0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

FONDO AJIBIWA JE UANA WA YESU UNAOKOA?

JE UANA WA YESU UNAOKOA?

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameeleza katika Qur’ani kuwa asili ya itikadi kuwa Mola ana mwana ni itikadi ya wayahood wakadai kuwa Uzair ni mwana wa Mwenyezi Mungu.

[Na Mayahudi wanasema: Uzeir ni mwana wa Mungu. Na Wakristo wanasema: Masihi ni mwana wa Mungu. Hiyo ndiyo kauli yao kwa vinywa vyao. Wanayaiga maneno ya walio kufuru kabla yao.

Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!]

[Quraan 9:30].

Katika Quraan 2:116, Mwenyezi Mungu Mtukufu anawarudi mayahoodi na wakristu kwa madai yao kuwa Allah Subhanahu wata’ala  ana mwana akasema:

[Na ati wanasema: Mwenyezi Mungu ana mwana. Subhanahu! Ametakasika na hayo. Bali vyote viliomo mbinguni na duniani ni vyake. Vyote vinamt’ii Yeye.]

Huu ni ushirikina mkubwa , kila unachokiona na usichokiona vyote vina mtii Yeye kwa unyenyekevu, na Mtume Rehma na amani zimfikie yeye akasema kupitia hadith aliyoieleza ibn Abbas, kuwa Allah Mtukufu amesema Mwana wa Adam anasema uwongo dhidi yangu, japo hana haki kufanya hivyo, ananitukana Yakuwa hana haki ya kufanya hivyo. Kwa kusema uwongo dhidi yangu husema kuwa siwezi kumuumba tena alivyokuwa baada ya kufa, na kwa kunitukana ni kule kuwa nina mwana, la ametukuka! Hana mke au mwana’

Napenda sana kuwajulisha wasabato na wakristu kwa jumla kuwa usitafute sababu yoyote ili Mola awe na mwana, huo ni upagani ulio wazi, na moja katika sababu kubwa ya Allah Subhanahu wata’ala kuiteremsha Qur’ani ni kuwaonya wale wanaodai Mola ana mwana wao hawana ilmu au baba zao na hawasemi ila uwongo, na fondo ni mmoja wao, Qur’ani 18:4-5. Kwa nini kujisumbua kama uana uutakao wewe ni wa kizazi au heshima. Kwa Allah Subhanahu wata’ala sote ni viumbe vyake tu [Isaya 44:24], Fondo wajisumbua sana eti ALIYEZALIWA na mungu hatendi dhambi. Malaika wote hawatendi dhambi na wala hawajaitwa watoto wa mungu. Usiweke vigezo vya kutafuta muradi wako. Kwamba Yesu Alayhi salaam mwana wa maryam ni mtakatifu siyo hoja haswa kwa wakristo kwa kuwa Mathayo,Marko,Luka na Yohana wote ni watakatifu, na Pope pia ni mtakatifu!.

Bwana Fondo anafanya ubaguzi, Daudi Alayhi salaam aliongea kwa uwezo wa roho mtakatifu na hakuitwa mwana wa mungu, na kuhusu ushahidi Mola ni shahidi tosha wala hatuhitaji mwingine, na juu ya hayo na watu watakao dai madai kama ya Fondo watakuwa wamefeli, na kujiingiza katika ushirikina ulio wazi.

Katika utafiti ambao tumefanya unatuonyesha kuwa Yesu Alayhi salaam mwana wa maryam alijiita mwana wa Adam mara themanini na tatu [83], lakini kaitwa mwana wa mungu na hawa wapotofu mara ishirini na nne [24] tu!. Jee una lengo lipi kama huwezi waambia wafuasi ukweli huu?.

Kwa wasomi wa Qur’ani, mtagundua kuwa Mwanamke aliyetajwa kwa jina katika aya za Qur’an, ni mwanamke mmoja tu nae ni  Maryam binti Imran, soma katika  sura ya kumi na tisa [19].

