0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

JE YESU ALISULUBIWA NA KUFA MSALABANI?

JE YESU ALISULUBIWA NA KUFA MSALABANI?

Wengi katika ndugu wakristo hufikiri Nabii Yesu[as] ndiye aliye kuja na msalaba kwa hivyo wakautukuza mno hadi wengine kudai msalaba waweza kuokoa jambo ambalo si kweli hata kidogo. Ni kwa hili ndipo sisi kama waislamu tukaona umuhimu wa kutafuta ile kweli na kuufahamisha umma ambao unajiangamiza kwa fikra ,au akida isiyo kuwa ya kisawasawa .

Quran na baadhi ya maandiko ya Biblia yaliyo salimika yanaafikiana kuwa msalaba ni alama ya laana na si vyema kujihusisha nao kwa ushahidi ufuatao:

1.Torati 21:22-23
2.Yoshua 10:26-27
3.Esta 9:24-25
4.Quran 5:33-34
5.Wagalatia 3:13-14
1.Quran 3:54-56
2.Yohana 11:45-52
3.Quran 4:155-156
1.Quran 4:157-158- Allah andhibitisha wazi kuwa Nabii wake hakufa kifo cha laana
2.Mathayo 26:24-25-majuto kwa msaliti
3.Mathayo 27:27-29 –vazi jekundu
4.Marko 15:16-18 vazi la rangi ya zambarau
5.Mathayo 27:45-46 saa sita Yesu yuko msalabani
6.Yohana 19:14-15 saa sita Yesu yuko mahakamani
7.Marko 15:25 saa tatu asubuhi Yesu ameshasulubiwa

ISHARA YA NABII YESU
1.Mathayo 12:38-40 ishara ya nabii Yona ni ipi
2.Yona 2:1-2 Yona aliomba ndani ya tumbo la samaki
3.Yohana 19:3-35 maiti aweza kuvuja damu?

MWISHO WA YUDA ULIKUWAJE?
1.Mathayo 27:3-7 Yuda alienda akajinyonga?
2.Matendo 1:16-19 Yuda alianguka kwa kasi akapasuka tumbo?

WALIOENDA KABURINI NI WANGAPI?
1.Mathayo 28:1-2 wanawake walio enda kaburini ni Mariamu Magdalene na Mariamu Yule wa pili
2.Marko 16:1-walio enda ni Mariamu Magdalene,Mariamu mamaye Yakobo,naSalome
3.Luka 24:1,10 walioenda kaburini ni Mariamu Magdalene,Yoana,Mariamu mamaye Yakobo na wale wanawake wengine waliokuwa pamoja nao
4.Yohana 20:1-2 Mariamu Magdalene peke yake alikwenda kaburini
5.Luka 24:36-40 ushahidi kuwa Nabii Yesu hakusulubiwa
6.Quran 2:119-120
7.Quran 2:111 -changamoto kwa ndugu wakristo wadhibitishe kifo cha Nabii Yesu
Paulo aliye muasisi wa ukristo,aliwachanganya wakristo akisema usipo uamini msalaba huwezi kamwe kuokoka 1 wakorintho 15:14,jambo ambalo si kweli.

Mwandishi wa kikristo asema kwenye kitabu chake “The Crucified God”
“Kifo cha Yesu msalabani ndicho kiini cha ukristo wote ……………………mazugumzo yote ya kikristo kuhusu Mungu,uumbaji ,dhambi,na kifo zote zina chimbuko katika Yesu ‘aliyesulubiwa’.Mazungumzo yote ya kihistoria, kuhusu kanisa, imani ,kutosheka na kuhusu mambo yajayo ,kuhusu tumaini,yote yameitikadiwa kwenye kusulubiwa kwa Yesu”……………..Prof. Jurgen Moltmann
Naye mwandishi mwingine Josh Mcdowell katika kitabu chake kiitwacho ”The Ressurection Factor” asema”Nililazimika kwenye uamuzi kufufuka kwa Yesu huenda ni uwongo,ukora ,ujanja uliopangiliwa na kuingizwa kwa bongo lamwanadamu,au ni tukio kubwa la kihistoria”
Yote haya yanadhibitisha wazi msalaba ni upotofu mkubwa kwa wanadamu.

IMETAYARISHWA NA :
ADAM AMBETSA
MWEMBE TAYARI TABLIGH GROUP
MOBILE NO. 0723 17 41 54
MOMBASA, KENYA.

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.