au Nabii, sasa lazima kila atakaye kuwa wakili wa Biblia awe na Kanisa lake au Imani tofauti na wale wengine, mfano wengine ni jumamosi, na wengine jumapili. Wengine husema Yesu [Alahi salaam] mwana wa maryam ni mungu, na wengine husema mwana wa mungu au ni mungu tena ni mwana wa mungu!.

Sote ni viumbe vya Allah [Subhanahu Wata’ala], naye ametuweka katika daraja mbali mbali kwa kadiri ya uchaji Mola wako na ushahidi ni Qur’ani 49:13, ‘ .[Mmbora wenu ni Yule anaye mcha Mola’.] Katika hawa wanadamu Allah [Subhana wata’ala] aliwachagua Manabii watakao pewa ujumbe wake ili wawapelekee watu waliotimilizwa kwao, na hao Manabii anao wataja Amos, Ezekiel, Daniel,Samuel, Daudi, Yeremia, Isaiah, Yesu [Alahi salaam] mwana wa maryam, n.k, wote walitumwa kwa wana wa Israeli tu, na hata kama waliandika kama anavyodai basi ujumbe wao bado ni kwa wana wa Israeli tu.

Kudai kuwa Nabii Musa [Alahi salaam] aliandika vitabu vitano vya kwanza katika Biblia , mwanzo, kutoka, walawi, hesabu na kumbukumbu la torati, si kweli kwa sababu katika kumbukumbu Musa [Alahi salaam] anakufa lakini bado anasimulia maziko yake, jambo ambalo haliwezekani kamwe. Ndugu Fondo amka, toka usingizini, kumekucha watu wanasoma, watu wanasilimu hata ndugu zako!. Suhufi kwa kiarabu ni nyaraka, na kwa fondo na wasabato yafaa mjue kuwa Nabii Musa [Alahi salaam] anao utumishi mara mbili, kwanza kwa Firaun aliyejiita mungu Qur’ani [53:36, ] na pili ni Tourati kwa Wana wa Israel, Qur’ani [5:45,]  [11:110 ], na sina shaka Fondo nimjuae si katika wana wa Israel!.

Waislam hatusemi, kwa nini Qur’ani iliandikwa, bali twasema , ipi hekima ya Allah [Subhanahu wata’ala] kuifunua Qur’ani, hii ni kwa sababu Mtume [Rehma na amani ziwe juu yake ] alikuwa hajui kusoma wala kuandika, [Quraan 7:157]

[Ambao kwamba wanamfuata huyo Mtume, Nabii, asiye soma wala kuandika, wanaye mkuta kaandikwa kwao katika Taurati na Injili, anaye waamrisha mema na anawakanya maovu, na anawahalalishia vizuri, na ana waharimishia viovu, na anawaondolea mizigo yao na minyororo iliyo kuwa juu yao.].

Wakristu walipoweka fikra hii ya “ kuiandika Biblia ”, haikukoma bali wanaendelea kuikarabati hata leo, nayeye Fondo ajua kwa uzuri kuwa takriban kila kanisa lina Biblia yake tena kwa faida yake tu, na ajabu ni licha ya wao wenyewe kuandika Biblia yao bado hawaiamini kamwe na ni sababu ya Nabii Yesu [Alayhi salaam] mwana wa maryam alipowaambia ‘ kusikia mtasikia wala hamtaelewa ‘, kwa sababu mioyo imesusuwaa, kila mmoja kwa faida yake.

Luka mmoja katika waandishi wa Bibli asema katika utangulizi wake ambao baadhi ya wasomi wa kikristu wanapenda sana kuyahariri asema katika utunzi wake kwa Mfalme Theofilo, “ kwa kuwa watu wengi wametia mikono kutunga kwa taratibu habari ya mambo yale yaliyo timizwa katikati yetu kama walivyo tuhadithia wale waliokuwa mashahidi wenye kuyaona, na watumishi wa lile neon tokea hapo mwanzo, nimeona vema name kwa kuwa nimejitafutia usahihi wa mambo hayo yote tangu mwanzo kukuandikia kwa taratibu, Theofilo mtukufu “.