Mama huyu Allah Mtukufu kamtaja kwa jina na kumueleza kwa undani kwa sababu ndiye alomzaa Nabii Issa Alahyi salaam (Yesu) mwana wa Maryam ambaye baadhi ya wakristu wamemuita Mwana wa Mungu, na wengine kudai ndiye Mungu haswa!. Sisi kamwe hatujengi hoja kwa sura ya Qur’ani 112:1-3, kwa kuwa muradi wa aya ni Tawheed yaani kumpwekesha Mola, kumtakasa, cheo chake,uwezo wake ,utajiri, uumbaji wake na kuwa hakuna mwenginewe ila Allah Mtukufu, na haya ni majibu yake Allah Subhanahu wa Ta’ala kwa wale waliotaka kujua hakika ya mambo.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ni muumba, na sifa ya kuza ni ya majini, wanadamu na wanyama Mwenyezi Mungu mtukufu amekamilika kwa hali ya kipekee.

Fondo na baadhi ya wakristu wanashangaa kwa nini mbingu hazitatuki, na milima kuwa kama sufi kama ilivyoeleza Qur’ani, ukweli ni kwamba Rehma za Allah zimetangulia Hasira zake, na waswahili walishasema ‘ aulizae atapata ‘. Kwa kudai madai haya Fondo amedhihirisha ukafiri wake, na Maana haswa ya ukafiri ni kukanusha haki,kuficha haki na kuikataa haki. Kufanya kibri kwa maneno yake Allah Subhanahu Wata’al, ni hatari kubwa sana ambayo Fondo na wakristu wenzake wanafanya, na ni fikra za kijahiliya na ni dalili ya kutokuwa na ilmu kwake na babu zake na ni upotofu uliodhahiri.

Allah Subhanahu Wata’ala, ametuonya sana kuepukana na uzushi, na kama angekuwa na mwana angelibainisha katika vitabu, na Manabii wala asingetuacha kuwauliza wasiokuwa na ilmu kama ndugu zetu.

Kwamba Nabii Isaa Alayhi salaam (Yesu) Mwana wa Maryam hana Baba, haimfanyi awe mwana wa mungu au mungu, na kuwa fikra au imani hiyo ni upotofu na hauna faida yoyote ikiwa mja hatamwabudu Mwenyezi Mungu Mtukufu kama ilivyonukuliwa katika Mathayo 4:10, Yohana 14:1-, na Yohana 17:3. Jambo la pili ni kuwauliza ndugu wakristu, Nabii Adam Alayhi salaam hana baba wala mama, lakini hajaitwa mwana wa mungu au mungu, na ndio twasema kuwa hao wanaotangaza upotofu huu ni lengo la kufaidika kibinafsi, wala sio kuelekeza watu katika uzima wa milele.

Ni makosa kwa Bwana Fondo kutumia janja kugeuza au kuficha mashetani wanao kizazi kwa kuwa wanazaana, Allah Subhanahu wa Ta’ala ni muumba na hana watoto, lakini kwa bwana Fondo ili afikie faida yake ya binafsi lazima ageuze aya ya Qur’aan 2:116, anapodai kuwa Qur’ani inakubaliana na fikra hii ya kijahiliya.

Katika Kumbukumbu La Tourat 32:39-40, Mola anajitukuza mwenyewe kuwa ndiye anayeuua na ndiye pekee anayeweza kuweka hai, ndiye anayejeruhi na kuponya na pekee tu ndiye MWOKOZI, leo kwa bwana huyu kudai kuwa uana wa Yesu Mwana wa Maryam unaokoa ni wazi haelewi anachozungumzia, na cha maana kwake ni apate muradi wake tu.

IMETAYARISHWA NA :
ADAM AMBETSA
MWEMBE TAYARI TABLIGH GROUP
MOBILE NO. 0723 17 41 54
MOMBASA, KENYA.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.