0%

https://uongofu.com/wp-content/uploads/2021/06/services-head-1.png

MATENDO YA MAHUJAJI SIKU YA ARAFA (SIKU YA TISA YA MFUNGOTATU)

SOMO LA FIQHI

1. Jua linapo chomoza siku hii ya tisa mahujaji wataelekea Arafa na huku wakileta talbiya

لبيك اللهم لبيك

[labbayka allamuhmma labbayka]

Na ni sunna kukaa (Namirah) mpaka jua lipinduke na kuingia wakati wa Adhuhuri, na wakati unapo ingia ni sunna kwa kiongozi wa kiislamu au naibu wake awahutubie mahujaji hutuba yenye kunasibiana na hali yao, awakumbushe kumpwekesha Mwenyezi Mungu na awafunze hukumu za hijja na mambo muhimu kuhusu dini yao.

2. Kisha atawaswalisha Adhuhuri na Alasiri kwa kuzikusanya, kutanguliza na kuzipunguza.

3. na sunna kwa Haji siku hii aelekee kibla, na azidishe kumuomba Mungu na ajitahidi sana katika kuomba, na adhihirishe unyonge wake na udhaifu wake na kumuhitajia kwake Mwnezi Mungu ﷻ na akariri maombi.

Amesema Mtume ﷺ:

خير الدعاء دعاء يوم عرفة ، وخير ما قلت أنا والنبيّون من قبلي : لا إله إلا الله وحده لا شريك له ، له الملك ، وله الحمد ، وهو على كل شيء قدير      رواه الترمذي

[Dua bora ni dua ya siku ya Arafa, na maneno bora niyale niliyo yasema mimi na manabii kabla yangu: hapana mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi mungu pekeyake hana mshirika ufalme ni wake, na kusifiwa ni kwake yeye, na yeye ni muweza wakila kitu]   [Imepokewa na Tirmidhi]

na afanye pupa kuomba dua zilizopokelewa kwa Mtume  na ajiepushe na dua ya kujikalifisha, na asome Qur’ani kadiri anavo weza, na akithirishe kumswalia Mtume .

4. Baada ya jua kuzama muhujaji wataondoka kutoka arafa wakielekeya Muzdalifa na haifai kuondoka kabla ya kuzama kwa jua, na akiondoka kabla kuzama kwa jua itamlazimu arudi hata kama ni usiku na asiporudi itamlazimu yeye damu kuchinja nayo ni kuchinja mbuzi au fungu la saba la ngamia ama fungu lasaba la ngombe

na nisunna kwa mahujaji kuondoka kwa utulivu na upole bila ya kuwaudhi watu, na aondoke hali ya kuleta talbiya na kumtaja mwenyezi mungu  .

Toa maoni yako

Begin typing your search above and press return to search.