Haya maneno ya kutunga yaweza kuwa ya Mola?, na vipi utayalinganisha na Qur’ani Tukufu ambayo ndio ufunuo wa mwisho kwa wanadamu wote, Qur’ani ndicho kitabu pekee kilicho bakia katika asili yake, na leo twaisoma kama alivyo isoma Mtume Muhammad [Rehma na amani ziwe juu yake ] kinyume na Biblia yenye ‘Versions’ mbali mbali, Qur’ani pekee ndio iliyosimamisha ujumbe wa Tawheed, yaani kumtukuza Mwenyezi Mungu Mmoja tena wa pekee, kinyume na Biblia inayotangaza miungu mitatu [utatu mtakatifu], ni Qur’ani pekee inayo wahimiza Waislam kuwaheshimu na kuwahami Manabii wote, kinyume na biblia inayo wabagua ,kuwasuta na kuwatukana Manabii watukufu na twasema bila uwoga kuwa Qur’ani ni muujiza wa kuendelea tunaoishi nao, na Allah [Subhana wata’ala] Mwenyewe ameapa kuilinda kutokana vitimbi vya akina Fondo na wenzake.

Allah [Subhana wata’ala] ndiye aliyekamilika kwa sifa zote zilizo kamili, kinyume na huyu Mungu ambaye Fondo anamtembeza kwenye kikapu, aliyezaliwa, ana mama mzazi, alikula samaki wa kupaka, alilipa kodi, alilala usingizi, alipigwa makofi, aliuwawa, kasha akadai kufufuka. Allah [Subhana wata’ala] ana uhai wa maisha, ni mjuzi yote yaliyo mbinguni na ardhini, kusinzia hakumshiki wala kulala, hali, ndiye mtoaji Riziki na kwa ufupi amekamilika kwa sifa zote zilizotakasika.

Pope John Paul II, aliandika kitabu “ crossing The Threshold “ mwaka 2000, na ndani yake akawa analalamika na kuona ghere kuwa kila sifa njema zote amepewa Mola wa Waislam!.

Waandishi wa Biblia walilenga kukutoa katika njia sahihi ya Allah [Subhana wata’ala], na kukutumbukiza kanisani, na haya yanadhibitishwa na Paulo anaye shuhudia kuwa alifanya mambo mengi yaliyo pingamana na jina lake Yesu [Alahi Salaam] mnazarethi, ‘ kweli mimi mwenyewe naliona ndani ya nafsi yangu kwamba yanipasa kutenda mambo mengi yaliyopingamana na jina lake Yesu……..’, naam Paulo aliwaita wafuasi wake waende kanisani kinyume na Nabii Yesu [Alahi Salaam] mwana wa maryam aliyehubiri katika masinagogi [misikiti ya wayahoodi], matendo 26:9, luka 4:44, na ushahidi ni katika I wakorintho 4:14-17, ‘ basi nawasihi mnifuate mimi. Kwa sababu hii nimemtuma Timotheo kwenu, aliye mwanangu mpendwa………. Atakaye wafundisha njia zangu…….. kama vile nifundishavyo kila mahali katika kila kanisa.’

Kwa nini Fondo husemi ukweli huu kwa wakristu ili waujue ukweli, kwa nini unaificha kweli hali unaijua?, mtu wa Mungu aweza kukamilika anapo someshwa na kuambiwa uwongo?, kwa nini wabadilisha maandiko kwa manufaa ya kibinasfi?, kesho mbele za Mola Mwenyezi utasema nini?. Nabii Issa Yesu [Alayhi Salaam] mwana wa maryam alipewa kitabu cha Injeel [ kimoja sio vinne], na sisi hatuna shaka kwa hilo, kwako kutumia janja kwa kunukuu mathayo 5:17-18, kasha ukafikiri wajenga hoja ya biblia ni maneno ya kusikitisha.

Tourat, Zaburi na Injeel, viliharibiwa na waandishi kama wewe Fondo. Yesu [Alayhi Salaam] mwana wa maryam alimwabudu Mola mmoja kama ilivyosema Tourat, na akawa mwenye kumsujudia Mola, Mathayo 4:10, Marko 12:28-30. Kwanini wawafundisha wakristu na wasabato kumuabudu Yesu [Alayhi Salaam] mwana wa maryam, na kupiga magoti badala ya kusujudu?, je hujaliona andiko hili katika Ufunuo 22:9 “ na wale washikao maneno ya kitabu hiki MSUJUDIE MUNGU”.

