0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

JE YESU NDIYE MUNGU MUUMBA?

JE YESU NDIYE MUNGU MUUMBA?

Huu ni ukweli ambayo wakristu wengi wanajitahidi kuficha, kwamba kuna mpasuko mkubwa baina ya wakristu,sehemu ya hawa wanao jiita walokole hudai kwa akili zao kuwa Yesu mwana wa Mariam ndiye anayestahiki kuabudiwa, hali ACK, JEHOVA WITNESS hawakubali kamwe na maandiko yote yanasadikisha hayo.

Mamlaka yote aliyokuwa nayo YESU mwana wa Mariam alikuwa amepewa na Mola Muumba, na kila aliye pewa mamlaka kuna aliye juu yake. Wakristu wengi wanaamini kuwa Yesu mwana wa Mariam alihukumiwa na Pilato ili afe kifo cha msalaba, swali ndogo tu, vipi kiumbe kimhukumu muumba wake?, inakuwaje Mola mwenye uwezo wote awe atakufa kifo cha laana?. Ushahidi katika biblia watuonyesha kuwa Yesu mwana wa Mariam alikuwa Nabii Mteule, na hilo hakuna shaka, na kwa ushahidi ndugu wakristu yafaa wasome maandik yafuatayo:
1. Luka 1:26
2. Quraan 5:45
3. Yohana 5:45
4. Yohana 17:3,6
5. Yohana 14:24,28
Niukweli usiyofichika kwamba Nabii Yesu mwana wa Mariam alifanya miujiza mingi zama zake kwa uwezo wa Allah[swt], na yafaa tu wewe ndugu mkristu usome mwenyewe ili usipotezwe na hawa wenye kupanda ‘mbegu ‘, na nyote siku ya kiyama ni kilio tu kwa sababu mlipotea kwa kutoyajua maandiko wa Uwezo wa Mungu, na Quraan ikaweka wazi wale waliobadilisha aya za Allah[swt] kwa dhamani ndogo watapata adhabu kali siku hiyo,Quraan 14:21-22.
Waandishi wa biblia waliazimu kukuhakikishia kuwa miujiza yote waliofanya Manabii Watukufu ni kwa uwezo wake Allah[swt], na kuwa Manabii wote hawana ujuzi ila waliofunuliwa, angalia aya zifuatazo:
1. Matendo ya Mitume 2:22
2. Yohana 5:30
3. Mathayo 20:20
4. Mathayo 24:36
Kwa baadhi ya ndugu wakristu kuuchukia Uislamu, Waislamu na Quraan ni masikitiko kwao kuamua kuwa wafuasi wa Paulo, aliye mwasisi wa ukristu na kupuuza misingi yote aliyofundisha Yesu mwana wa Mariam, na kufanya hivyo ni kujipalilia moto wa jahanam, angalia aya hizi, Matendo 26:9,II Wakorintho 11:14-15, II Wakorintho 11:16-20 na II Wakorintho 12:16, Paulo mwandishi asema bila kuficha kuwa aliwapata wakristu kwa HILA, na hawa wa leo bado wanaendeleza matumizi ya hila ili kuwapata wakristu pamoja na kuhubiri chuki dhidi ya Waislamu.
Ukweli ambao wakristu hawaambiani ni kuwa hakuna andiko hata moja linalo tia nguvu Ukristu au wakristu, ila wameshikilia fikra za Paul kuwa atawafundisha mambo matano kwa akili zake ili na hao viongozi wa makanisa wakafundishe maneno elfu kumi kw akili zao, I Wakorintho 14:19!. Ukweli wa biblia ambao haupingiki ni kuwa Yesu mwana wa Mariam alitumwa kwa wana wa Israeli tu, na hawa wakubwa wenu wamewafanya vitega uchumi kwa , lakini wasia wangu kila kumbuka maandiko haya:
1. Mika 5:2
2. Mathayo 15:21-26
3. Mathayo 10:23
4. Mathayo 19:27-30
5. Ufunuo 21:9-14
Demokrasia wenyewe wameieleza kama uhuru wa maoni, mtu/watuwaweza kujieleza na kuwalingania watu kwa jambo Fulani ambalo laweza kuwa la kheri au shari, na nijukumu lako kuamua utaeneza kheri au shari, lakini yasikitisha wengi wameamua kueneza shari kwa faida zao huku wakisingizia eti wanamhubiri Yesu mwana wa Mariam. Mtu msomi ni Yule anaye mjua Muumba wake, Mitume yake na kuwaheshimu, na jambo la tatu ajue Dini yake sawasawa kwa dalili za kitabu kitukufu wala si kwa maneno ya kijanja, na ikiwa atafundisha bila ujuzi na elimu nzuri, 1. Atawazuia watu na njia yake Allah[swt], 2.

Ataigeuza ile njia sahihi kwa kuleta mafundisho ya uwongo, na Mithali 30:5 imeshawaonya, 3. Bila elimu sahihi utayageuza maneno matukufu ya Allah[swt] kama walivyo fanya mayahood na manasara, Quraan 9:30.
Kuwa na imani ni kutafuta akida inayoweza kujibu maswali na shida kwa hali zote, ili huyu mwanadamu aweze kutulia kiakili. Matokeo yake ni mtu mwenye mafikirio mema, anao ufahamu mzuri, kwa hivyo aweza kuchanganua mambo na kufikia uamuzi sahihi. Mtu aliye amini kisawa na anao usomi na hekima, akili yake siyo finyu, anayo maono naufahamu utakaomletea heshima na sharafu, ni mpole.

Elimu inaondoa unafiki, kibri, jeuri na huyu aliye elimika atafanya kila kitu kwa ajili ya Allah[swt], haya ni kinyume kabisa katika ukristu, kila mmoja anajiona kuwa bora kulikoni wengine. Mtu msomi ameelezewa kuwa mtu aliyeenda shule,chuo cha ujuzi ili kujipatia maarifa au ujuzi, kwa hivyo kusikia mtu aliyefikia kiwango cha “Dr”, na anasema Yesu mwana wa Mariam ndiye Mungu, basi elimu yake tutaitilia shaka kubwa, na atakuwa jeuri, na Marian Webster Dictionary wameeleza ujeuri kuwa:
1. Kukosa elimu/ujuzi juu ya jambo Fulani
2. Kuonesha kutokuwa na elimu,ujuzi,maarifa yoyote na kuupuza dalili za wazi na kweli.

Quraan imetaja neon maradhi na maana mbili, maradhi ya nafsi na yale ya kimwili, na tafsir ya Ibn Kathir imetaja hayo maradhi ya nafsi ni unafiki,hasadi,zinaa Quraan 33:32,Riyaa na Zaburi 10:3 imetaja hivi:

1. Akusamehe maovu yako [ Maradhi ya nafsi ]
2. Akuponye magonjwa yako yote [maradhi ya kimwili ]
Hizi ni baadhi tu ya kuwa Muislam, kuyafahamu mambo kwa haraka, twawakaribisha ndugu wakristu wote , lakini kwa khiari zao si kwa lazima, Quraan 2:256.

IMETAYARISHWA NA
ADAM AMBETSA
MWEMBE TAYARI TABLIGH GROUP
MOBILE NO. 0723 17 41 54
MOMBASA, KENYA.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.