Fondo wachekesha, kusema Biblia itadumu mpaka lini. Leo kuna Biblia za Anglican zina vitabu 66,za Roman Catholic zina vitabu 73,za Orthodox zina vitabu kati ya 76 na 84, sasa ipi katika hizi Biblia itadumu milele?, naona kiu kikubwa kwa wakristu na wasabato tafadhali waambie ukweli, lau sivyo utaulizwa na Mola na sijui utamwambia nini.

Kama Waislamu, kila tunapopata nafasi ya kueleza ukweli, kamwe hatutumii Biblia kwa sababu si kitabu cha Mola, japo kuwa kuna baadhi ya maneno yaliyo salimika wakati huo na sijui kama safari hii yatasalimika. Qur’ani 5:44, Allah [Subhanahu wata’ala] alimfunulia Nabii Musa [Alayhi Salaam] kitabu cha Tourat ili kiwe mwongozo kwa wana wa Israel, na walitakiwa wakihifadhi kitabu hicho ili kiwahukumu kwa kila jambo, lakini kikaharibiwa [Qur’ani 11:110] na hao wafuasi wake kwa uzushi wao.

Uzushi ni jambo nzito mno na laweza kuwapoteza wengi na mifano tunayo.

Bwana Fondo anapo sema na kutangaza kuwa Yesu [Alayhi Salaam] ndiye anayestahili kuabudiwa, ni uzushi mkubwa. Kuharibiwa kwa Tourat hakukutoa nafasi ya kutunga kitabu kingine “ Kumbukumbu la Tourat “ ambacho ni tofauti kabisa na “ Tourat “ aliyopewa Nabii Musa [Alayhi Salaam]. Sio hoja kama Biblia inakubali au haikubali, ukweli ni kwamba waandishi wa Biblia wanaafiki ukweli wa Qur’ani kuwa Tourat aliyopewa Nabii Musa [Alayhi Salaam] “ imekuwa REPLACED” na kumbukumbu la tourat.

NIV study Bible, katika kuto sherehe juu ya Zaburi, wanasema kuwa huenda kuna ukweli kidogo kuwa Nabii Daudi [Alayhi Salaam] aliandika sehemu ya Zaburi hadi sura ya sabini na nane [78], lakini kuanzia sura ys sabini na tisa [79] mwandishi wake hajulikani, na ndio sababu Muislam halazimishwi kuyaamini maandiko ya Biblia, maandiko ambayo ya mtukana Nabii Daudi [Alayhi Salaam] kuwa alikuwa mzinifi [subhana llah], na wengine wenye tama ya utajiri wakajifanya watunzi wa nyimbo za Injeel, kama Daudi alivyokuwa akiimba.

Fondo asema kihakika kuwa Yesu [Alayhi Salaam] mwana wa maryam alipewa Injeel, na SI mathayo, marko, luka wala yohana, [Qur’ani 5:46,]  [Qur’ani 57:27,] lakini wakaivuruga matokeo yake leo ni kutoaminiana na kuchanganyikiwa kwa wakristu na kama Paulo alivyo wapata wakristo kwa hila, IIwakorintho 12:16, na Fondo naye anaazimia hilo! Hatuwezi kulinganisha hata kidogo mfumo wa Qur’ani na ule uliofidiwa kwenye Biblia. Yashangaza kuwa na makosa yote pamoja na udhaifu bado Fondo aweza andika mwisho mada hii kuwa japo biblia imeonyesha kuwa mungu atafanya ukahaba, Isaya 23:17, na kuwa Mola alimdanganya Nabii Yeremiah 4:10 na mengi eti bado biblia ina mwongozo sahihi kwa wanaadam!.

IMETAYARISHWA NA :
ADAM AMBETSA
MWEMBE TAYARI TABLIGH GROUP
MOBILE NO. 0723 17 41 54
MOMBASA, KENYA.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.